Machozi ya Jakaya ni mawe yanayowapiga wapinzani na CCM wazawa

DsmicSound

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Messages
1,430
Points
2,000

DsmicSound

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2015
1,430 2,000
Na: George Kabadi

''Watanzania nimewaletea rais mnaemtaka"

Ni kauli iliyotoka kinywani mwa rais mustaafu Dr Jakaya Kikwete, ni kauli ya kiongozi anayeonyesha kufurahia mwisho wa uongozi wake kwa jamii.
Bila shaka Jakaya alikuwa amechoshwa na dhihaka, kutukanwa na kukejeliwa, hakika jamii ya vipofu wa fikra hawakuuona ubora wa Jakaya.

Yale matusi aliyotukanwa na wapinzani na kukosekana kwa uadilifu wa wateule wake, ambao ni wanaccm, nina uhakika Jakaya, alikuwa akilia na kumwachia Mungu awajibu watesi wake, kwa sababu;-

I) WANACCM WALIMWANGUSHA
:- Jakaya aliteua vijana wengi hasa wanaccm kushika nyadhifa mbalimbali, lakini wanaccm hao walimwangusha na kufanya atukane vya kutosha kwa maana waliopata fursa walitanguliza masrahi yao mbele na kuliacha taifa bila huduma muhimu, Jakaya aliyaona yote lakini alilia ki-faru John.

II) UHURU KWA VYAMA VYA UPINZANI
:- Katika uongozi wa Jakaya, wapinzani walau walipata uhuru kwa 75%, lakini uhuru huo waliutumia kumdhihaki na kumdhalilisha, walisema wazi wazi kuwa nchi imemshinda kwa sababu hakuna maendeleo yoyote aliyoyaleta.

Ki-uhalisia Jakaya anapaswa apongezwe tena pongezi kuu, watu wengi wasichokijua ni kuwa Jakaya ndiye---
:- Kujenga daraja la juu la Tazara, Dr Magufuli akiwa waziri wa ujenzi siku kadhaa kabla ya uchaguzi wa 2015.
:- Kujenga daraja la Nyerere(daraja la kigamboni)
:- Kujenga 50% ya shule za kata.
:- Kujenga barabara na Zahanati nyingi kuliko rais ye yote nchini.

Pamoja na kazi kubwa aliyokuwa akiifanya Jakaya, bado jamii haikuona thamani yake, lakini dunia inaijua thamani yake.

SWALI TAMU LINALOISHA KWA UCHUNGU NI:
Ivi ma-Daktari na Walimu mliokuwa mkiandamana kutwa kuchwa mkiomba kuongezwa mshahara, siku hizi mishahara mmeongezewa maana siwaoni mkiandamana?

Ivi wapinzani ule uhuru mliokuwa mnaupata na kuutumia kumdhihaki Jakaya, mbona siku hizi mnafanya mikutano kwenye magheto, vipi mmeupata uhuru mliokuwa mkimdai Jakaya?

:- Naweza kusema dunia haijawahi kumsaliti mtu, bali mtu husalitiwa na mtu. Mulimsaliti Jakaya kwa sababu ya hekima za ukimya wake, hamkutaka kumsikiliza wala kumuunga mkono, mlimtukana na kumuona hafai.
Msichokifahamu ni kuwa Jakaya alikuwa akilia na kumwachia Mungu, Machozi ya Jakaya ndiyo mawe yanayowapiga kimya kimya watesi wake.

Nadhani sasa akina William Ngeleja, Anna Tibaijuka na wanaccm wengine waliopewa nafasi na Jakaya wakamwangusha pamoja na akina Mdude, Roma, Tundu Lisu, Erick Kabendera na wengine waliokuwa wakiona Jakaya hafai nadhani leo ukiwakurupusha kwenye usingizi ukawaambia Jakaya atagombea 2020 kwa kauli moja wataitikia:
'' Twende na Jakaya 2020"

Kwa maana Machozi ya Jakaya ni mzimu unao-watesa wengi.
Usiutumie vibaya ukimya wa mtu mwenye hekima ya kukaa kimya, maana Mungu atakujibu kwa niaba yake.

''Magufuli ni jibu la dhambi zenu kwa Jakaya"

Kalamu Ya Mwebrania
Na: George Kabadi
0759 131 717
 

LIKE

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2013
Messages
3,468
Points
2,000

LIKE

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2013
3,468 2,000
rekebisha heading...andika 'machozi ya Pinda ni mawe yanayowapiga wapinzani na CCM wazawa'

NB:JK siyo wa kuwalilia wapinzani au hao CCM wazawa,na lait ingekuwa hivyo mamvi Leo hii ndio angekuwa Obama road

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,391,363
Members 528,393
Posts 34,079,096
Top