Mada maalum: Mchakato wa udahili vyuo vya afya

Kizibo255

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
508
367
Baada ya kuona kuna mkanganyiko mkubwa, nimeamua kuwaelewesha wenzangu wanaotaka kusomea mambo ya nursing kwa kozi yoyote ile.

1. CERTIFICATE (Ngazi ya cheti)

Mwombaji awe na D TATU ktk masomo ya sayansi PCB(Physics, Chemistry na Biology)
Hii inajumuisha vyuo vya serikali na binafs(Private)
Kama huna sifa hizo USIJARIBU ktk chuo chochote kwan utapotezewa muda

2. DIPLOMA (Stashahada)

Kama ni form 4, uwe na C katik BC (Bios na Chemistry) na D au zaid ya Physics.

NB: Sifa zote za ufaulu ziwe katika kikao kimoja cha mtihani.

Naamini sasa wale wanaouliza watakuwa na majibu sahihi!
Mungu akipenda nitaweka baadhi ya vyuo vya afya vipatavyo 30 ili kwa wale wenye sifa wachague.

NAWASILISHA!

ORODHA YA VYUO VYA AFYA TANZANIA (Haijakamilika)

  1. Tosamaganga School of Nursing, Iringa
  2. RAO Health Centre
  3. Royal Pharmacy Training Institute, Dar es Salaam
  4. Tarime School of Nursing, Mara
  5. IMTU, Dar es Salaam
  6. Hubert Kairuki School of Nursing, Dar es Salaam
  7. Shaabani Robert
  8. Mount Ukombozi, Dar es Salaam
  9. KAM College, Dar es Salaam
  10. Rubya School of Nursing, Muleba
  11. Same School of Nursing, Same
  12. Bulongwa School of Nursing, Bulongwa
  13. School of Dental Therapist, Bulongwa
  14. School of Dental Therapist, Mbeya
  15. School of Optometry
  16. School of Physiotherapy, Moshi
  17. Sengerema School of Nursing
  18. Sharati School of Nursing, Rorya
  19. Singida Health Science Laboratory Assistants Training Centre, SINGIDA
  20. St. Aggrey College of Health Sciences
  21. St. Gaspar Nursing School, SINGIDA
  22. St. Magdalena school of nursing KAGERA
  23. Sumaye school of nursing KWIMBA
  24. Suve health institute ARUSHA
  25. Tandabui institute of health sciences Mwanza
  26. Training centre health records technology Moshi
  27. Primary health care
  28. Tanga school of nursing
  29. Health training centre Ifakara
 
Jamani naombeni mnisaidie kujua vyuo vya afya hapa Tanzania kwasababu nataka kujiunga na chuo chochote cha afya sector ya clinical officer nina matokeo ya form four....nimepata four.26 .
 
Division 4 point 26 kwa upande wa degree sidhani labda ujaribu Diploma na labda kuanzia Nursing labda utafanikiwa..Kila heri.
 
Kuna chuo cha clinical officers pale kibaha (COTC) Ni kizuri sana kuanzia mazingra ya kujisomea na kila kitu ,ila kinatoa certificate na diploma.
 
Kuna chuo cha clinical officers pale kibaha (COTC) Ni kizuri sana kuanzia mazingra ya kujisomea na kila kitu ,ila kinatoa certificate na diploma.

Private or gover na ada shiling ngapi?
 
Ni goverment na kwa marks zako moja kwa moja wanakuchuku, ada sina uhakika sana ila ts about lak 5 -lak 7>am not sure kwa hlo.
 
Je kama una C ya Bio na C ya chemia D ya phy math D na engl D inawezekana kusoma dip?

Unapata coz diploma wanataka C ya bios na chem den uwe na D za phy ,eng, math au zaid, wahi haraka coz kuna ushindani sana now.
 
Je kama una C ya Bio na C ya chemia D ya phy math D na engl D inawezekana kusoma dip?

Sikukatishi tamaa, lakini kwa vyuo vya gvt ni ngumu labda wende private.
Mimi binafsi nina c kwa masomo yote ya sayans niliomba mwaka uliopita nikakosa. Kuna mwenzangu alikua na kama mimi ila alinizid kwa kuwa na B ya biology aliekwa reserve mpk keshaenda private ndo anapigiwa simu aende
Wanaoomba gvt wanakua weng na kunakua na competition kubwa
 
Mdogo wangu ana IV pts 29 "D" CHEM,D BIOS,D PHYCS,D ENG,D GEO,D KISW, AFU F THE REST, ANAWEZA KUPATA NAFASI NA KUPATA AJIRA BAADAE?
 
Jamani naombeni mnisaidie kujua vyuo vya afya hapa tanzania kwasababu nataka kujiunga na chuo chochote cha afya sector ya clinical officer nina matokeo ya form four....nimepata four.26 .
Ka reset mtihani hayo matokeo yako hayafai kumchoma mtu sindano..!!!Labda ng'ombe. Au kasukume chaki Ngumbaru..angghrrr eti Afya...nani kakudanganya,??? Mimi nilianza na Diploma lakin sikucheza miaka minne darasani na kutoka na hicho kiwango chako. Unaaibisha fani yangu.!!!:embarassed2:
 
Je kama una C ya Bio na C ya chemia D ya phy math D na engl D inawezekana kusoma dip?

Jamani nadhan hamkunielewa mbona cna F hata moja mabaya kvp coz yaliobak zote D
 
Jamani naombeni mnisaidie kujua vyuo vya afya hapa tanzania kwasababu nataka kujiunga na chuo chochote cha afya sector ya clinical officer nina matokeo ya form four....nimepata four.26 .

Minimum qualification ni D katika Chemistry, Phyisics, Biology. Iwapo utasoma chuo cha private na wakakubali kukusomesha ukewa na F katika moja ya masomo hayo tatizo litakuja katika kuajiriwa hasa serikalini.
 
Nina chem&bio-C na mangine yote nina D.
 
Jf' ina watu watu vituko sana mdogo wangu vumilia matusi hayaruhusiwi najua umekurupuka haujasoma jf' rules, usitukane utapigwa Ban halafu hata shida yako haijatimia.
Kwa matokeo uliyonayo clinical officer ngazi ya cheti private au government unachaguliwa bila wasiwasi we omba kwote kisha ungojee majibu.
Si uhakika kwamba mtu aliyemaliza four 4 anaweza jiunga na chuo kusoma diploma sijawahi ila ufahamu wangu unaonyesha lazima upitie cheti then kwa cheti unarukia diploma na hata degree. Diploma wanaenda four 6 directly wakiwa qualification za kuingia huko.
Karibu jf'
 
Hebu pigeni hiyo ban nione kwani mtanifanya nn mkinipiga hiyo ban ntakufa,ntashindwa kulala au sitapata msosi acheni bit za majani
 
Back
Top Bottom