Madaktari wa Mwakyembe kuamua!

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,507
11,883
Madaktari wanaomtibu dr mwakyembe apollo-india wataamua kama wataendelea na matibabu au arejeshwe nyumbani!hivyo kusubiri uamuzi wa mungu kumponya au laa
 
Mkuu toa taarifa kamili! tunahitaji kujua hali ya Dr. ni moja ya watu waliowezesha mabadiliko makubwa nchini kutokana na kazi zao, najua wengi hawaamini jinsi nchi ilivyolipuka baada ya EL kujiuzuru.
 
Gazeti la mwananchi la leo nimeona kichwa cha habari kisemacho : Wiki muhimu ya Mwakyembe... Sijapata nafasi ya kusoma kilichomo kwenye habari kamili!
 
Nadhani ni muda wa yeye Naye Kwenda Kujaribu kwende Selou kwa Yule mtaalamu!!
 
Wiki muhimu kwa Dk. Mwakyembe


Madaktari wanaomtibu Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harisson Mwakyembe, wameanza kumfanyia tathmini ya mwisho ili kuamua kama aendelee na matibabu au arejee nchini.

Akizungumza na NIPASHE jana kutoka katika Hospitali ya Indraprasta Apolloa nchini India alikolazwa, Dk. Mwakyembe, alisema madaktari hao walianza kumfanyia tathmini hiyo kuanzia jana na itakamilika leo.

Alisema baada ya kukamilika kwa tathmini hiyo, madaktari wake watatoa taarifa kama amepona kabisa ili arejee nchini ama aendelee na matibabu.
Akizungumzia kuhusu maendeleo ya afya yake, Dk. Mwakyembe, alisema kuwa kimsingi inaendelea kuimarika na kwamba anachosubiri ni kupatiwa taarifa na madaktari wake kuhusu tathmini hiyo.

Aliongeza kuwa madaktari wanaomtibu wamekuwa karibu naye kwa kumpatia matibabu mazuri.
Kuondoka kwa Dk. Mwakyembe kwenda nje kupata matibabu kuliibua maswali mengi kwa wananchi, baada ya kuzuka kwa taarifa kuwa kuugua kwake kulitokana na kulishwa sumu, ambapo hadi sasa si serikali wala yeye aliyekanusha uvumi huo.

Dk. Mwakyembe alipelekwa India kupatiwa matibabu Oktoba 9, mwaka huu.
Akihojiwa na kipindi kinachorushwa na ITV cha Dakika 45, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alisema kuwa kuna uwezekano Dk. Mwakyembe amelishwa kitu kama sumu.

Sitta alisema alimwona Dk. Mwakyembe na hali aliyomkuta nayo kimsingi haikuwa nzuri kwani ngozi yake ilikuwa imeharibika na hata nywele zilikuwa zikipuputika.

KANDORO: WAOMBEENI VIONGOZI WANAOTIBIWA NJE

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewaomba wananchi wa mkoa huo na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuwaombea mawaziri, wabunge na viongozi wa kisiasa kutoka mkoani humo ambao ni wagonjwa na wanaoendelea na matibabu nje ya nchi ili wapone haraka na kurejea nchini kuendelea na majukumu yao ya kitaifa.

Kandoro alitoa ombi hilo wakati akifunga kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa Mbeya kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini hapa.
Alisema Profesa Mwandosya (Waziri wa Maji), Dk. Mwakyembe, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Nawab Mullah na Mbunge wa Viti Maalum mkoa (CCM), Hilda Ngoye, walistahili kuwepo katika kikao hicho, lakini bahati mbaya walikuwa wanaumwa na baadhi yao wapo nje ya nchi kwa matibabu.

Kandoro alisema kwa kuwa viongozi hao ni muhimu sana kwa maendeleo ya mkoa wa Mbeya na taifa kwa ujumla, wananchi wa ndani na nje ya mkoa kila mmoja kwa imani yake aendelee kuwaombea ili wapone haraka.

Hata hivyo, Profesa Mwandosya ambaye pia ni Mbunge wa Rungwe Mashariki, alirejea nchini Desemba Mosi, mwaka huu kutoka India alikokuwa akitibiwa ambako alikaa huko kwa takribani miezi mitano.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Mullah kwa takriban mwaka sasa amekuwa nje ya nchi kupatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Mullah ambaye naye amerejea nchini Desemba 4, mwaka huu akizungumza na NIPASHE alisema alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya St Elizabert iliyopo Singapore.

Alisema kwa sasa yupo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, ambako anapumuzika, kutokana na kuugua kwa muda mrefu, kazi za chama zimekuwa zikifanywa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Verena Shumbuko, ambaye pia katika vikao vya chama amekuwa akiviendesha kama Mwenyekiti wa CCM mkoa kulingana na kanuni na taratibu za CCM.

Kwaupande wake, Ngoye, akizungumza na NIPASHE kwa simu akiwa Dar es Salaam alisema anaendelea vizuri.



CHANZO: NIPASHE
 
Ndiyo, nchi ililipuka, but, in what direction?; FYI, kuna wengi walishangazwa na kusikitishwa na kitendo cha kamati kuleta taarifa ya kupika, FYI, swala la Richmond wabunge wengi walikuwa wanajua ukweli wake ambao ni tofauti na kilichoelezwa na taarifa ya Mwakyembe, so, you better read btn the lines, aliyemtumia Mwakyembe kuzungumza uongo ndiyo huyuhuyu ambaye sasa hamuhitaji Mwakyembe kwenye jukwaa la siasa.

Ukweli uko wazi lakini cha kushangaza ni kuwa bado hata GT wanadanganya jamii. Emancipate yourself from mental slavery, non but ourself can free our minds, have no fear for atomic energy cos non of them can stop the time.................................

how long shall they kill our prophets while we stand aside and look?. Wont you help to sing, the songs of freedon, its all i ever want, redemption song.
Mkuu toa taarifa kamili! tunahitaji kujua hali ya Dr. ni moja ya watu waliowezesha mabadiliko makubwa nchini kutokana na kazi zao, najua wengi hawaamini jinsi nchi ilivyolipuka baada ya EL kujiuzuru.
 
Kama kuna mtu wa karibu na Mwakyembe nashauri wajaribu hizi mbili maana zina uzoefu na hizi sumu za Urusi. Ujerumani na Austria. (sio Australia). India wana ujuzi kwenye mambo mengi lakini sidhani kama wamo kwenye hizi sumu za Puttin!
 
Ndiyo, nchi ililipuka, but, in what direction?; FYI, kuna wengi walishangazwa na kusikitishwa na kitendo cha kamati kuleta taarifa ya kupika, FYI, swala la Richmond wabunge wengi walikuwa wanajua ukweli wake ambao ni tofauti na kilichoelezwa na taarifa ya Mwakyembe, so, you better read btn the lines, aliyemtumia Mwakyembe kuzungumza uongo ndiyo huyuhuyu ambaye sasa hamuhitaji Mwakyembe kwenye jukwaa la siasa. Ukweli uko wazi lakini cha kushangaza ni kuwa bado hata GT wanadanganya jamii. Emancipate yourself from mental slavery, non but ourself can free our minds, have no fear for atomic energy cos non of them can stop the time.................................how long shall they kill our prophets while we stand aside and look?. Wont you help to sing, the songs of freedon, its all i ever want, redemption song.

wewe hujui unachokiongea my friend. eti taarifa za kupika, hujui unachokinena. mwakyembe ni mmoja kati ya watanzania walioleta mabadiliko makubwa katika nchi hii kwa kuweza kumtoa madarakani mwizi no 1 edo
 
wewe ni kibaraka wa edo. huwezi ukawa unatetea ujinga kiasi hicho . yani unataka kuhalalisha wizi alioufanya edo? hatuwezi kukubaliana na wewe katika ujinga huu unaotueleza . watanzania wanaelewa pumba na mchele ni upi. usiwafanye wa tz ni wajinga kama wewe kibaraka wa edo. endelea kukubali kushikiwa akili.
 
wewe hujui unachokiongea my friend. eti taarifa za kupika, hujui unachokinena. mwakyembe ni mmoja kati ya watanzania walioleta mabadiliko makubwa katika nchi hii kwa kuweza kumtoa madarakani mwizi no 1 edo


walewale sijui msaidiweje...ebu angalia signature yangu labda utapona

CCM iondoke madarakani wajinga nyie...
 
Wewe ndo mwenyekiti wa chama chake, jibu hoja alizozitoa kwenye kiao chenu cha DODOMA kilichopita, wajinga hujadiri watu badara ya issues. Time will be your best hakimu...... BTW, hata hujaona kuwa taarifa yake alilenga kumtetea mwizi na aliyelenga kudidimiza sekta ya nishati?, what have you improved so far kwa kusingizia kuwa EL was behind Richmond ukijua siyo kweli?!, tuko kwenye timeline, punde kitufe kitabonyezwa na tutawashuhudia mukimalizana ili ukweli usijulikane.
wewe hujui unachokiongea my friend. eti taarifa za kupika, hujui unachokinena. mwakyembe ni mmoja kati ya watanzania walioleta mabadiliko makubwa katika nchi hii kwa kuweza kumtoa madarakani mwizi no 1 edo
 
Back
Top Bottom