Waliopo mtaani pia baadhi yao huja mitandaoni.Hutokea kama nasibu tuu mtandao kuwa sehemu mojawapo ya kukutana na mwenza wako kama ilivyo kwenye usafiri, harusini, masomoni , msibani nk...
Kwangu shida ni pale akili inapotumwa kuja mitandaoni kutafuta wenza, maranyingi watu hao huishia kwa kuridhisha tamaa za mwili huku wengine wakibanwa na kitu kama ujauzito kuoana ama mmoja kugangamala na kung'ang'aniza kuingia ndoani baada ya kuona alichokuwa akikitamani kimejileta...
Pia kuna wale wanye kasoro fulani za kimwili (maumbile na ulemavu) na kiakili baada ya mitaa kuwakwepa huamua kuwatafuta wasiowajua na kuwaingiza ndoani kuja kushtuka ushaapa kwenye shida na raha