Madaktari huu ni ubinafsi, wekeni uzalendo mbele acheni maslai binafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari huu ni ubinafsi, wekeni uzalendo mbele acheni maslai binafsi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by gango2, Jun 29, 2012.

 1. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,224
  Likes Received: 446
  Trophy Points: 180
  WanaJF
  Habari zenu,  tafadhari hili jambo sio la mzaha, kweli madaktari wanamadai (kama ya msingi haya kama sio ya msingi sawa), lakini lazima tukubali kuwa mgomo sio suruhu wa matatizo jamani, watu wanakufa mahospitalini, najua kuna watu humu ndani wanashabikia sana mgomo, ukweli ni kuwa wengi wetu tulio na uwezo hata wa kubrows net tunaweza kuenda Marie stopes, mikocheni shop au hospital nyingine yoyote ya private.


  Leo nimetembelea pale mwananyamala na amana hali ni mbaya jamani, watu wanakufa ambao wanaweza kupona kama watapata huduma, hebu try to imagine umempeleka mzazi wako hospital (mama au baba yako) kisha unafika pale unapewa kauli na muhudumu ‘bora afe mbona wengi wamekufa toka asubuhi’ utajisikiaje??  Tusishabikie mgomo kwa kuwa tunauwezo wa kwenda private hospital hebu fikiria Yule asiyeweza kwenda private anavyo umia. Leo humu kuna watu wanajifanya wanadiriki kushabikia mgomo kwakuwa wapo wazima na hawaumwi lakini kumbukeni kuna watu wako serious wanahitaji huduma ya haraka.


  Hiki ni kipindi cha soko huria, mi nafikiri ukiona huridhiki na mshahara wa selikarini ni vizuri ukatafuta kazi private sector, kuliko kuomba kazi kisha hutaki kufanya kazi eti unagoma kudai mshahara zaidi
  Madaktari msitumie umuhimu wa taaluma yenu kuwaadhibu watu wasio na hatia, hebu kuwani na moyo wa huruma. Kwani hayo mzingira bora ya kazi mnayodai si huko nyuma yalikuwa hivyo hivyo, mbona walimu wanapelekwa vijijini wanajitahidi na wale wanaoshindwa wanaacha kazi.


  Najua kuna watu wao kazi yao kushabikia tuu tena ushabiki usio na maana!! Hebu katika hili tusiwe kama watoto wadogo, lamsingi warudi hospitalini kufanya kazi zao, hoja kuwa udaktari ni kazi sana kuusomea haina tija, tena ni sababu dhaifu sana kwenu, watu wengine mbona waliona bora wasomee fani nyingine ili kuondoa kadhia kama hizi kwa wagonjwa sasa nyie mliopewa nafasi msitutese bila sababu ya msingi>
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Comrade Gango2, hii mada yako mbona ni kama kachumbali?!, umechanganya issues mno: hivi Amana na Mwanyamala nao wako kwenye Mgomo?!, hivi kweli umepata nafasi ya kupitia madai ya madaktari vizuri?!, mbona madai ya nyongeza ya mshahara ni moja kati ya madai mengi ya kuboresha mazingira ya kazi hasa uwepo wa vifaa bora?!, pitia vizuri orodha ya madai yao kabla hujawa one sided kwenye maamuzi.
   
 3. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,224
  Likes Received: 446
  Trophy Points: 180
  tafadhari, inawezekana hujafika hapo bali nenda kaone wewe pale, ndio hawa watu wanamadai lakini kwanini wagome ile hali kazi zao zinahusiana na kuokoa maisha ya mwanadamu?. wanamkomoa nani? serikali au mwananchi? nani hajui maisha mabovu anayoishi mwalimu wa leo? mbona wao hawagomi? KUMBUKA UHAI HAUJI MARA MBILI KAKA!!

  Hamna kitu muhimu na chenye dhamani kama uhai wa mwanadamu, sasa kwanini wewe usababishe upotee??? je niwangapi wanaomtegemea nyuma??
   
 4. m

  mazombe Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka mimi ni daktarri nimefanya kazi vijijini many years na degree yangu, nimetibu kina mama usiku na mchana bila kuchoka nugu yangu, nimepikia wagonjwa wanaotoka maili nyingi chakula na kuwapa nauli, nimechangia wagonjwa damu many times...

  Mimi ni mzalendo tena sana, mazingira magumu sasa basi yametosha,,, hivi unajua watu wanakufa vijijini kwa kuwa hakuna mipira ya kulishia puani ambao moja haufikii sh 5000?

  Tuna serikali kweli sisi?tunaendesha upuuzi wa sabasaba na nane na week ya utumishi wa umma....ila watu wanakufa kwa hili dogo....UZALENDO!!!!

  Kama wewe mzalendo sana kasomee udaktari hujachelewa Am sure then utajua kwa nini tunagoma, na tutaendelea kugoma ndugu yangu....migari ya serikali kila siku mipya,,,,,,dawa hawaleti vifaa hawaleti.....wazalendo sana na wao wakosomee udaktari, walimu they do not want to dare...WE CAN DARE ...
   
 5. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,224
  Likes Received: 446
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu huo ndio uhalisia wa mazingira yetu, tena sio tu Tanzania bali almost Africa nzima, na sio kwamba leo au kesho yatatatuliwa, HIVI KAMA MAZINGIRA HAYO YAMEKUSHINDA KWANINI USITAFUTE PRIVATE hospital uende huko, sio kwamba watu wameshindwa kusomea udaktari ili nadhani walifikiri mwanzo kuondoa kadhia hizo za kugoma bora waende sekta nyingine na natumai kama wewe usingesomea udaktari ungetoa chansi kwa mtu mwengine asomee.
   
 6. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiki ni kipindi cha soko huria, mi nafikiri ukiona huridhiki na mshahara wa selikarini ni vizuri ukatafuta kazi private sector, kuliko kuomba kazi kisha hutaki kufanya kazi eti unagoma kudai mshahara zaidi
  Madaktari msitumie umuhimu wa taaluma yenu kuwaadhibu watu wasio na hatia, hebu kuwani na moyo wa huruma. Kwani hayo mzingira bora ya kazi mnayodai si huko nyuma yalikuwa hivyo hivyo, mbona walimu wanapelekwa vijijini wanajitahidi na wale wanaoshindwa wanaacha kazi.
   
 7. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  madactari wapo kisiasa zaidi wala si kimaslahi(waliogoma)na mtashindwa!
   
 8. N

  NASUBIRI Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  salaam ndugu wapendwa!
  ni kweli inauma na kusikitisha unapofika na mgonjwa kisha madaktari wanakuangalia
  kama vile umekwenda kuuza sura. mgonjwa analia huna lakufanya. huruma imewatoka, mafunzo wameyasahau ubinadamu hawana tena. wamesahau muda wote wapo masomoni ni fedha za watanzania hawahawa wagonjwa wakiwemo wakilipa kodi ziwasomeshe wao na leo wanaendelea kulipa kodi walipwe mishahara na dawa zinunuliwe.
  watoto hawa ambao leo ni watuwazima wengi wao wametoka vijijini. wamesahau maisha waloishi mwanzo wamejitenga na jamii na kujiona wao ni daraja la juu kuliko wafanyakazi wote nchini. wanatuangalia tukifa wazazi wao, walimu wao tulowafundisha leo hii wakawa madaktari, marafiki zao tuliosoma nao toka msingi,sekondari na vyuo, tukawasupport
  kwa hali na mali. wapi bwana hawasikii la kuu wala la mjukuu. wao na maslahi wao na maisha ya juu.

  hapana tuwakumbushe hawa madaktari wakumbuke haya.
  watuhudumie, tunateseka ndugu zao,watanzania wenzao sisi,
  sie sio wakimbizi kwanini wanatutesa tumekosa nini? kwanini wasiache kazi kama mshahara mdogo?
   
 9. grndossy

  grndossy JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wewe sio daktari, usingezungumza hivyo bila kuwaonea huruma wagonjwa maana hivyo unavyoongea ni kinyume hata ya kiapo cha udaktari. Usitangulize vifaa mbele sema kwa uhakika mishahara ndio kipaumbele chenu msihadae watanzania na vifaa ili tuwaunge mkono. Ungechukua kwa hesabu wagonjwa wanaokufa mkiwa kazini na sasa mkiwa katika mgomo utapata picha gani??? Hivi kwa usomi wako sasa hivi mnamwadhibu nani, Serikali au mgonjwa?????????? Acheni kilio cha mamba bwana!!!!!!!!!!!!!!! kuweni wakweli na muwe na huruma na wananchi wanyonge wa nchi hii. Hii laana ya vifo vya watu wasio na hatia haitawaacha salama nyie na familia zenu. Narudia msitumie uongo na mgongo wa vifaa kudai mishahara mikubwa kwa gharama ya damu za watanzania zinazomwagika bila kuwa na hatia. Eleweni kodi za hawa mnaowaache wafe sasa ndio zimewasomesha hadi kuwa madaktari, wengine kama sio hizo kodi leo mngekuwa waganga wa kienyeji. Muwe na huruma.
   
 10. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,827
  Likes Received: 4,191
  Trophy Points: 280
  Acha wagome na bado walimu (km wanaweza lkn), serikali gani isiyojua vipaumbele vya maendeleo, vipaumbele vya serikali hii ni safari zisizo na tija za jk na msururu wa watu, kusheherekea miaka 50 kwa mabilion, kuongeza mikoa na wilaya ili kuwapa maswahiba ulaji. Serikali yetu imekuwa tajiri kwa kauli na sera zisizotekelezeka, mara kilimo kwanza, mkukuta, vision 2025, what a nonsense!
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,303
  Likes Received: 22,104
  Trophy Points: 280
  :bolt:
   
 12. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  We hujui unachoongea, Huko nyuma kwani watu walikuwa hawafi!!, umeuliza kwanini walikuwa wanakufa na madaktari wapo!!.
   
 13. s

  sugi JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  tell them"LIWALO NA LIWE"
   
 14. kussy

  kussy JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 15, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  A doctor can go on holiday not on strike!


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kuna nguvu kubwa sana naona inaanza kutumika hasa kuanzia jana mchana ya kutaka kugeuza hili swala la madaktari ili lionekane ni mishahara tu. Kwa makusudi kuna watu hawataki kuongelea hoja 'kamili' kama madaktari walivyokubaliana na waziri mkuu.

  Kwa nini watu hawaongelei wagonjwa kulala chini? kwanini watu hawataki kuongea kuhusu ukosefu wa dawa muhimu, hivi kama hakuna x-machine daktari atamtibu mgonjwa kwa kupiga ramli? Kama doctor hana dawa atamtibu mgonjwa kwa kuimba? Au wagonjwa watapona kwa kuona watu walivaa makoti meupe tu? Kwa nini hatutaki kuongea issue nzima?
   
 16. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
   
 17. M

  Mboerap Senior Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  madaktari naona swala la vifaa hio ni zuga tu. Kama kweli mngekua ni vifaa ndo vyawagusa sana basi mlipoongezewa posho za ON CALL na EXTRER SHIFT Pamoja na hio ya "posmotum" si mngeikataa kwanza na kuishauri serekali iwanunulie vifaa kwanza? Jamani mimi siijui sekta iliokamilika vifaa hapa nchini. kwa nn hawa jamaa wanatugeuza wagonjwa ndio ngao ya kukinga mishale kwenye vita yao na serekali? Mm siungi mkono hata kidogo kwani tatizo la upungufu wa vifaa lipo sehem zote; ukienda Polisi utaambiwa kanunue karatasi au jaza mafuta tumfuate mhalifu wako. Shule ndo usiseme, tunanua vitabu, daftari, kalam hata chaki twachangishwa kununua. Madaktari semeni tu mmetuchoka. Kwani kila kukicha mnabadilika. Mlianzia na mgogoro wa ma dk wanafunzi, ikabadilika mkauvaa mgomo nyie. Mkamtosa Pinda kwenye usuluhishi, mkakomaa waziri atimuliwe na wasaidizi wake (wakatimuliwa) mkaenda ikulu mkarudi. Hatujakaa sawa mmegoma tena. Yaani sijui hata agenda yenu ni ipi. Kama leo sh 1,500,000/= haiwatoshi basi hata kama mtapewa hizo ml 3.5 kamwe hazitokidhi tamaa zenu. Wacha sisi tufe ili nyie mtimiziwe mradi wenu. Inaniuma sana
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  jana kwenye taarifa ya habari ITV wameonyesha ajali ya pikipiki ilibeba mshkaki, mmoja wa majeruhi amepondeka vibaya mguu na anatoka damu kichwani, alipelekwa hospitali ya Bombo, madaktari hawajamtibu maana hakuna mashine ya XRAYS.

  Na mkuu wa kitengocha xray amesema wazi kuwa hospitali haina mashine ya xray.... Na inapotokea matatizo kama hayo hushauri kuoeleka wagonjwa kupiga xray kwenye hospitali zenye huduma hiyo...

  Sasa unategemea hali ya majeruhi huyu iweje? Kama xray hawana vipimo vingine itakuwaje??? Ataishia kupata huduma ya kwanza then what next?

  Ingawa mgomo huu unaumizq na kusikitisha, ila kuna joja za msingi nyuma yake....
   
 19. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  wewe kama muhanga wa mgomo umefanya/umeisisitiza vipi serikali iboreshe huduma za afya na iwajali madaktari? DAKTARI ANAKUTUMIKIA NAWEWE MSAIDIE SI KULALAMIKA TU
   
 20. D

  Danniair JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acheni wagome. Mandela asingeikubali jela A.Kusini isingejipatia uhuru. Sisi wenyewe tukienda mahospitalini
  huwa tunaziba pua. Lakini madkt ndimo wanamoshindia. Sisi tuko kwenye viyoyozi wa wamo matanuruni.
  Tunataka huduma za afya ziboreshwe. Kama serikali haitafanya kwa hiyari basi njia mbadala zitatumika.
  Lakini hekima ya kujishusha kwa serikali ndiko kunakotakiwa.

  Mwenyeji ndiye akuambie matatizo yake na si wewe kujiamulia juu ya matatizo yake. Kama kweli tunataka
  kusonga mbele kimaendeleo.

  Angalia pesa zilizotengwa kwa ajili ya madkt toka nje. Je hazitoshi kununulia mtambo wa kusindika unga
  wa mahindi na kuuuza huko sudani na kwingineko kwenye njaa Afrika?
   
Loading...