MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Mwalimu upo vizuri sana mimi mwanangu mazingira tuliyopo sio ya kuichanganya ili kuweza kufikia mawazo yako Nazani daycare itambadilisha
 
Hilo ni tatizo ikiwa hasikiii! ila kama anasikia inawezekana hapo mlipo mtoto mnamsemesha luga zaidi ya moja nayo ni sababu ya mtoto kuchelewa kuongea.
Yupo mtoto wa rafikiangu yupo AUSTRALIA ana umri wa miaka 3 haongei, baada ya kumpeleka hospitality majibu yakaja kuwa mtoto wazazi wanamuongelesha luga tatu kiswahili kizigua na kiingereza ndio iliomchanganya ashidwe kuongea mapema
 
Mtoto wako hana tatizo akbisa.

Tatizo ni mazingira kwa sababu mtoto ili aongee haraka ni lazima akae muda mrefu na watu wa lugha husika.

Mwanao kama anacheza na watoto wenzake mnooo basi itakuwa ngumu kongea haraka kwa sababu hao watoto nao hawapatii maneno.

Mtoto kama anakaa nyumba ambayo hakuna pirika za maisha ni ngumu kuomgea kwa sababu mtoto hujifunza na matukio.

Ndio maana watoto wa kizaramu huwa wanaongea sana kwa sababu wanaishi kwenye mchanganyiko wa watu hivyo ni rahisi kwao kujifunza mapema lugha.

Mtoto acheze na watu wajuzi wa lugha,kqma mtoto anakaa na wstu wakimya basi atachelewa kuomgea.

Kuna msemo huwa katika falsafa yangu ya kumkuza mtoto kiligha inasema " mtoto ataweza kuongea lugha ambayo anaisikia tu,na atakiongea kile anachokisikia tu"

Usitegemee mtoto aseme naomba maji wakati hajawahi kusikia hiyo kauli katika mazingira anayoishi ikitamkwa mara kwa mara.

Mtoto usitegemee anasema "baba unnarudi wapi" wakati hajawahi kumsikia mama yake akikuuliza wewe baba.

Mtoto hawezi kusema "hili ni shati" wakati hawawahi kusikia neno hilo likitamkwa mara kwa mara.

Jitahidi ili awe anaongea lazima akae na watu waongeaji.

Lakini akikaa na watu wa matusi mtoto naye matusi hayatamuisha.

Huo umri wa mwanao hapo ndo hujifunza yote mazuri na mabaya na mbaaya zaidi hajui baya wala zuri,na baya zaidi ukimuambia hili baya haelewi yeye naajua kuiga tu.

Solution sasa awe anakaa sehemu salama ya tabia na asikilize sana watu wakiongea sio mtoto wafungie ndani na mama ake tu yeye anachosikia "acha hiyooo"

Takuchapaaaa

Toka hapaaaa.

Kulaaaa
 
Mwalimu upo vizuri sana mimi mwanangu mazingira tuliyopo sio ya kuichanganya ili kuweza kufikia mawazo yako Nazani daycare itambadilisha
Mkuu i wish nisaidie bure maana nina knowledge kubwa sana ya kusaidia watoto, wazungu wametunoa sana tunamaarifa hayo......japo hizi shule hata kama bei ila inategemea na personality ya mwalimu, mwalimu ndio atakuwa msaada wa mtoto kipindi chote cha makuzi.....

mkeo akiwa anafanya shughuli ndogondogo mtoto akiwa karibu awe anajiongelesha like hapa naosha vyombo, hii ni rangi ya blue, hapa napika, huu ni mchele, mimi ni mama etc.......

Kwa nyimbo za english zinazosaidia mtoto kuongea na kuchangamka Ni Johny johny, The wheels on the bus, Twinkle twinkle little star, shake shake the mango tree, BINGO dog, Elephant elephant etc Hizo nyimbo huwa zinainvolve vitendo kuimarisha muscles za mwili na concentration pia zinakuwa fun ukijua kuziimba kwa kuchange tones.....

Hizo nyimbo zote zinapatikana Youtube mkuu

Mungu akusaidie mkuu.
 
Anajikojolea tu hasemi chochote, maji anaenda kuchukua kikombe anakuletea, ukimwambia njoo anakuja
Pole

kabla ya mtoto kulala mkojoleshe na ile alfajiri mwamshe akojoe na ikibidi ule usiku wama8 Fanya hilo zoezi...mkanye akijinyea pia MPE na poti LA kujisaidia ikibidi

Fanya zoezi hilo Mara kwa Mara LA kumkumbusha

Wife anafanya hivyo kwa dogo wa umri kama huo;hajikojolei wala kujinyea na anatumia choo cha familia,anasaidiwa kutawazwa tu na asiposafishwa analia

na akitaka maji ya kunywa anaomba tena kwa sauti na hadi apewe.Leo ameanguka akajigonga jioni aliponiona akasema 'baba nataka dawa' kumchek nikaona ana ngeu ya kuanguka...akapewa paracetamol na kupakwa cream.
 
Jaribu kumuwekea katuni za kiswahili zile zinazoongea wanaita animation zenye hesabu kuimba n.k zinapatikana you tube zitamsaidia na kumchangamsha zaidi
 
Ndugu duh mtoto miezi minne aongee dah ! Bado huyo
mtoto anafikisha hata miaka 2 na anachoongea anakijua mwenyewe huwezi muelewa sembuse hiyo miezi minne hata kusimama dede bado achilia mbali kutembea
 
Ndugu duh mtoto miezi minne aongee dah ! Bado huyo
mtoto anafikisha hata miaka 2 na anachoongea anakijua mwenyewe huwezi muelewa sembuse hiyo miezi minne hata kusimama dede bado achilia mbali kutembea
Mkuu soma uzi vizuri ndo ujibu uzi, maana hapa umetia aibu. Huyo mtoto ana miaka minne na sio miezi minne.

Asante
 
Mkuu soma uzi vizuri ndo ujibu uzi, maana hapa umetia aibu. Huyo mtoto ana miaka minne na sio miezi minne.

Asante
Mkuu umesoma vizuri kweli???
Aisee nimechanganya desa Nimesoma vibaya aisee nikajua ni miezi minne ndio maana nikashangaa kumbe ni miaka 4
Dah ! Hapo kweli lazima uwe na shaka na ukose amani kama mzazi
pole sana mkuu wangu Prince mrema
Sikusoma vizuri post yako
 
Mpeleke CCBRT kuna speech therapist niliwahi sikia.

Au specialist wa watoto yoyotw km bado hujampeleka

Ila kubwa zaidi, kama hajaanza shule mpeleke day care haraka. Huko atajua kuongea haraka sana. Hii nimeishuhudia kwa mtoto wa ndugu yangu kbs. Alifika umri km huo hajui kuongea. Wakaenda CCBRT wkaambiwa mtoto hana shida. Wakampeleka shule tu day care. Hapa mwaka haujaisha tayari mtoto anaongea vizuri sana na kuunda sentensi.
 
mchanganye na watoto, inawezekana hua hamumzungumzishi alipokua mdogo namaanisha kuongea naye ile kitoto toto niliambiwa hua inasaidia kwa hapo mlipofikia jaribuni kumpeleka hospital pia mkiambiwa hana tatizo mpelekeni shule
 
niliwahi kuambiwa vitu viwili

kwanza kabisa mtoto anapokua mdogo akianza kujiongelesha mzaz unatakiwa umjibu umfatishe vile vile usimuache akaongea peke yake

kingine mama yake aangekua anamlambisha mwiko, kama anapika mboga vile vinavyobakia kwenye mwiko anamlambisha wanasema wahenga inasaidia kufunguka kwa maneno au akivunja naz wakat anataka apike ampe maji yake anywe asimwekee kwenye kikombe anywe na naz yake

lakini pia mwekeni kwenye watoto wenzie acheze nao inasaidia
 
Mpeleke kwa wataalam wakukata kilimi fasta wakamchunguze...wang alikua hivyo wakanishauri kwenda kule mtalam akasema anakilimi chin yaulim kilikua kinampa uzito angechelewa angekua bubu nashukur baada yakumkata akaanza kuongea
 

Hii ilinitokea kwa mwanangu wa kwanza alichelewa mno kuongea na kutembea pia

Yaani she was lazy isipokuwa kwenye kula

Nilipomletea mdogo wake mambo yakabadilika

Mdogo kaanza kuongea na miezi 10 na kutembea hapo dada anajikongoja
Akawa anakula kipigo toka kwa mdogo wake

Hadi sasa amekuwa very strong,yaani angekuwa mwenyewe sijui Kama hata angejiangaisha na chochote
 
Kusikia anasikia maana ukiwasha Katuni toka chumba cha pili hata kwa sauti ndogo lazima akulupuke kuja kuchungulia, kuhusu lugha tunaongea lugha moja ya Kiswahili ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…