Madai: Steve Nyerere wa Bongo Movie alia, kisa kukosa U-DC

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
nyerere.jpg

Madai! Kufuatia Rais Dk. John Pombe Magufuli kuteua wakuu wa mikoa (ma-RC) na wale wa wilaya (ma-DC) kuna madai kuwa msanii wa lamu za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amekuwa akilia baada ya kuukosa ukuu wa wilaya.

Chanzo chetu cha kuaminika ambacho kimekuwa kikizunguka maeneo mbalimbali na msanii huyo, kimedai kuwa kila wanapokuwa kwenye vikao vyao, Steve amekuwa akisononeka sana kwa kunyimwa uongozi kwenye serikali ya awamu ya tano.

“Malalamiko makubwa ya Steve ni kwamba amekuwa akishirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa hali na mali na hata kwenye kampeni alishiriki vyema na wasanii wenzake kumuunga mkono Rais Magufuli lakini ameambulia patupu, hata u-DC ameukosa,”kilisema chanzo hicho.

Kufuatia malalamiko hayo, mwandishi wetu alimtafuta Steve na kumuuliza kama madai hayo ni ya kweli ambapo alikanusha kusononeshwa na kunyimwa uongozi lakini akasema kwamba umri wake bado mdogo na maisha yanasonga.

“Watu wanapaswa wajue kuwa kila zama na wakati wake, nawaamini walioteuliwa na rais, na nawaomba wasimuangushe kwa heshima kubwa aliyowapa.

“Umri wangu bado unaruhusu kama Mungu atanijalia uchaguzi ujao nitaingia tena mchakatoni, ila kama wasanii wangepewa nafasi japo mbili kwenye uteuzi huo ingekuwa safi sana,” alisema Steve.

Steve, Wema Sepetu na wasanii wengine waliungana na kuanzisha Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao ambayo rais mstaafu, Jakaya Kikwete aliizindua rasmi na ilihusika katika kuzunguka maeneo mbalimbali ya nchi kuhamasisha watu waichague CCM katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, huku Makamu wa Rais, Samia Suluhu akiongoza kampeni hiyo.
 
Back
Top Bottom