Mada maalum:Je umetenga asilimia ngapi ya kipato chako kwa ajili ya wazazi wako?

Inategemea, siyo kila mzazi anataka au kuhitaji pato la mwanae wapo wazazi ambao wao bado wanatoa mitaji kwa watoto wao ili wasimame. Sasa mzazi wa hivyo unampelekea kijipesa chako cha kijinga atashangaa.

Ila iko hivi waweza kununua zawadi itakayo beba maana tofauti na pesa ukawapelekea watashukru sana na kuona unajua kushow love kwao.

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna kama mzazi hasa kwangu mimi Mama ndio kila kitu changu,wakati wa uhai wake hela yangu yeye ndio anajua
nna kiyasi gani kwenye account,na anayo card yake anaweza kuchukua hela kwenye account yangu wakati wowote,na hata mfano anataka kuchukua hua ananambia naomba nitoe hela,namwambia Mama usiombe chukua,siwezi kumpa shoga wala sadaka kabla mzazi wangu pepo iko chini ya miguu yake na mimi nimwanamke kama yeye najua Adhabu ya kua mzazi,ila Baba nampa lakini sio kama Mama...
 
Inategemea, siyo kila mzazi anakata mpaka kuhitaji pato la mwanae wapo wazazi ambao wao bado wanatoa mitaji kwa watoto wao ili wasimame. Sasa mzazi wa hivyo unampelekea kijipesa chako cha kijinga atashangaa.

Ila iko hivi waweza kununua zawadi itakayo beba maana tofauti na pesa ukawapelekea watashukru sana na kuona unajua kushow love kwao.

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app

Nimeeleza pia kuhusu wenye uwezo kushinda wewe waweza kuwaandalia zawadi kwa wakati fulani kumjali mzazi sio lazima pesa tasilimu
 
Asante sana kwa transformative thread kama hii. Kikweli wengi hatuna fungu maalum kwa ajili ya wazazi wetu. Binafsi huwa najisahau wakati mwingine kutimiza huu wajibu. Mfano ni leo hii najua huwa kila jumapili ya mwisho wa mwezi nimnunulie mama hisa ila nimejisahau hadi kanikumbusha.
Mungu atujalie tuwajali wazazi wetu maana wao ndio wametufikisha hapa tulipo. Ila malipo tunayowapa ni uchungu na vilio kwa baadhi yetu
 
Asante sana mkuu kwa uzi mzuri!
Yaani natamani sana kufika mahali ambapo ntakua na uwezo wa kupeleka angalau gunia la unga au mchele kwa wazazi... Kwa kidogo nnachopata hua nahakikisha kila nikienda kuwasalimia siendi mikono mitupu... Nikishindwa kabisa nanunua ata Fursana (mama anapenda sana hii kitu )... Naomba nifanikiwe zaidi ili nizidi kuwahudumia.
 
Usijar Mungu atakufanyia wepesi
 
kimsingi hmna kiwango kinachokidhi kuwapa wazazi.Thamani yao ni kubwa sana ila kujitahidi kuwapatia chochote kilicho ndani ya uwezo wako.
NB:Sio lazima wala sheria bali ni utaratibu wa binadamu kutunza njia iliyomfikisha pahala fulani.
 
Wazazi walikuzaa ili uwasaidie na wewe unazaa uje usaidiwe kweli umaskini hauwezi isha
 
Back
Top Bottom