Kama nilivyobashiri kuwa CCM na Tendwa watakuja na majibu ya kupuuza madai ya Ccj ndivyo inavyotokea sasa bado tutasikia mengi toka kwa Tendwa,Pasco na MMKJ nafurahi kuona mnavyojitahidi kuwafanya watu waone Ccj ni mkombozi, ni kama vile namona Pasco alivyokaa akisubiria hilo tamko. Jamani tumeona na kusikia matamko mangapi we need physical action now na si blaa blaa, leo Ccj wakimaliza tamko lao kesho Tendwa anatoa tamko lake keshokutwa Ccj watakuja na tamko kali maradufu baadaye Tendwa atawapuuza na sinema itakuwa imefika tamati. Mwisho Ccj kwa kujitetea watasema mnaona wasingenishika shati ningemgaragaza, ngumi za utotoni hizo.
Kama nilivyobashiri kuwa CCM na Tendwa watakuja na majibu ya kupuuza madai ya Ccj ndivyo inavyotokea sasa bado tutasikia mengi toka kwa Tendwa,
SIKU moja baada ya Chama Cha Jamii (CCJ) kutoa shutuma kali za kuhujumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kisipate usajili wa kudumu, madai hayo yamepuuzwa na uongozi wa juu wa chama tawala.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara na Spika wa zamani, Pius Msekwa, aliwataka Watanzania kupuuza madai hayo aliyoyaita ya kizushi.
Ndiyo binti yangu, kwani wewe unayaamini hayo? Msekwa alimuuliza mwandishi wa habari hizi aliyeomba kupata kauli ya CCM kuhusu madai ya kufanya hujuma pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ili kukinyima usajili wa kudumu CCJ.
Hakuishia hapo Msekwa aliendelea kusema, Jawabu lako ni kupuuzia maneno usiyoyaamini usiyape uzito maneno ya kipuuzi na kizushi ambayo hata wewe huyaamini, eee basi tuishie hapo endelea kuyapuuzia, alisema Msekwa.
Katika madai yake, CCJ ilinukuu kauli mbalimbali za kejeli, zenye kuonyesha kuwa ni ndoto kwa chama hicho kipya kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao zilizotolewa na viongozi wa chama tawala na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kwa nyakati tofauti.
Sisi wenye akili tuna jua yeye Msekwa ndiye mpuuzi na anafaa kuuuzwa!
Upo mzee wa texas?
Nipo kiongozi najiandaa August kwenda kwenye Kampeni!
Tutakutana huko mzee!
Na wewe unakwenda kwenye hichi chama kipya nini?
Huyu mzee anazeeka vibaya! Walichofanya CCJ ni kunukuu aliyoyasema huko nyuma. Kwa nini anataka Watanzania wayapuuzie aliyoyasema mwenyewe?
Kama nilivyobashiri kuwa CCM na Tendwa watakuja na majibu ya kupuuza madai ya Ccj ndivyo inavyotokea sasa bado tutasikia mengi toka kwa Tendwa,
SIKU moja baada ya Chama Cha Jamii (CCJ) kutoa shutuma kali za kuhujumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kisipate usajili wa kudumu, madai hayo yamepuuzwa na uongozi wa juu wa chama tawala.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara na Spika wa zamani, Pius Msekwa, aliwataka Watanzania kupuuza madai hayo aliyoyaita ya kizushi.
"Ndiyo binti yangu, kwani wewe unayaamini hayo?" Msekwa alimuuliza mwandishi wa habari hizi aliyeomba kupata kauli ya CCM kuhusu madai ya kufanya hujuma pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ili kukinyima usajili wa kudumu CCJ.
Hakuishia hapo Msekwa aliendelea kusema, "Jawabu lako ni kupuuzia maneno usiyoyaamini… usiyape uzito maneno ya kipuuzi na kizushi ambayo hata wewe huyaamini, eee basi tuishie hapo endelea kuyapuuzia," alisema Msekwa.
Katika madai yake, CCJ ilinukuu kauli mbalimbali za kejeli, zenye kuonyesha kuwa ni ndoto kwa chama hicho kipya kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao zilizotolewa na viongozi wa chama tawala na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kwa nyakati tofauti.
Mlinitaka aseme 'ndiyo tumekula njama'-are you serious? Karibu kwenye siasa za upinzani MM mtayakuta mengi. Hapo bado hamjashinda uchaguzi lakini mkurugenzi wa uchaguzi anamtangaza ambaye hakushinda, na akishatamka yeye ndiyo imetoka hiyo, welcome to TZ politics!!