Mada maalum ya ndege toka FB

Taarifa za awali zinaeleza kuwa ndege aina ya Let L-410 yenye namba za usajili 9S-GUC imepata ajali mjini Kenge, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), siku ya Ijumaa, Septemba 25, 2026, huku taarifa zikidai kuwa watu 13 wamepoteza maisha.

Kwa mujibu wa taarifa zinazozunguka kuhusu orodha ya abiria na wafanyakazi waliokuwa ndani ya ndege hiyo, jina la Luteni Jenerali Mutombo Katalay Tiende Joseph, ambaye ni Mkuu wa Kwanza wa Mahakama Kuu ya Kijeshi ya DRC, limetajwa miongoni mwa waliokuwemo katika ndege hiyo.

Taarifa rasmi za awali zinazopatikana pia zinamtaja Mutombo Katalay Tiende Joseph kama Mkuu wa Kwanza wa Mahakama Kuu ya Kijeshi.

Aidha, hati ya safari ya kikazi ya tarehe 19 Agosti 2026 inadaiwa kuonyesha kuwa ujumbe huo uliongozwa na Luteni Jenerali Mutombo Katalay Tiende Joseph.

Miongoni mwa maafisa wengine waliotajwa katika ujumbe huo ni Luteni Jenerali Likulia Bakiumi Lucien René, Meja Luntala Kibanzidi Albert na Kapteni Mbuku Pasipamba, pamoja na maafisa wengine.

Hata hivyo, utambulisho wa waathirika wa ajali hiyo bado haujathibitishwa rasmi na mamlaka husika. Hivyo, majina yaliyotajwa katika orodha hizo yanapaswa kuchukuliwa kama taarifa za awali hadi pale mamlaka za DRC zitakapotoa uthibitisho rasmi.
 
According to JC EXPLORER..... ndege za kisasa zina mfumo wa flaps. Ambazo zinavuta ndege nyuma ili kupunguza kasi ya mwendo na upepo... flaps zinapatikan kwenye mabawa. Kama dreamliner za air tanzania au BOEING 777-300ER.
 
Unapoitazama anga kutoka ardhini, linaweza kuonekana kuwa kubwa na lisilo na mipaka. Lakini nyuma ya safari ya kila ndege kuna mfumo maalum wa njia za angani zilizopangwa na kudhibitiwa kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha ndege zinafika salama kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Ndege haziruki tu katika mwelekeo wowote zinapotaka. Zinafuata njia maalum zinazojulikana kama 'Airways au Air Corridors, ambazo zimeainishwa na mamlaka za usafiri wa anga kwa ajili ya kupanga na kudhibiti mtiririko wa ndege.

Moja ya mambo muhimu katika mfumo huo ni urefu wa ndege angani. Njia za ndege hutenganishwa kwa viwango tofauti vya urefu vinavyojulikana kama Flight Levels.

Kwa mfano, ndege inaweza kuwa katika Flight Level 330, sawa na takribani futi 33,000, huku nyingine ikiwa Flight Level 370, takribani futi 37,000.

Hivyo, ndege zinaweza kupita katika eneo moja la anga bila kuwa katika kiwango kimoja cha urefu, jambo linalosaidia kupunguza hatari ya migongano.

Lakini si urefu pekee unaoongoza safari. Ndege pia hutumia Waypoints, ambazo ni sehemu maalum zilizowekwa kwenye mfumo wa urambazaji wa anga (Air Navigation).
Rubani na mifumo ya ndege hutumia taarifa hizi kufuata njia iliyopangwa kutoka wakati wa kuondoka hadi kufikia eneo la kutua.

Katika safari hiyo, waongiza ndege 'Air Traffic Control (ATC) huwa na jukumu muhimu la kufuatilia na kupanga mienendo ya ndege angani. Waongoza ndege huwapa marubani maelekezo kuhusu mwelekeo, urefu na mabadiliko ya njia pale inapohitajika, kulingana na hali ya anga na msongamano wa ndege.

Jambo jingine linalozingatiwa ni hali ya hewa na matumizi ya mafuta. Njia ya ndege inaweza kubadilishwa ili kuepuka maeneo yenye dhoruba, upepo mkali au hali nyingine hatarishi. Wakati mwingine, ndege pia hupanga njia zinazoweza kunufaika na upepo wa juu angani, ikiwemo jet streams, ili kupunguza muda wa safari na matumizi ya mafuta.

Kwa hiyo, kila unapouona ndege ukipita juu yako, ujue kuwa nyuma ya safari hiyo kuna mfumo mkubwa wa urambazaji, mawasiliano, teknolojia na udhibiti wa anga.

Anga linaweza kuonekana kuwa wazi na lisilo na mipaka, lakini kwa ndege, kuna “barabara” zisizoonekana ambazo zinahitaji kufuatwa kwa usahihi mkubwa ili kuhakikisha usalama wa safari.
 
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imesimamisha mara moja Cheti cha Uendeshaji Ndege (AOC) cha TRACEP Congo Aviation, kufuatia ajali ya ndege aina ya Let 410 UVP iliyotokea Ijumaa karibu na Kenge, mkoani Kwango.

Ajali hiyo, iliyohusisha ndege yenye usajili 9S-GUC, ilisababisha vifo vya watu 17, wakiwemo abiria 13 na wafanyakazi wanne, pamoja na maafisa wawili wa ngazi za juu wa kijeshi.

Kwa mujibu wa Wizara ya Uchukuzi ya DRC, shughuli zote za TRACEP Congo Aviation zimesimamishwa nchini kote hadi kukamilika kwa uchunguzi unaoendeshwa na BPEA, chombo kinachohusika na uchunguzi wa ajali za anga.
 
Kuanzia Oktoba 1, 2026, wasafiri wa kigeni wanaoingia Tanzania Bara kupitia viwanja vya ndege, bandari au mipaka ya nchi watahitajika kuwa na bima ya lazima ya safari (Inbound Travel Insurance) yenye gharama ya Dola 44 za Marekani kwa mtu mmoja.

Kwa mujibu wa Government Notice No. 256, iliyochapishwa katika Gazeti la Serikali tarehe Septemba 4, 2026, bima hiyo itatolewa kupitia National Insurance Corporation (NIC) na itakuwa na uhalali wa hadi siku 92.

Bima hiyo itagharamia huduma mbalimbali ikiwemo matibabu ya dharura, uokoaji wa kitabibu, kurejeshwa kwa mgonjwa au mwili wa marehemu, pamoja na upotevu wa mizigo.

Hata hivyo, raia wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wameondolewa kwenye sharti hilo.
 
Mnamo Juni 10, 1990, safari ya kawaida ya ndege ya British Airways (Flight 5390) iliyokuwa ikitoka Birmingham kuelekea Malaga nchini Hispania iligeuka kuwa moja ya matukio ya ajabu na ya kusisimua zaidi katika historia ya usafiri wa anga duniani.

Ndege hiyo aina ya BAC One-Eleven ilipofika mwinuko wa futi 17,300 juu ya Didcot, Oxfordshire, ghafla kioo cha kushoto cha chumba cha marubani kiling'oka kutokana na shinikizo kubwa la hewa, hatua iliyosababisha Nahodha Tim Lancaster kuvutwa ghafla kuelekea nje ya ndege kupitia tundu hilo.

Kwa wepesi na ujasiri wa hali ya juu, mhudumu wa ndege Nigel Ogden aliyekuwa ndani ya chumba hicho alikimbia na kuwahi kuishika miguu ya nahodha huyo kabla hajatupwa kabisa angani, huku nusu ya juu ya mwili wa Lancaster ikiwa imelala juu ya paa la ndege ikipigwa na upepo mkali wenye kasi ya zaidi ya kilomita 600 kwa saa na baridi kali ya nyuzi joto -17 (chini ya sifuri)

Licha ya joto kupungua ghafla, ukungu mzito kutanda ndani ya chumba cha rubani, na karatasi pamoja na vifaa kupeperushwa, rubani msaidizi Alastair Atcheson alichukua usukani mara moja, akashusha ndege hiyo kwa dharura ili kurejesha oksijeni inayoweza kuvutwa, na kuanza kuelekea uwanja wa ndege wa Southampton.

Wahudumu wengine walimsaidia Ogden kumshikilia Lancaster kwa nguvu licha ya nguvu kubwa ya upepo, wakiamini hata kama alikuwa amepoteza maisha walipaswa kuhifadhi mwili wake usinyonywe na injini ya ndege.

Baada ya dakika kadhaa za mapambano ya kukata na shoka angani, Atcheson alifanikiwa kutua salama Southampton ambapo timu za uokoaji zilimkuta Lancaster akiwa bado hai kimiujiza, akiwa na majeraha ya baridi kali na mivunjiko midogo, na baada ya kupata matibabu alipona kikamilifu na kurejea tena kazini kurusha ndege za abiria.

Baada rubani Lancaster alitoa simulizi ya jinsi alivyoona mkia wa ndege na injini zikifanya kazi akajua ndiyo mwisho wa maisha yake kabla ya kuooteza fahamu.
 
Ukiangalia bodi ya ndege, utaona una mistari mingi ya misumari ya riveti ndogo zinazoshikilia vipande vya chuma pamoja.

Tofauti na baadhi ya magari na vyuma vingine, sehemu nyingi za ndege hazijaunganishwa kwa kutumia moto wa kuchomelea.

Sababu kubwa ni usalama na uimara. Ndege hupitia misukosuko, mabadiliko ya shinikizo "Pressure" na msongo mkubwa wakati wa kuruka na kutua.
Riveti husaidia kusambaza nguvu hizo vizuri kwenye sehemu mbalimbali za ndege.

Pia, kutumia moto wa kuchomelea kuunganisha baadhi ya vyuma vya ndege kunaweza kubadilisha ubora na uimara wa chuma kutokana na joto kali.
Riveti hazizalishi joto hilo.

Faida nyingine ni kwamba riveti ni rahisi kukaguliwa na kubadilishwa ikiwa imeharibika.
Hii hurahisisha matengenezo ya ndege.

Hata hivyo, ndege za kisasa zinaweza kutumia pia teknolojia maalumu za kuunganisha chuma kwa moto wa kuchomelea katika baadhi ya sehemu.

Kwa hiyo, si kwamba ndege haziwezi kuunganishwa kwa moto, bali riveti huchaguliwa katika maeneo mengi kwa sababu ya usalama, uimara na urahisi wa matengenezo.
 
BURUDANI!

Kumbukizi:

Kundi la maprofesa wa sayansi liliitwa kupanda ndege kwaajili ya safari ya uzinduzi wa ndege mpya.

Baada ya wote kuingia na milango kufungwa, walipewa taarifa kupitia spika ya matangazo kuwa; Ndege hiyo ilitengenezwa na wanafunzi wao waliowafundisha”

Mara tu waliposikia hivyo, maprofesa wote wakaanza kukimbilia mlangoni, wakiomba washushwe kutoka kwenye ndege hiyo.

Lakini kulikuwa na profesa mmoja aliyebaki ameketi kwa utulivu kabisa akiwa akisoma gazeti, akiwa hana hofu yoyote

Mtoa tangazo akamuuliza,
“Mbona huhangaiki kushuka kama wenzako?”

Profesa akajibu kwa kujiamini:
Kwasababu nawajua wanafunzi wangu vizuri.

Mtu huyo akashangaa na kumuuliza tena:
“Kwahiyo una uhakika uliwafundisha vizuri?”

Profesa akatabasamu na kusema:
“Kama ni wanafunzi wangu kweli walishiriki kutengeneza hii ndege, nina hakika kabisa haifiki hata kwenye njia ya kurukia ndege, wacha kupaa.
😊
 
Picha hii inaonyesha Pan American Airways Boeing 314 California Clipper (NC18602) ikiwa juu ya maji ya Puget Sound, Washington, mwaka 1939. Boeing 314 ilikuwa ndege kubwa ya majini (flying boat) iliyoundwa na Boeing kwa safari za masafa marefu za Pan Am.

California Clipper ilikuwa Boeing 314 ya kwanza kukabidhiwa Pan Am, tarehe 27 Januari 1939. Ilianza safari zake za Pacific na tarehe 29 Machi 1939 ikaanzisha huduma ya kawaida ya abiria kwenye njia ya San Francisco–Hong Kong kupitia vituo kadhaa vya Pacific.

Ndege hiyo baadaye ilijulikana kama Pacific Clipper, na ikapata umaarufu mkubwa baada ya kufanya safari ya karibu kuizunguka dunia mwishoni mwa 1941 hadi Januari 1942, kufuatia kuzuka kwa Vita vya Pili vya Dunia na shambulio la Pearl Harbor.

Hii ni moja ya ndege zilizowakilisha mwanzo wa zama za safari za kimataifa za abiria kwa ndege za majini kipindi ambacho safari za kuvuka bahari zilikuwa tukio kubwa sana katika historia ya usafiri wa anga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…