Madaktari leo kujadili sakata la Ulimboka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari leo kujadili sakata la Ulimboka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by richone, Aug 7, 2012.

 1. r

  richone Senior Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  WAKATI kukiwa na taarifa za kurejea nchini kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka viongozi wa Jumuiya hiyo na Umoja wa Madaktari Tanzania (MAT), wanatarajia kukutana leo kujadili mkanda mzima wa sakata lililomkumba kiongozi huyo. Baada ya kikao hicho, madaktari hao watakutana na familia yake na kisha kumuuliza Dk Ulimboka kama angependa kilichomtokea kiwekwe wazi kwa jamii. Dk Ulimboka ambaye alikuwa anaratibu mgomo wa madaktari uliokuwa ukiendelea nchi nzima, alitekwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumatato ya Juni 27 mwaka huu na kupelekwa katika msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji a Dar es Salaam, ambako aliteswa na kujeruhiwa vibaya. Katika tukio hilo daktari huyo aling'olewa meno mawili na kucha za mkono mmoja na baadaye kulazwa katika Kitengo cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalum (ICU) katika Taasisi ya Mifupa (MOI).

  Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya Juni 30 mwaka huu, alisafirishwa kwenda Afrika a Kusini kwa ajili ya vipimo na matibabu. Kusafirishwa kwake kulifuatia taarifa ya jopo la madaktari lililokuwa linamhudumia kutoa taarifa kwa madaktari bingwa kuhusu abadiliko ya afya. Taarifa za kurejea kwa Dk Ulimboka zimezagaa katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam, huku baadhi ya watu wakizijadili katika mitandao ya kijamii. Akizungumza na gazeti hili Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Edwin Chitage, alisema kuwa hali ya Dk Ulimboka inazidi kuimarika lakini alisita kueleza wazi ni lini kiongozi huyo wa madaktari atarudi nchini. "Tukiwa tayari tutatoa taarifa katika vyombo vya habari juu ya suala zima la afya ya Dk Ulimboka," alisema Dk Chitage. Alisema leo au kesho viongozi mbalimbali wa MAT na Jumuiya ya Madaktari, watakutana kujadili suala la kiongozi huyo. "Ndani ya siku mbili hizi (leo na kesho) viongozi tutakutana na kujadili ripoti ya matibabu ya Dk Ulimboka na tutajadili kama tuvieleze vyombo vya habari ama laa," alisema Dk Chitange.

  Hata hivyo Dk Chitange alisema hatua hiyo itategemea na kauli ya familia ya Dk Ulimboka na yeye mwenyewe (Dk ULimboka) kwa kuwa na wao pia watashirikishwa. "Dk Ulimboka na familia yake tutawashirikisha katika mambo ambayo tutayajadili," alisema Dk Chitage. Alipoulizwa kama kiongozi huyo wa madaktari sasa anaweza kufanya shughuli zake kama awali, alisema hana uhakika kwa kuwa hana taarifa za ndani zaidi .
   
 2. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wangesema tu tuone Ikulu watajifichia wapi!!!
   
 3. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,092
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  apone kwa kweli
   
 4. I

  IDIOS Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mm nngependa waiweke wazi tasrifa hyo ili umma uelewe hasa ni kitu gani kilichotokea.

  Hapo tutaona kama na wao watawafungia kama mwanahalisi walivyolifanyia.

  Ni aibu kubwa kwa watawala wetu.
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  MAT,Hili swala lipo mahakamani.
   
 6. maria pia

  maria pia JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 516
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  yaan ulimboka akikaa kimya nitamshangaa!...yale ya mwakyembe ctaki kuyasikia
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160

  Kwani wewe umekuwa gazeti? Mbona maneno haya yanaonekana wazi umetoa kile ulichokisikia tu mitaani? Familia ya Ulimboka haina msemaji wa Familia mpaka Madaktari waongee kwa niaba yao, kwa sababau naona kama kikao hicho ni cha familia.
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Sasa kama ukweli unatengenezwa unafikiri atasema nini. Yule ni Daktari, siyo kama Kubenea ambaye akisikia hata Ndege akilia anatafsiri na kuandika.
   
 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hata kama lisingekuwa mahakamani, halina mvuto tena kwa sababu yule mtengeneza uongo kishapigwa stop.
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kuna ukweli ambao utazidi, ule uongo uliotengenezwa na CDM kupitia gazeti la Mwanahalisi? tehe tehe tehe , yangu macho is CDM vs government under the shadow of Ulimpoka and Said Kubenea. Nasikia CDM hivi
  sasa wanapita uswazi angalau kupata taarifa zaidi zinazohusu kutekwa kwa Ulimboka.
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kwani Ulimboka hana kzi? Yule alishawatemesha Madaktari wenzake Serikalini yeye anakuja kupeta tu, anakuja kula bata kwa pole kibao huku watoto wa wenzake wakijuliza watakula nini baaba ta wazao wao kudanganyika na kugoma. Sijui wale ndugu wa marehemu waliofariki kutokana na mgomo watamuelewa vipi huyu Uli. Itabidi apewe ulinzi otherwise atakuwa na maadui wengi.
   
 12. m

  malaka JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Waseme tu hili Jeshi sio la kuliamini kabisa hili bora mtu ujulinde mwenyewe tu.
   
 13. t

  thatha JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  wajadili tupate maendeleo ya uli,sio kulishwa makasa na sadist kubenea
   
 14. K

  Kichiringa Member

  #14
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aeleze ukweli tuuuuu...

  LIWALO NA LIWE.
   
 15. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hivi hawa Madaktari vipi?, yaani hadi leo bado WANAJADILI sakata la Dr. Ulimboka? It is time now for ACTION NOT FOR TALKS.

  Serikali iumeunda kangaroo tume ambayo hata mtoto wa STD I hawezi kuikubali.

  Madaktari wanachotakiwa kufanya sasa hivi ni kuji-organise kwa KUSHIRIKIANA na Watanzania wanaoitakia nchi hii mema, kuwaita SCOTLAND YARD kufanya uchunguzi HURU sambamba na hiyo kangoroo tume ya Msanii Kova.

  Wazalendo wa nchi hii tutachanga kwa hali na mali kuhakikisha SCOTLAND YARD inatua hapa nchini na kutufanyia uchunguzi ambao hautaacha hata punje ya masahaka na kuuweka hadharani.

  Plese Madaktari tunataka Scotland yard watufanyie uchunguzi huru wa kutekwa na kuteswa kwa Dr. Ulimboka.
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada anasema watu wasiojulikana ndo walimteka dr Uli,,,,,,,,ni kweli hawajulikani?????
   
 17. m

  matawi JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  nimetafuta kitufe cha dislike sijakiona
   
 18. j

  joneslubinza Member

  #18
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwavile swala la Ulimboka limegubikwa na utata si vizuri kuendelea kulijadili hadharani. Madaktari walijadili kwa tahadhari maana kilichomsibu mwenzao bado kiko palepale( wabaya wao) !
   
 19. i

  ishisabita Member

  #19
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo umenena
   
 20. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #20
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa ndo nimeelewa kwani serikali ililifungia gazeti kwa muda usiojulikana, Dr akisema tu kilicho mtokea utasikia wanalifungulia gazeti hasa kama kile kilicho andikwa na Mwanahalisi kitafanana na atakachokisema Dr. nchi ya maajabu hii.
   
Loading...