Mada maalum ya ndege toka FB

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la KLM, Marjan Rintel, amevalia sare ya wahudumu wa ndege na kushiriki kutoa huduma kwa abiria katika safari ya ndege kutoka Amsterdam, Uholanzi, kwenda Johannesburg, Afrika Kusini.

Katika safari hiyo ya ndege aina ya Boeing 777-300ER, Rintel alishiriki kutoa huduma kwa abiria, na kujaribu huduma mpya ya chakula kwa safari za masafa marefu na kupata maoni ya wasafiri kuhusu huduma wanazopata ndani ya ndege.

Kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa LinkedIn siku ya Oktoba 22, Rintel alisema uzoefu huo unamsaidia kuelewa majukumu na changamoto zinazowakabili wahudumu, ambao hutumia muda mrefu wakiwa kazini huku wakitakiwa kuendelea kuwa makini na kutoa huduma bora.

Alisisitiza kuwa wahudumu wana mchango mkubwa katika kuwafanya abiria wajisikie wamekaribishwa na kuwa huru wanaposafiri na KLM.

Rintel, aliyekuwa Rais na Mkurugenzi Mkuu wa KLM tangu Julai 2022, aliwahi pia kushiriki kazi za wahudumu katika safari ya kwenda Los Angeles, Marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…