Raia mwema
Nchem Nchicheme? Novemba 14, 2007
KWAMBA kuna daktari mmoja au wawili, au watatu wamefanya uzembe wa hatari kwa maisha ya mgonjwa, hakuna mjadala. Hakika, uzembe uliosababisha mgonjwa wa mguu kufumuliwa kichwa ungetakiwa uwe simulizi ya kuchekesha na kuchangamsha baraza, lakini kwa bahati mbaya unahusu maisha ya binadamu, kwa hiyo hatuwezi kucheka.
Shauku iliyozushwa na sakata hilo, pia inaeleweka, kwani wananchi wanayo sababu ya kuingiwa na woga kwa kuwa hawajui wakimbilie wapi, iwapo kituo cha kuwaponya kimegeuka kuwa kituo cha maafa makubwa kuliko waliyokuja nayo.
Hatua zinazochukuliwa ili kuwabaini waliofanya uzembe huo, pia ni muhimu, kwani si sawa kuachia uzembe kama huo ukaonekana kama jambo la kuzoeleweka.
Hata hivyo, ingefaa tujisaili sisi sote, tupate kujua kama uzembe wa aina hii ni wa hospitalini pekee au ni aina ya saratani iliyotapakaa katika jamii yetu kwa ujumla.Ni kweli kwamba mgonjwa anapokuwa katika matibabu anakuwa amejikabidhi yeye na roho yake moja kwa moja kwa daktari na wauguzi. Maisha yake yanakuwa mikononi mwao, na kupona ama kufa, tukiacha amri ya Mwenyezi Mungu, itategemea wanafanya nini na mgonjwa huyo.
Lakini wako watu wengi ambao tumejikabidhi kwao, nao wanaamua juu ya maisha yetu, kufa au kupona, hata kama kazi zao si nyeti kama za madaktari na wauguzi, na kila siku tunashuhudia jinsi wanavyotumaliza.
Mfano mdogo tu ni uzembe wa madereva ambao wamekuwa wakichinja watu kwa makumi, kiasi kwamba tumekuwa kama tumepigwa ganzi: hata kuomboleza kumepungua isipokuwa tu akifa mtu mkubwa katika ajali.
Yapata miaka kumi iliyopita watu wakaribiao elfu walipoteza maisha katika meli mv Bukoba, lakini hatukumsikia kiongozi hata mmoja akikubali uwajibikaji na kujiuzulu kwa kukiri kwamba kwa njia moja au nyingine alihusika na uzembe uliosababisha vifo hivyo vya halaiki.
Baada ya mv Bukoba ni vigumu kufikiria ni tukio gani jingine linaweza likatushtua kama Taifa kiasi cha kusema, basi!
Tunayo haki ya kuwalaumu madaktari na wauguzi kwa uzembe wao unaohatarisha maisha ya wananchi, lakini tusiishie hapo. Hivi, askari wa usalama barabarani anayeacha magari yanakwenda kwa kasi ya kutisha hadi yanapinduka, hahusiki na vifo vya abiria?
Na je, mtendaji wa serikali anayeiingiza nchi katika mikataba inayoinyima mapato halali ambayo yangetuwezesha kununua dawa za kutibu watoto wanaokufa kwa malaria, hahusiki na vifo vya watoto hao? Ni swali linaloweza kuulizwa kuhusu kila eneo la maisha ya nchi yetu, kwa sababu uzembe umetapakaa kila kona.
Hapa nafikiri kuna hoja.
Sijasikia watu wakiogopa kupanda daladala au mabasi ya abiria.Kama Mnakumbuka wiki kama mbili zilopita pale Ubungo Stand ya Mkoa,nusura abiria wawapige polisi wa usalama barabarani walipotaka kusimamisha mabasi ya abiria yaendayo mikoani yaliyobainika kubadilishwa au kuwa na mashine na vipuri vya maroli.Hapa kweli kuna kazi