gango2
JF-Expert Member
- Aug 31, 2011
- 1,942
- 2,251
WanaJF
Habari zenu,
tafadhari hili jambo sio la mzaha, kweli madaktari wanamadai (kama ya msingi haya kama sio ya msingi sawa), lakini lazima tukubali kuwa mgomo sio suruhu wa matatizo jamani, watu wanakufa mahospitalini, najua kuna watu humu ndani wanashabikia sana mgomo, ukweli ni kuwa wengi wetu tulio na uwezo hata wa kubrows net tunaweza kuenda Marie stopes, mikocheni shop au hospital nyingine yoyote ya private.
Leo nimetembelea pale mwananyamala na amana hali ni mbaya jamani, watu wanakufa ambao wanaweza kupona kama watapata huduma, hebu try to imagine umempeleka mzazi wako hospital (mama au baba yako) kisha unafika pale unapewa kauli na muhudumu bora afe mbona wengi wamekufa toka asubuhi utajisikiaje??
Tusishabikie mgomo kwa kuwa tunauwezo wa kwenda private hospital hebu fikiria Yule asiyeweza kwenda private anavyo umia. Leo humu kuna watu wanajifanya wanadiriki kushabikia mgomo kwakuwa wapo wazima na hawaumwi lakini kumbukeni kuna watu wako serious wanahitaji huduma ya haraka.
Hiki ni kipindi cha soko huria, mi nafikiri ukiona huridhiki na mshahara wa selikarini ni vizuri ukatafuta kazi private sector, kuliko kuomba kazi kisha hutaki kufanya kazi eti unagoma kudai mshahara zaidi
Madaktari msitumie umuhimu wa taaluma yenu kuwaadhibu watu wasio na hatia, hebu kuwani na moyo wa huruma. Kwani hayo mzingira bora ya kazi mnayodai si huko nyuma yalikuwa hivyo hivyo, mbona walimu wanapelekwa vijijini wanajitahidi na wale wanaoshindwa wanaacha kazi.
Najua kuna watu wao kazi yao kushabikia tuu tena ushabiki usio na maana!! Hebu katika hili tusiwe kama watoto wadogo, lamsingi warudi hospitalini kufanya kazi zao, hoja kuwa udaktari ni kazi sana kuusomea haina tija, tena ni sababu dhaifu sana kwenu, watu wengine mbona waliona bora wasomee fani nyingine ili kuondoa kadhia kama hizi kwa wagonjwa sasa nyie mliopewa nafasi msitutese bila sababu ya msingi>