Mada: Je, ni sahihi kutafuta mpenzi mtandaoni?

Mada: Je, ni sahihi kutafuta mpenzi mtandaoni?

Mapenz huanzia popote
Haijalish uko wap kujiamin
Kwako ndo kunakupa mwenza

Watu wanatongozana hata
Kwa mazish
Kujiamini kwako kunaweza kukupa mwenzi lakini kujiamini huko kunaweza kusikupe mwenzi bora wa maisha.
 
Mpenzi anatafutwa kwa njia yoyote halali. Jambo kuwa sahii au la ni suala la mapokeo siyo la uhalisia.
Unaposema ni swala la mapokeo na sio uhalisia unamaanisha nini mkuu? Naomba ufafanuzi tafadhali.
 
Mimi mwenyewe wakwangu sikumpata mtandaoni na ninatamani hata sa ivi apelekwe uhamishoni Syria tena kule kwenye mji wa Alepo wenye mapambano makali akaishi huko
Si vyema kumuombea mwenzako mabaya hata kama amekosea maana sote ni wakosefu na hakuna aliyemkamilifu.
 
Mmenikumbusha kutafuta mchepuko ngoja niingie badoo nikatafute mrupo nile nao raha wiki ijayo maana ni wiki ya mshahara
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]

Hakuna mchezo mkuu n mwendo tu wa kula bhata
 
Unaposema ni swala la mapokeo na sio uhalisia unamaanisha nini mkuu? Naomba ufafanuzi tafadhali.
Waingereza wanasema perception. Hakuna kitu kama sahii na kisicho sahii, ni mtazamo wako tu, mfano kikwetu kaka yako akifiwa na mke wake unaweza kumrithi, hii ni mila yetu na kwa miaka mingi tumeanini hivyo na tumechukulia (perceive) kuwa sahii. Sasa wakaja wazungu na mtazamo (perception) tofauti na sisi tuka give in. Hivyo hivyo kwenye mambo mbali mbali kama dini na siasa mitazamo (perception) ndiyo inayofanya watu wasikubaliane kwenye usahii wa mambo na vitu mbali mbali. nadhani umeelewa sasa.
 
Waingereza wanasema perception. Hakuna kitu kama sahii na kisicho sahii, ni mtazamo wako tu, mfano kikwetu kaka yako akifiwa na mke wake unaweza kumrithi, hii ni mila yetu na kwa miaka mingi tumeanini hivyo na tumechukulia (perceive) kuwa sahii. Sasa wakaja wazungu na mtazamo (perception) tofauti na sisi tuka give in. Hivyo hivyo kwenye mambo mbali mbali kama dini na siasa mitazamo (perception) ndiyo inayofanya watu wasikubaliane kwenye usahii wa mambo na vitu mbali mbali. nadhani umeelewa sasa.
Nimekuelewa mkuu...
 
Kwenda mtandaoni kwa lengo la kutafuta mwenza ni udhaifu na ni hatari sana, ila unaweza connect na mtu kupitia mtandao na mambo yakajipa.
well said,
hapa ndiyo watu hu`mix concepts, coz hao waliona accounts mitandaoni ndiyo hao hao wananchi huenda, kanisan, shuleni, sokon, sehem za starehe, etc, so when you connect mtakua more close kujuana unless otherwise nyie mnataka kujuana online na ndoa yenu mfungie facebook or thru Skype, bila kuonana in person.
 
Nionavyo huwa ni mara chache sana kupata mwenza aliyesahihi kupitia mtandao kwani kuna ugumu wa kujua nia ya mtu ya moyoni kwani pale unapotafuta mwenza wanaweza wakaja hata wanaume zaidi ya kumi lakini wote wakawa hawana nia ya mahusiano ya kudumu.

Tofauti na yule anayekufuata uso kwa uso ni rahisi kimgundua mienendo yake na hata tabia zake na ukazijua kwa haraka tofauti na mitandaoni ambapo unaweza ukachati na mtu hata zaidi ya mwaka kumbe ana familia yake na wewe huwezi kujua.

Na upande wa jinsia pia ni vigumu kujua mia kwa mia kama unayechati naye ni jinsia kama yako kwani kuna wengine ni wanawake wanaweka profile za kiume.

Hivyo ni vyema kupata mwenza nje ya mitandaoni.
hapa ndiyo watu hu`mix concepts, coz hao walio na accounts mitandaoni ndiyo hao hao wananchi huenda, kanisan, shuleni, sokon, sehem za starehe,etc. so when you connect mtakua more close kujuana unless otherwise nyie mnataka kujuana online na ndoa yenu mfungie facebook or thru Skype, bila kuonana in person. and again its all in one`s MIND!
 
Ukiona hivyo mtu huyo yuko katika jockey, ila watu hawasomi atama za nyakati na kutuma no za simu sasa uliza uwa wanajibiwa. Japo kuwa nimeshudia watu walio oana na kutoka fb! Ila kwa mimi uwa siamini kabisa .ila wapo wabaya na wazuri.
 
Katika karne hii ya 21 imekuwa ni kawaida sana kwa watu hasa vijana kutafuta wapenzi ama wenzi wa maisha mitandaoni. Lakini swali linakuja; Je ni sahihi kutafuta mpenzi mtandaoni au la?

Jibu la hilo swali linaweza kuwa ndio au hapana na nitalezea kama ifuayavyo kwa nini naweza kukubali au kukataa kuhusiana na hili swala la kutafuta mpenzi mtandaoni:

NDIO
Naweza kukubaliana kuhusu hili swala la kutafuta mpenzi mtandaoni kwa sababu katika ulimwengu huu hakuna sheria au andiko kutoka katika vitabu vya dini ambavyo vinatamka kuwa mpenzi ama mwenzi wa maisha anapaswa kutafutwa wapi ama atatoka wapi. Hiyo imefanywa hivyo kwa makusudi ili kutoa uhuru kwa mwanadamu kutafuta mpenzi au mwenzi wa maisha popote ambapo yeye anaona panafaa.

Lakini kwenye vitabu vya dini vinazungumza ya kuwa mwenzi bora wa maisha anatoka kwa Mungu kitu ambacho ni sahihi kabisa kwa sababu Mungu ndiye muumba wa vitu vyote na anajua yote na ni yeye pekee ndiye mwenye kujua ni mwenzi yupi akufaaye.

Lakini wengi wetu huwa tunatafsiri vibaya haya maandiko. Wengi wetu hudhani kuwa kwa kuwa maandiko yanasema kuwa mwenzi bora wa maisha anatoka kwa Mungu, basi ni lazima mwenzi huyo umpate kwenye sehemu za kuheshimika au sehemu za ibada kama vile kanisani. Lakini tunasahau kuwa Mungu ndiye muumba wa vitu vyote na yeye pekee ndiye mwenye mamlaka juu ya vitu vyote vilivyopo mbinguni na duniani hivyo anaweza kutumia kitu ama kiumbe chochote kufanya kazi yake. Hivyo Mungu huyo huyo anaweza kutumia hata mtandao kukupa mwenzi wa maisha.

HAPANA
Kutafuta mpenzi kwenye mitandao kunaweza kusiwe sahihi endapo lengo la kutafuta mpenzi huyo ni kwa ajili ya kufanya uzinzi na uasherati na mwisho wa siku badala ya kupata kilicho chema utaishia kupata takataka na vilivyo oza.

Kutafuta mwenzi wa maisha kunaweza kusiwe sahihi ama kusiwe na manufaa endapo utakurukupuka na kuamua kutafuta mpenzi mtandaoni bila ya kuomba msaada wa Mungu ili akuangazie uweze kumtambua huyo mwenzi bora wa maisha maana mwenzi bora wa maisha hana alama usoni, kwenye umbo, mali au mavazi ambayo sisi ndio tunayashabikia sana. Yeye pekee ndiye anayeweza kukusaidia kumtambua huyo mwenzi wa maisha.

Pia kutafuta mwenzi wa maisha kunaweza kusiwe sahihi endapo utawekeza nguvu, mawazo na akili yako yote kwenye kutafuta mpenzi mtandaoni pekee. Mtu anayetafuta mpenzi au mwenzi wa maisha anapaswa kuhangaika huku na kule kama simba atafutaye mawindo porini maana huwezi jua mwenzi wako utampata wapi.

HITIMISHO
Mimi ni binadamu, kiumbe dhaifu niliye vumbi na jivu na neno langu sio sheria maana mimi sio mkamilifu, naweza kuwa sahihi ama nisiwe sahihi. Hivyo nakaribisha, maoni, maswali, mawazo au ushauri kutoka kwenu wadau.

Nawasilisha!!!
its all in one`s mind.. the way dunia inabadilika its the way mambo nayo yanabadilika, so its one`s choice ambayo anaona ni suitable kwake, wanaifata tuu.
 
Hakuna tatizo lolote lile. Mtandaoni ni kama uraiani tu watu wanakutana mitandaoni wanapendana na baadhi hufikia hata kufunga pingu za maisha na watoto wakapata na ndoa zao zikadumu kipindi kirefu. Kule India mitandao ndiyo inatumika kutafuta wachumba kuliko sehemu nyingine yoyote ile.
Tatizo bongo watu katika mtandao wanachukulia ni sehemu ya kujitoa ufahamu na kuwa na matusi kibao ila mataifa mangine inaunganisha watu tena sana unajua mtu huwezi kumbadirisha mtu ili awe mstarabu kama ulivyo wewe ata siku 1.
 
Ni ipi tofAuti ya raia wa mtandaoni na raia wa uraiani+?
 
Mke mwema hutoka kwa Bwana, mi nafikiri kwamba na mazingira nayo huchangia katika kumtafuta yule ambaye unaona atakufaa.
 
Katika karne hii ya 21 imekuwa ni kawaida sana kwa watu hasa vijana kutafuta wapenzi ama wenzi wa maisha mitandaoni. Lakini swali linakuja; Je ni sahihi kutafuta mpenzi mtandaoni au la?..............................................................................

Pia kutafuta mwenzi wa maisha kunaweza kusiwe sahihi endapo utawekeza nguvu, mawazo na akili yako yote kwenye kutafuta mpenzi mtandaoni pekee. Mtu anayetafuta mpenzi au mwenzi wa maisha anapaswa kuhangaika huku na kule kama simba atafutaye mawindo porini maana huwezi jua mwenzi wako utampata wapi.............................................

Hivyo nakaribisha, maoni, maswali, mawazo au ushauri kutoka kwenu wadau.

Nawasilisha!!!
Uko sawa mkuu. Ni vizuri kumshirikisha Mungu alie msaada wetu kwa kila jambo kwa wale waaminio.
 
Si vyema kumuombea mwenzako mabaya hata kama amekosea maana sote ni wakosefu na hakuna aliyemkamilifu.
Mkuu kua uyaone.kabla ya kuishi na hawa viumbe wanakuaga watamu ila ukishaanza maisha ya jumla ndio utaona ubaya wao.
 
ukitafuta mpenzi mtandaoni mnasema ni kosa si sahihi mbona mkitafuta pesa mtandaoni huwa si kosa? tunawaona manetwork marketing wangapi wamewin kimaisha through mitandao?
 
Hakuna tatizo lolote lile. Mtandaoni ni kama uraiani tu watu wanakutana mitandaoni wanapendana na baadhi hufikia hata kufunga pingu za maisha na watoto wakapata na ndoa zao zikadumu kipindi kirefu. Kule India mitandao ndiyo inatumika kutafuta wachumba kuliko sehemu nyingine yoyote ile.
Uko sahihi mkuu, muhimu ni kukutana au starting point ni nini au wapi! Mbona kuna watu huanza kwa kupewa namba ya mtu na hajawahi muona....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom