Madaktari waliofukuzwa waula Namibia, Botswana, Rwanda na A.Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari waliofukuzwa waula Namibia, Botswana, Rwanda na A.Kusini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MKL, Jul 18, 2012.

 1. MKL

  MKL Senior Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 126
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Balozi za nchi hizo tajwa zimetoa ofa nono kwa madoctor woote waliofutiwa lesseni na wizara ya afya na TZ kwa ngazi zoote kuanzia seniors hadi intern, Intern wataandikishwa kama intern pindi wakifika kwenye nchi husika chini ya uangalizi wa Senior Doctors huku wakipewa mishahara na marupurupu yakuwatosha na wakimaliza shule wanapewa vyeti na lesseni za udoctor wa nchi walipo.

  Wale masenior ambao wamenyang√°nywa lesseni wao wakifika wanaandikishwa kwenye chama cha madoctors wa nchi husika na kupewa lesseni mara moja na kupangiwa kazi ikiambatana na haki zoote wanazostahili.

  Balozi za nchi hizi zinawaomba madocta woote wajiandikishe tayari kuajiriwa kwenye nchi watakazo kati ya hizo tajwa.
  haya sasa kwa mara ingine tena TZ inaelekea kupoteza Brain zake kwa kile kinachoitwa mgomo ili hali walipa kodi wanateseka kwa kukosa watabibu.

  Masini nchi yangu itatuchukua muda gani kuwapata madoctor kama hawa tena kama kweli wakiitikia mwito wa nchi hizi na wakaondoka.....?

  Source: Raia Mwema Leo 18/07/2012 page 3
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mpaka pale tutakapoancha kuwaabudu wanasiasa kwa kuamini ndiyo solution ya matatizo yetu, na kuweka mfumo unaomthamini kila mmoja ndipo tutaona umuhimu wa watu wanaosotea fani zao kwa miaka rudi huku wakihatarisha mambo mengi.
   
 3. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,367
  Likes Received: 8,382
  Trophy Points: 280
  Mungu okoa hii nchi plz Sir God
   
 4. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Serikali hainifu, haijali rasilimali zake.
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  waache waende maana tanzania kinachofanyika ni kuwasomesha na wakihitimu wanafukuza........mdogo wangu alishafika rwanda na tayari kazi alishapata ni miongoni mwa wale waliotimuliwa mbeya ....
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Bora waende wakafie mbele sasa kama walikuwa na hiyo option kwanini walikuwa wanagoma? si wangeacha kazi kimya kimya wakaenda huko kwenye mafano manono?
   
 7. D

  Dina JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ilionekana kama utani na masihara, bila kusahau maamuzi ya jeuri na vitisho, lakini impact yake ni kwa sisi wananchi wenyewe......Haya nendeni bwana, manake sisi kama sisi hatuna jinsi ya kuwazuia.
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kwanini daa tuwafutie ubalozi woote watakaowaiba madr wetu!
   
 9. only83

  only83 JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Ni udhaifu wa serikali ya Chama Cha Madhaifu aka CCM.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  One day we will be matured enough to make decisions wisely. Kwasababu wengi hatukujua extent ya ubaya wa maamuzi tunayoyafanya pengine tulidharau uwezo na umuhimu wa madaktari.
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nabii siku zote hatambuliki kwao. Sioni sababu ya serikali kuamua kutunishiana misuli na watendaji wake. Serikali inaogopa pale itakapokubaliana na madaktari, basi walimu, wazee, trl, na wengine wataidai serikali. Kama serikali yc ccm ndio inachotaka basi itakipata soon
   
 12. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  "Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo." (JK et al., 2012)
   
 13. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Uzalendo huwa unauma sana, usifikiri wote wanafurahi kwenda huko. Ni ujinga wetu. Sasa na sisi tukachukue wa Africa kusini tuwalete.

  RIP CCM
   
 14. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  labda watajitetea kuwa walitaka watusaidie sisi ndugu zao!
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Tumewasomesha ili wakafanye kazi huko! hatuna haja na madaktari, tuna waganga wa kienyeji kibao
   
 16. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,377
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Tanzania kushney!
  Safi sana ila muda si mref serikali ita anza kulia na kupiga magoti
  iwarudishe!!!
   
 17. m

  mariavictima Senior Member

  #17
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mungu awabariki Ma-DR. Nendeni mkatafute maisha bora sehemu yenye maslahi na mazingira bora ya kazi. Sisi tutaendelea kwenda kwa Babu Loliondo mpaka tutakapofunguliwa kujuwa umuhimu wa Ma-Dr.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ni kiburi tu cha wanasiasa; wanafikiria udaktari ni "kama fani nyingine" tu. Gharama ya madaktari wetu kuondoka ni kurudisha huduma ya afya kwa miaka kadhaa nyuma. Lakini kwa vile tatizo lenyewe halijashughulikiwa bado kutakuwa na mgongano wa madaktari na serikali in the future. Hii yote ni matokeo ya sera zilizoshindwa za CCM.
   
 19. d

  dandabo JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Porojo hizi sasa zinakera. Ndugu wengine tunafanyakazi kwenye mojawapo ya balozi ulizotaja. Acha uongo, si tabia nzuri!
   
 20. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu! Jk aliongea kwa hasila si wakumsikiliza sana tuangalie kanchi ketu kenyewe haka matatizo ni mengi tumsaidie jk!
   
Loading...