Madaktari waliofukuzwa sasa kuhojiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari waliofukuzwa sasa kuhojiwa

Discussion in 'JF Doctor' started by sir.JAPHET, Aug 10, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Thursday, 09 August 2012 21:32

  Geofrey Nyang’oro
  MADAKTARI waliofukuzwa kazi na wale waliositishiwa leseni za muda wanatarajia kuanza kuhojiwa wakati wowote na Baraza la Madaktari Tangayika (MCT).
  Katibu wa Jumuiya ya Madaktari inayoshughulikia madai ya madaktari ambayo pia iliratibu mgomo huo, Dk Edwin Chitage aliliambia gazeti hili jijini Dar es Salaam kuwa madaktari wanasubiri utekelezwaji wa hatua hiyo.

  Alisema Jumuiya pamoja na Chama cha Madaktari nchini (MAT) watachukua hatua zaidi baada ya kuona utekelezaji wa hatua hiyo ambayo itatoa mwanga juu ya mwelekeo wa Serikali katika kutatua mgogoro baina yao na Serikali.

  “Tuna taarifa kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inakusanya ushahidi na kila daktari kwa waliofukuzwa na waliositishwa usajili wataitwa na kuhojiwa mmoja mmoja na Baraza”, alisema Dk Chitage na kuongeza:

  “Kufuatia hatua hiyo Jumuiya ya Madaktari imejipanga kukabiliana na tukio hilo kwa kufuata taratibu za kisheria.

  (MCT) ina sura ya mahakama na kimsingi inastahili kufanya kazi kwa sura hiyo, sisi tumejipanga, yapo mambo ya kisheria itabidi tuyafanyie kazi”alisema.

  Akizungumzia afya ya Dk Stephen Ulimboka anayeendelea na matibabu nchini Afrika Kusini alisema kwa sasa imezidi kuimarika ingawa siku rasmi ya kurejea nchini haijajulikana.

  “Afya ya Mwenyekiti wetu (Dk Ulimboka) inaendelea vizuri, lakini tarehe ya kurudi bado haijajulikana,tukipata taarifa hizo tutasema,”alisema.

  Katika hatua nyingine katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dk Rodrick Kabangila alisema madaktari hawana imani na MCT kwa kuwa haiwezi kutenda haki katika shauri hilo.

  Alisema sababu ya kukosa imani inatokana na baraza hilo kuundwa na Serikali.

  Baraza la madaktari Tanganyika (MCT) ndilo linaloshughulika na usajili wa madaktari na mwenyekiti wake kimuundo ni Mganga Mkuu wa Serikali.
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hivi ukinifukuza kazi halafu ukaniita kunihoji utakuwa unanihoji nini??
  Hizi ni sheria za wapi zinazofuatwa hapa!

  Haya mazingaombwe haya ndo maana hatuendelei wala nini!!
   
 3. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Pamoja na mfumo m-bovu wa kimahakama unaopendelea serikali, acha tu watu wa MAT wajipange hivyohivyo ingawa nawashauri wajiandae kupokea kilichopangwa kuamuliwa na serikali ya ccm na sio mahakama. USHAURI WANGU KWA WATANZANIA; TULIONDOENI HILI LI-SERIKALI, LIMESHAJIGEUZA ZIMWI, LITATUMALIZA.
   
 4. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kuhojiwa na kisha kutekwa mmoja mmoja, wanataka kupunguza hela za safari za mkulu.?
   
Loading...