Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,768
- 3,621
Katika karne hii ya 21 imekuwa ni kawaida sana kwa watu hasa vijana kutafuta wapenzi ama wenzi wa maisha mitandaoni. Lakini swali linakuja; Je ni sahihi kutafuta mpenzi mtandaoni au la?
Jibu la hilo swali linaweza kuwa ndio au hapana na nitalezea kama ifuayavyo kwa nini naweza kukubali au kukataa kuhusiana na hili swala la kutafuta mpenzi mtandaoni:
NDIO
Naweza kukubaliana kuhusu hili swala la kutafuta mpenzi mtandaoni kwa sababu katika ulimwengu huu hakuna sheria au andiko kutoka katika vitabu vya dini ambavyo vinatamka kuwa mpenzi ama mwenzi wa maisha anapaswa kutafutwa wapi ama atatoka wapi. Hiyo imefanywa hivyo kwa makusudi ili kutoa uhuru kwa mwanadamu kutafuta mpenzi au mwenzi wa maisha popote ambapo yeye anaona panafaa.
Lakini kwenye vitabu vya dini vinazungumza ya kuwa mwenzi bora wa maisha anatoka kwa Mungu kitu ambacho ni sahihi kabisa kwa sababu Mungu ndiye muumba wa vitu vyote na anajua yote na ni yeye pekee ndiye mwenye kujua ni mwenzi yupi akufaaye.
Lakini wengi wetu huwa tunatafsiri vibaya haya maandiko. Wengi wetu hudhani kuwa kwa kuwa maandiko yanasema kuwa mwenzi bora wa maisha anatoka kwa Mungu, basi ni lazima mwenzi huyo umpate kwenye sehemu za kuheshimika au sehemu za ibada kama vile kanisani. Lakini tunasahau kuwa Mungu ndiye muumba wa vitu vyote na yeye pekee ndiye mwenye mamlaka juu ya vitu vyote vilivyopo mbinguni na duniani hivyo anaweza kutumia kitu ama kiumbe chochote kufanya kazi yake. Hivyo Mungu huyo huyo anaweza kutumia hata mtandao kukupa mwenzi wa maisha.
HAPANA
Kutafuta mpenzi kwenye mitandao kunaweza kusiwe sahihi endapo lengo la kutafuta mpenzi huyo ni kwa ajili ya kufanya uzinzi na uasherati na mwisho wa siku badala ya kupata kilicho chema utaishia kupata takataka na vilivyo oza.
Kutafuta mwenzi wa maisha kunaweza kusiwe sahihi ama kusiwe na manufaa endapo utakurukupuka na kuamua kutafuta mpenzi mtandaoni bila ya kuomba msaada wa Mungu ili akuangazie uweze kumtambua huyo mwenzi bora wa maisha maana mwenzi bora wa maisha hana alama usoni, kwenye umbo, mali au mavazi ambayo sisi ndio tunayashabikia sana. Yeye pekee ndiye anayeweza kukusaidia kumtambua huyo mwenzi wa maisha.
Pia kutafuta mwenzi wa maisha kunaweza kusiwe sahihi endapo utawekeza nguvu, mawazo na akili yako yote kwenye kutafuta mpenzi mtandaoni pekee. Mtu anayetafuta mpenzi au mwenzi wa maisha anapaswa kuhangaika huku na kule kama simba atafutaye mawindo porini maana huwezi jua mwenzi wako utampata wapi.
HITIMISHO
Mimi ni binadamu, kiumbe dhaifu niliye vumbi na jivu na neno langu sio sheria maana mimi sio mkamilifu, naweza kuwa sahihi ama nisiwe sahihi. Hivyo nakaribisha, maoni, maswali, mawazo au ushauri kutoka kwenu wadau.
Nawasilisha!!!