Madaktari walioajiriwa wametoswa?

moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,555
3,536
Wale madaktari walioajiriwa siku chache zilizopita tulitangaziwa wataripoti vituo vya kazi kuanzia juzi Jumatatu(24/4/2017). Sasa huku Tabora mbona hakuna aliyekwisharipoti? Hata kwa mikoa ya jirani nimejaribu kuulizia nao hakuna aliyekwisharipoti.

Au tuamini hizi tetesi ya kwamba wanasubiri hadi mwaka ujao wa fedha?
 
waziri wa afya si alisema mtukufu atawalipa mwenyewe sio mfuko wa serikali
kwan wewe ushasikia matamko mangapi kutoka kwa viongozi wako na hakuna ambalo limefanywa!!!
we subiri bajeti.. hao mawaziri siku hz waropokokaji tu..!!!!
 
Wale madaktari walioajiriwa siku chache zilizopita tulitangaziwa wataripoti vituo vya kazi kuanzia juzi Jumatatu(24/4/2017). Sasa huku Tabora mbona hakuna aliyekwisharipoti? Hata kwa mikoa ya jirani nimejaribu kuulizia nao hakuna aliyekwisharipoti.

Au tuamini hizi tetesi ya kwamba wanasubiri hadi mwaka ujao wa fedha?

Kwa Mara ya kwanza nimeamini kuwa hii serikali ni ya kisanii sana...walisema jumatatu mi siku ya kuripoti ila Mpaka wikiendi inaisha kulikuwa Hamna taarifa.
Jana Niko kwenye mizunguko yangu nikaamua nipite pale wizarani posta.... Niliishia kuzungushwa tu, nilipitishwa karibu ofisi zote hadi ya chief medical officer Na kwa hakika kila mmoja hakuwa Hata Na taarifa juu ya ajira hizo, yani wizara Mzima hakuna anayejua lolote kuhusu hizo ajira. Sikuamini macho yangu...nikajiondokea
 
Hivi kama hawa 250+ tuu uzungushwaji ni wa namna hii vipi zile intake mbili, wanaofanya kuwa na madaktari kama 1700+ mtaani wataajiriwa kweli?

Back
Top Bottom