Mustakabali wa usafiri wa anga wa Dubai umewekwa kwa uthabiti kwenye Kituo Kikuu cha Dunia cha Dubai maarufu kama Dubai World Central (DWC) - ikiwemo Uwanja wa Ndege mpya wa Kimataifa wa Al Maktoum, katika maandalizi ya kuhama kiwanja cha ndege cha sasa cha Dubai International (DXB) ambao unakaribia kikomo chake cha kufanya kazi.
Paul Griffiths, Mkurugenzi Mtendaji wa Viwanja vya Ndege vya Dubai, amethibitisha kwamba mabadiliko kamili ya ujenzi wa DWC sio tu mpango, lakini ni lazima, na lengo thabiti lililowekwa kwa mwaka 2032.
Griffiths alibainisha kuwa, licha ya maboresho yanayoendelea katika mifumo, teknolojia, na miundombinu, DXB inaweza tu kupanua uwezo wake kwa sasa.
"Tunafikiri tunapofikia takriban abiria milioni 110-115, tutafikia kikomo ya kile ambacho DXB ina uwezo wa kuhudumia," alielezea.
DXB, kwa sasa ndio uwanja wa ndege wenye shughuli nyingi zaidi duniani kwa abiria wa kimataifa, inakadiriwa kufikia uwezo wake wa juu zaidi wa takriban abiria milioni 110-115.
Sampuli ya mradi wa kiwanja kipya cha ndege cha kimataifa cha Al Maktoum sasa kipo kwenye maonesho ya anga ya Dubai.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Maktoum (DWC), unaojulikana pia kama Dubai World Central, unafanyiwa upanuzi mkubwa na kuwa uwanja mkubwa zaidi wa ndege duniani, wenye makadirio ya uwezo wa kubeba abiria milioni 260 kila mwaka.
Mradi huu kabambe utakuwa mara tano ya ukubwa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai (DXB).
Upanuzi huo, unaokadiriwa kugharimu dola bilioni 35, unajumuisha njia 05 za kuruka na ndege sambamba, milango 400 ya ndege, na kituo kikuu cha siku zijazo iliyoundwa kushughulikia ongezeko la abiria na mizigo.