Madaktari msiwasikilize wanasiasa, jitafutieni taarifa wenyewe

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
Madaktari mnaoomba kwenda Kenya ni vema kwanza mtafakari sababu za ghafla za serikali ya Kenya kutaka madaktari 500. Hamtakuwa salama huko Kenya kama sababu za kuwahitaji ni za kisiasa. Mkumbuke pia maombi hayo yamekuja baada ya mgomo wa madaktari wa huko, na inasemekana kuna madaktari 1400 nchini Kenya ambao hawana ajira rasmi.
Kwa hiyo kabla hamjaomba kwenda Kenya, mjiridhishe.

NB: Msiwasikilize wanasiasa, jitafutieni taarifa wenyewe.
 
Na hiyo ajira si ya lazima bali ni hiari kama mtu anapenda kuomba aombe na asiyependa aache
 
aisee 4M plus accomodation while kwa bongo unapewa 1.5M without accomodation,

Hili halihitaji akili ya ziada,unakwenda tu!
 
Lengo ni zuri sana lakini Ukweli mazingira ya kule itakua kasheshe manake wale wakenya wataona mnaenda kuwasaliti ili serikali yao isitimize ahadi au makubaliano yao,,,suala la usaliti liko sana hapa bongo na kwa kweli huwa halina issue saaana ila kule kenya ukweli ni mambo tofauti kabisa wale jamaa wana hasira kali na wanaweza kufanya kitu kibaya ila kwasababu wameahidiwa ulinzi wataamua wenyewe...na unajisikiaje kutokua huru katika nchi isiyo yako...mazingira mageni ni kitu kigumu sana hiki...
 
Back
Top Bottom