Hata leo kuna hoja kamahiyo iliibuka kwenye daladala kutoka tabata kwenda posta, tumetumia zaidi ya masaa mawili watu wamechoka,joto kali konda kadata basi ni hasira kwa kwenda mbele, ndipo mtu mmoja kasema '' kwa hali hii watu bado wanatoa kura kwa ccm'' kila mmoja kaja na lake wengine wanasema hatudanganyiki pamoja na mameseji ya kututisha, kila mtu anatoa simu yake na kuonyeshana zile meseji za kumchafua dr Slaa.
Chamsingi watu wengi washachoka na ccm, imebaki huko vijijini sana, watu hawasikii kuhusu ccm, Chadema tufanyeni kampeni za kukata nashoka sasa maana ccm wanachafua hali ya hewa. Kikwete naye anahubiri kumwaga damu nani kamwambia kunamgombea anataka kumwaga damu? wamekosa sela, ahadi zimewaishia wameanza vitisho, walianza na redet, wamekuja navitisho vya kumwaga damu, wamekuja synovete sijui leo watakuja na nini? kampeni chafu zimeanza huku wao wakihimiza ustaarabu.
Tuamkeni zimebaki siku chache sana, chadema nunueni air time kwenye radio na tv. wanataka chadema waache kuhubiri sera zao ili muanza kujibu tuhuma kuweni makini. by the way where is Mpendazoe, afanye kampeni hata kwenye madaladala asubuhi panda basishuka kituo cha pili panda lingine hivyo hivyo. kampeni si lele mama.