Machupa kucheza ligi kuu ya Denmark | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Machupa kucheza ligi kuu ya Denmark

Discussion in 'Sports' started by Babuji, Dec 23, 2008.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Dec 23, 2008
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Mohamed Abdallah Machupa, amesema klabu hiyo imemdhalilisha vya kutosha, hivyo hafikirii kuichezea tena klabu hiyo.

  Akizungumza leo jioni, Machupa, ambaye kwa sasa yupo Tanzania akikamilisha taratibu za kujiunga na klabu yake mpya ya Aalborg BK 1885 ya Denmark, inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo, alisema kuwa Simba isahau kufikiria kumwita katika kikosi chake kutokana na vitendo alivyofanyiwa wakati anaichezea.

  Klabu ya Aalborg BK 1885 inashiriki katika michuano ya UEFA baada ya kushika nafasi ya tatu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kundi lililohusisha timu za Manchester United na Villareal, ambazo zilishika nafasi mbili za juu katika kundi hilo.

  Source : NIFAHAMISHE Tanzania news portal
   
 2. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2008
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni vyema tukajua amedhalilishwa kivipi. Mimi katika kumbukumbu yangu ni kwamba aliomba mwenyewe asisajiliwe katika kikosi cha Simba 2008/2009. Au jamaa walimtema halafu wakasingizia ameomba kuachwa?
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,154
  Likes Received: 1,245
  Trophy Points: 280
  Kiwango chake kilishuka, na kama ujuavyo timu zinakuwa zinakuhitaji pale tu unapokuwa katika peack, au yeye alitaka waendelee kubaki na jina. hata hao waDanish akiporomoka hawana deal naye. Take care
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  mambo ya kutukana wakunga wakati...

  aliondokea Simba kuja uingereza kwa mbwembwe za kucheza soka la kulipwa, akaishia kuchezea Hounslow FC, timu hata daraja la nne haipo ...kama Nonda Shaaban aliweza kucheza mpaka EPL, yeye alishindwa nini? au Discipline?!

  halafu akarudi Simba....

  sasa analalamika Simba 'walivyomfanyia', au kiwango chale kimeporomoka vibaya? mpira na ubishoo ni vitu viwili tofauti, bora aende 'kujilipua' tu huko abahatishe maisha, mpira umekwisha.

  Na yule mtoto wa Remmy, Kalimangonga Ongala naye aliishia wapi? naye alijaribiwa Bradford FC, hapa uingereza, nikasikia yupo Sweden...kisha kimyaaaaa...   
Loading...