Mada Maalumu ya Afya ya Akili

mchemsho

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
3,212
867
Wakuu,

Tukubali tukatae kwa sasa kumekuwa na matukio mengi ambayo sio ya kawaida Kama vile Kuuwana, kufanya vituko vya kujiaibisha na mhusika akaona ni sawa nk nk.

Ukisoma machapisho kadha wa kadha mambo haya yakekuwa yakihusishwa na janga la Afya ya Akili. (mental health).

Kwa bahati mbaya hili halijawahi kuwa kipaumbele cha Serikali wala Wizara ya Afya.

Je, serikali imefanya vya kutosha kuhusu kadhia hii?

Nini ni dalili za ugonjwa wa Afya ya Akili?

Ipi ni tiba ya Afya ya Akili?
Je, ukitambua mtu ana tatizo la Afya ya Akili hatua gani za kuchukua bila kumkwaza?

Mental health issue is real.
Social media if mishandled is a a disaster.

Uzi tayari.
 
Watu wataangamia sana maana tunaona afya ya akili kama hakituhusu
Serikali ifanye mjadala wa kitaifa maana mauaji ni kama yamezidi
 
Soma vitabu vya psychology, Mimi nilikuwa na hili tatizo la wivu kupitiliza hii ilitokana na mwanamke wangu wa kwanza kuchepuka na kumkuta tukapigana chini sikuweza kusamehe na sitokaa nije niweze

Ishu ikaanzia kwa Huyu mpya imani ni sifuli ila nimepambana na iyo ishu naendelea kuishinda mbinu ya kwanza

1. Jipende
2. Kubali kuwa ni mapito
3.kula tizi sana hasa gym ukirudi usingizi
4.kula vzr
5. Tafuta hela au mafanikio kwa nguvu zote.
6.jua mwanamke hujazaliwa naye ko anaweza ondoka mda wowote.
7. Sali sana kwa imani yako mungu akupe mke bora
8. Usichukulie serious sana mahusiano ata kama ni mke wako
9. Usiwe na mwanamke mmoja ( japo ni hatari kuwa makini ikiwezekana kacheki afya na wanawake zako wote)
10. Likikukuta muachie mungu kwa sababu yeye anajua mwanzo na mwisho


Baada ya kufanya aya yote now niko fit nilikonda ila saizi ukiniona bonge la mtu

N.B mapenzi ni upuuzi jipende mwenyewe.
 
Soma vitabu vya psychology, Mimi nilikuwa na hili tatizo la wivu kupitiliza hii ilitokana na mwanamke wangu wa kwanza kuchepuka na kumkuta tukapigana chini sikuweza kusamehe na sitokaa nije niweze

Ishu ikaanzia kwa Huyu mpya imani ni sifuli ila nimepambana na iyo ishu naendelea kuishinda mbinu ya kwanza

1. Jipende
2. Kubali kuwa ni mapito
3.kula tizi sana hasa gym ukirudi usingizi
4.kula vzr
5. Tafuta hela au mafanikio kwa nguvu zote.
6.jua mwanamke hujazaliwa naye ko anaweza ondoka mda wowote.
7. Sali sana kwa imani yako mungu akupe mke bora
8. Usichukulie serious sana mahusiano ata kama ni mke wako
9. Usiwe na mwanamke mmoja ( japo ni hatari kuwa makini ikiwezekana kacheki afya na wanawake zako wote)
10. Likikukuta muachie mungu kwa sababu yeye anajua mwanzo na mwisho


Baada ya kufanya aya yote now niko fit nilikonda ila saizi ukiniona bonge la mtu

N.B mapenzi ni upuuzi jipende mwenyewe.
Acha uongo eti umesoma vitabu vya psychology

Kwa analysis ndogo tu,, bado uko kwa stage ya kwanza ya "The ego comes alive"
 
Soma vitabu vya psychology, Mimi nilikuwa na hili tatizo la wivu kupitiliza hii ilitokana na mwanamke wangu wa kwanza kuchepuka na kumkuta tukapigana chini sikuweza kusamehe na sitokaa nije niweze

Ishu ikaanzia kwa Huyu mpya imani ni sifuli ila nimepambana na iyo ishu naendelea kuishinda mbinu ya kwanza

1. Jipende
2. Kubali kuwa ni mapito
3.kula tizi sana hasa gym ukirudi usingizi
4.kula vzr
5. Tafuta hela au mafanikio kwa nguvu zote.
6.jua mwanamke hujazaliwa naye ko anaweza ondoka mda wowote.
7. Sali sana kwa imani yako mungu akupe mke bora
8. Usichukulie serious sana mahusiano ata kama ni mke wako
9. Usiwe na mwanamke mmoja ( japo ni hatari kuwa makini ikiwezekana kacheki afya na wanawake zako wote)
10. Likikukuta muachie mungu kwa sababu yeye anajua mwanzo na mwisho


Baada ya kufanya aya yote now niko fit nilikonda ila saizi ukiniona bonge la mtu

N.B mapenzi ni upuuzi jipende mwenyewe.
nyinyi bhana... Sasa hayo si km mateso tuu... Unaishije na mtu ambaye humuamini?.. then kuwa na wengi sio ujanja.
 
Kamalizia vema sana hapo mwishoni, mapenzi ni upuuzi…. muhimu jipende mwenyewe.
Yes hapo ni kweli kwenye kujipenda. Jipende haswaa... Uwe kipaumbele chako ww mwenyewe. Lakini mapenzi sio upuuzi, mapenzi ni matamu mkuu, haswa mkipendana. Sitakuja kuchukia mapenzi kabisa...
 
Magonjwa ya Akili ni Nini na husababishwa na Nini?
• Magonjwa ya akili ni matatizo ya ubongo ambayo humfanya mtu kuwa na hisia, fikira na matendo tofauti na yale yanayotarajiwa na jamii na kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha. Magonjwa ya akili yanaweza kusababishwa na sababu za kibaiologia au kisaikolojia;

Sababu za kibaiologia
• Kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi,Magonjwa ya muda mrefu kama degedege, malaria kali, UKIMWI nk pia Matumizi ya dawa za kulevya

Sababu za kisaikolojia
• Majanga, ubakaji, uvamizi, ajali,utekaji nyara, kukosa elimu,kukosa ajira nk
• Kufiwa, kutengana, talaka, ugoni, kufungwa
• Kufukuzwa kazi, kukosa mishahara, kustaafu kazi nk.
• Kutokufanya vizuri kwenye masomo na Kufukuzwa chuo/ shule
• Matatizo yanayowaathiri watoto kisaikolojia Kunyanyaswa kingono, Kupigwa na kutengwa, Kutothaminiwa.. Kutokupata matunzo stahiki

Magonjwa ya akili yamegawika katika sehemu kuu mbili kulingana na ukubwa wake
1) Magonjwa ya akili ambayo mgonjwa hustahiki kutumia dawa au kulazwa hospital (major psychiatric disorder).
2) Magonjwa ya akili ambayo mgonjwa anaishi kawaida licha ya changamoto ndogo ndogo ila hajafikia kigezo cha kutumia dawa au kufikishwa hospitali.

Uhalisia wa maisha kwa mujibu wa taarifa ya APA, wapo wagonjwa wengi ambao wana magonjwa ya akili ila ni ngumu kwa wao kujitambua kua wana tatizo hilo kwa sababu ambazo inaweza kua ukosefu wa elimu, mila potofu, imani na hata kusikia aibu kuorodhesha Madhaifu yake kwa watu wengine.

Jionee baadhi ya magonjwa ambayo unaweza kujiona na wewe upo hapo!

1). Bipolar mania : Huu ni ugonjwa ambao mgonjwa anaonekana kufanya mambo bila kufikiria, anakasirika kirahisi kuliko kawaida, kuwa na furaha isiyo ya kawaida, kuwa na nguvu nyingi na kufanya shughuli nyingi kupita kiasi na hata kua na matamanio makubwa ya kimwili (hutokea kwa wanawake na wanaume kuanzia miaka 18 na zaidi.

2). Narcistic disorder :
Ugonjwa huu hutokea kwa wanawake zaidi. Mara nyingi mgonjwa huwa anaonesha dalili za kutaka kua mbele katika kila jambo. Mara nyingi yeye ndio anakua muongeaji mkuu na sifa nyingi akiwa darasani au sehemu fulani.

3). Obsessive compulsive disorder: Ugonjwa huu Mara nyingi hutokea kwa wazee lakini hata vijana huwapata. Mgonjwa anaweza kua na mawazo yenye kujirejea mara kwa Mara na kuchukua hatua juu ya mawazo Yale mfano unaweza kumkuta mtu amelala anaamka na kwenda kuangalia mlango mara kwa mara kwa hofu ya kuogopa hajafunga mlango.

4). Dysmorphic disorder;
Ugonjwa huu mara nyingi ni wanawake ila hutokea pia kwa wanaume. Mgonjwa hupenda zaidi kuhusudu maumbo yao. Anaweza kukaa chooni muda mrefu akijitazama au kukaa kwa kioo muda mrefu. Wanawake hutumia muda mwingi kujiangalia maumbo yao kama nywele, makalio, matiti na hips. Hali hii huwafanya wajione bado hawajapendeza kwa hiyo hutumia muda mwingi either kujipamba au katika kioo. Wanaume wao huhusudu zaidi vifua vyao na uume mkubwa.

5). Fetishisms disorder :
Mgonjwa aliye na tatizo hili huwa anatabia ya kuhusudu maumbile au mavazi ya jinsia nyingine, mfano; mwanaume anaweza kupenda kuangalia maumbile ya kike mfano kiungo na wakati mwingine huwa wanathubutu hata kuweka nguo za kike katika mabegi yao au kuzivaa.

6). Traverse fetishisms : Mgonjwa huvaa kabisa mavazi ya jinsia nyingine. Kwa mfano nguo ya ndani.

7). Exhibition sexual disorders ;
Mgonjwa anakuwa na tabia ya kuvua nguo na kuonesha maumbile yake ya siri kwa jinsia nyingine, mara nyingi i kwa wanaume.

8). Pedophilia :
Kwa jina jingne huitwa mafataki, ni tabia ambayo unaweza kumuona mzee anapenda kutoka na watoto wadogo aliowazidi umri. Hii hutokea zaidi kwa wanaume.

9). Froutering disorder (dubgadunga) :
Ni tabia ambayo mtu hupenda msuguano au kushikashika maumbile ya mtu mwingine akiwa ktk usafiri hususani daladala.

10). Voyeurism: mgonjwa hupenda ku enjoy kwa kuangalia wengine wakifanya tendo la ndoa, Mara nyingi kwa kupiga "chabo" madirishani, milangoni au hata kwenye mitandao (website) mbalimbali.

11). Hyperactive disorder :
Ni ugonjwa ambao mtu husika anakua na tabia ya kuhamaki mara kwa Mara hata kwa jambo dogo, pia anafanya maamuzi ya haraka haraka

12). Social phobias : Huu ni ugonjwa ambao mtu huwa na uoga au hofu ya kuongea au kuzungumza mbele za watu mfano mbele ya darasa, katika mikutano, mikusanyiko ya watu na hata nyumbani.

13). Hoarding disorders :
Unaweza sema karibu watu wengi wako na huu ugonjwa! Mgonjwa huwa na tabia ya kutunza vitu visivyokua na u muhimu tena kwa muda mrefu mfano unaweza kuona amehifadhi madaftari yake ya tokea shule ya msingi , nguo za shule za primary na hata mashilingi yaliopitwa na wakati.

14). Trichotilomania :
hii ni tabia au ulemavu ambao mwanaume hua na tabia ya kuchezea au kuvuta ndevu zake, nywele zake nk.
Tabia hii hujirudia mara kwa mara.

16). Agoraphobia : mtu aliye na tatizo hili hua na tabia ya uoga kupita sehemu ambayo anahisi kama atapita litatokea jambo baya au atakosa msaada mfano porini, katika daraja au kusafiri kwa treni n.k.

17). Antisocial behaviour:
Tabia hii unaweza kumuona mtu anashindwa kushirikiana na wenzake ,anajitenga na kufanya mambo yake ki vyake kwa kuamini kua watu hao n wabaya kwake au hawawezi msaidia.

18). Social pragmatic communication disorder : mgonjwa anashindwa kutumia sheria za mazungumzo mfano kuzungumza kabla mwingine hajamaliza kuzungumza. Yeye anakua na tabia ya kutosubiri mwenzake amalize.

19). Frontal lobe syndrome (disinhibition ): Mgonjwa anakua hawezi kujizuia tabia au maneno yao kulingana na eneo. Kwa mfano, unaweza kumkuta anatukana ovyo , anafanya tabia za ajabu kinyume na mila za eneo au watu husika anaweza hata kuvua nguo bila kujali

20). Hysteria (Mhemko wa kimwili): Sio ugonjwa wa akili ila mara nyingi huwakuta wasichana na wanawake na huambatana na dalili za magonjwa ya akili, mgonjwa hupoteza fahamu, kupandisha mashetani , kuanguka na kukukuta km mgonjwa wa kifafa. Mgonjwa hutambua kila kinachoendelea katika mazingira yake, hu fumba u ili kuwahadaa waliomzunguka ili waamini kuwa amezimia na hivyo kuvuta hisia ya watu/mtu aliye mkwaza.

Matibabu ya Magonjwa ya Akili
Matibabu ya magonjwa ya akili hutoafautiana kati ya ugonjwa mmoja na mwingine..
• Elimu kwa jamii kuhusiana na magonjwa ya akili ni kitu cha muhimu sana katika kuzuia kujirudia au kupata ugonjwa waakili, juu ya matibabu na msaada anaohitaji mgonjwa ili kuendelea na maisha yake ya kila siku.
• Kupatiwa uchunguzi mapema ili apatiwe tiba sahihi na ya mapema
• Tiba ya kisaikolojia (kujitambua aliko, anapotaka kuwa na kuamua kufanya mabadiliko kwa kutegemea uwezo wake mwenyewe
• Tiba kimwili kutumia dawa za hospitali
• Matibabu kwenye nyumba za upataji nafuu (Sober Houses)
• Ushirikiano kati ya mgonjwa familia na wataalamu wa tiba huleta mafanikio makubwa sana katika matibabu.
• Kutokutumia madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na vilevi
• Pata muda mrefu wa kupumzika
• Fanya mazoezi
• Usijitenge na jamii
• Kujibidisha kwenye shughuli za kuleta kipato



Ahsanteni kwa kunifuatilia kwenye bandiko hili


CHANZO/MAREJEO: MTANDAO NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (KITUO CHA AFYA)
 
Back
Top Bottom