Madafu sasa ni 1,600 kwa USD1, Mwaka jana ilikuwa ni 1400 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madafu sasa ni 1,600 kwa USD1, Mwaka jana ilikuwa ni 1400

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ntemi Kazwile, Jun 10, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wakati watanzania wakisherekea bajeti "inayowajari" na ambayo itapunguza ukali wa maisha shilingi ya Tanzania imeendelea kuporomoka, sasa inakimbilia $1 = Tzs1,600 ikilinganishwa na 1,400 ya mwaka jana.

  Kushuka thamani kwa pesa siyo lazima kuwa ni kitu kibaya lakini kwa nchi kama Tanzania ambayo inategemea zaidi kuagiza vitu kutoka nje ni hatari kwa mstakabali ya uchumi... Tanzania inaagiza vitu vifuatavyo:
  • Mafuta ya kula - zaidi ya asilimia 80% yanatoka nje
  • Mafuta ya kuendeshea mitambo na magari - 100%
  • Gesi ya kupikia majumbani - 100%, yes 100%
  • Magari na vyombo vingine vya usafiri- 100%
  • Pembejeo za kilimo, viwanda - zaidi ya 95%
  • Ngano - zaidi ya 90%
  • Nguo - zaidi ya 90%
  Ajabu ni kwamba kwenye bajeti ya serikali hakuna jitihada zozote zinazowekwa na serikali ya CCM kuhakikisha kuwa angalau tunaanza kupikia gesi inayopatikana nchini ingawa kila mtu anakubali kuwa kuendelea kupikia kuni au nishati itokanayo na mimea ni janga la kitaifa -- upungufu wa mvua unaongeza umasikini uliokithiri, upungufu wa mvua unaongeza uwezekano wa migogoro, n.k

  Serikali pia haijaweka jitihada zozote za makusudi kuhakikisha kuwa Tanzania inajitoshereza kwa mafuta ya kula licha ya ukweli kwamba tunauwezo wa kuwa wazalishaji wakubwa wa mafuta ya kula yatokanayo na alizeti na mazao mengine...

  Hadi tunafika Desemba itakuwa ajabu kama inflation haitakuwa imefikia asilimia 50% (ukilinganisha na Desemba 2010!)
   
 2. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  this is serious!!!!
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  na bado mpaka mtakapo acha kucheka na magamba..
   
 4. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Watu walitabiri gharama za maisha itakavyopanda endapo ****** atakapopata uongozi wa kipindi cha pili nchi hii,na ndivyo ilivo sasa na atakapoondoka ndo kabisa ni zaidi ya hapa tulipo, lets wait and see!
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Na bado mlipoichagua CCM tulisema itafika Shs itakuwa sawa thamani ya shilingi ya Zimbabwe na hapo ndio mtatia akilini itakapokuwa sukari haipatikani, mkate haupo, vitunguu havinunuliki . Gavana anakuaambieni tu kuwa Shillingi ikiporomoka ni vizuri na Waziri wa fedha anasema wazi wazi shillingi imeporomoka kwasababu ya kuzidi kwa matumizi ya dollar nchini. Sijui hawa watu hawajiulizi swali la je kuna faida gani basi ya kuwa na shillingi nchini????
   
 6. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,135
  Likes Received: 3,327
  Trophy Points: 280
  JK ajivue gamba,nchi imemshinda.
   
 7. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu,

  Ni wachache sana waliichagua CCM, walijiingiza madarakani kutumia hila na mtutu wa bunduki (mfano Shinyanga Mjini, Karagwe, Muleba, Segerea, n.k., n.k.)
  Itabidi tujipange tusiruhusu ujinga huu ujirudie mwaka 2014 (serikali za mitaa) na 2015 (uchaguzi mkuu)
   
 8. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Ndo maisha yetu bongo,pangu pakavu.
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  KIKWETE oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
Loading...