Machozi hayaniishii !!!!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Machozi hayaniishii !!!!!!!!!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Allah's Slave, Jul 17, 2012.

 1. Allah's Slave

  Allah's Slave JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]Asalam Alaykum Waungwana, Naombeni mnisaidie mawazo yenu ili niweze kumrudisha mke wangu aliyeondoka nyumbani yapata mwezi sasa. Tumejaliwa watoto wa wili na ndoa yetu ina miaka 6 sasa.[/FONT] [FONT=&quot] Tulikorofishana nyumbani akaondoka. Mke alikuwa mama wa nyumbani hivo sina hata house girl. Kupika sijui so nawalisha hoteli na junk food wakati wote. Kuwatayarisha waende shule asubui naona kazi nadhani na leo hawatoenda shule. Nahangaika bila mama yao na nimeshajaribu kumfuata kuongea naye imeshindikana. Ramadhani ndo imeshafika hivyo sijui nitafturu wapi. Nimemkumbuka sanaaaaaaa Mke wangu.
  [/FONT]
   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,674
  Trophy Points: 280
  Mh!Umetaja kazi tu hapo,inaonekana unamtazama mkeo kama mashine ya kukufanyia kazi na sio mke,ndo maana unamkumbuka kwaajili ya kazi na sio mapenzi na upendo.Hata kwenye kufunga umemkumb kwenye kukupikia futari. . . .
   
 3. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Oa mwingine kabla ya mwezi Ramadhani but hakikisha awe na huruma ya kutunza wanao. Ikishindikana huyo uliyempata kujari wanao, tafuta mwingine haraka kabla ya Holy month kuanza. Pole!
   
 4. jamiif

  jamiif JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 2,417
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  mh, mbona unaonekana ni mbinafsi sana wewe, kwa sababu unaweka interests zako mbele tu mbona huongelei kuhusu furaha ya mkeo utairudishaje?....umesema hata housegirl huna sasa ina maana angekuwepo basi usingekuwa na shida tena na mkeo, mara ramadhani inakuja utafuturu wapi, oh, watoto hawaendi shule, nk...kaka jiangalie muenendo wako na ujiulize kwa nini mkeo ameondoka isijekuwa ni wewe mwenyewe ndiye uliyesababisha akaondoka...huo ugomvi wenu sisi hatuujui wala hatuna haja ya kuujua, muhimu ni ukae chini jifikirie na ujiangalie umekosea wapi kisha fuata moyo wako....
   
 5. jamiif

  jamiif JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 2,417
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  nikweli kabisa jamaa ana ubinafsi sana..nakuunga mkono mkuu! ajiangalie na kuchunguza nafsi yake kwanza...
   
 6. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wacha kumbembeleza akiukumbuka atarudi mwenyewe, na kama ulikuwa unamkosea shauri lako wengine watampatia tu.

  Mwanaume lazima ajifunze kuvumilia na ajue anapo owa lazima awe anajua ndoa sio lele mama sio kila siku kugombana na mke wake.

  Mwanaume anapo owa lazima awe ana uhakika ugomvi ni suna wasio gombana ndani ya nyumba lazima wana matatizo ya kiakili na lazima wakapimwe, lakini ugomvi usifikie kutukanana na kuvunjiana heshima mpaa mna cross mipaka.


  FYI mimi nikiona sijagombana na wife lazima nimtafutie kaugomvi yani nimuone kisha hamaki ndo naona raha lakini hatujawahi kufikia hatua ya kutukanana kama wanavyo fanya watu wengine.

  Yallah wacha tukuombee dua ili mke wako arudi.

  DUA

  Ya rabi mjalie huyu kiumbe busara ajue nini mana ya mke na mjalie mke wake arudi nyumbani kwake kabla ya ramadhani.

  Mwenyezi mungu mjalie huyu kiumbe imani ya kumpenda mke wake na mjalie mke wake imani ya kumpenda mme wake na watoto zake, na mjalie siku ya leo imani ya kuwakumbuka watoto wake alio zao.

  Ya Allah bila yako wasinge owana na bila yako hawatarudiana wajalie viumbe hawa warudiane na wapendane kuliko mwanzo////Ameen.
   
 7. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Pole, Jaribu kuhusisha ndg zake wa karibu pamoja na wazazi wenu labda anaweza kubadilika. Hapo kwenye bold inamaanisha umemkumbuka sana kwa sababu Ramadhan imefika??? Napata mashaka kidogo!
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  Unataka tukusaidiaje kumrudisha mkeo?
  Chanzo cha kuondoka ni nini?
  Unataka kumrudia kwa kuwa umeshindwa malezi
  au kwa kuwa unampenda mkeo?
  Na unadhani kwa attitude uliyoonyeshz hapa mkeo ana hamu ya kurudi?

  Hivi unajua mama wa nyumbani anavyochoka? Unajua kazi za nyumbani zinavyochosha? Unamsaidia hata kidogo(ooophsss sorry ungekuwa unamsaidia usingelalamika hapa loh)?

  Kiufupi mkuu mjali mkeo...
  Mpende mkeo...
  Mdhamini mkeo....
  Mke sio machine ya kazi....
  Muappreciate mkeo....


   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  ila wanasema tembo hashindwi kubeba mkonga wake, inakuwaje tena mkuu? Mbona unashindwa?
  Yaani huwezi kupikia wanao?
  Huwezi kuamka saa kumi na moja kuwaandaa wanao?
  Loh....
   
 10. L

  Luluka JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ha ha ha!we umeua bendi!!
   
 11. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  It is next to impossible not to love u!
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,674
  Trophy Points: 280
  I was born to make u happy,remmember?
   
 13. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Hiyo ni adhabu tosha juu yako, sasa nadhani utaona thamani ya mke wako, usikate tamaa jaribu tena kwenda kuongea nae atarudisha moyo kwako tuu.
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,834
  Trophy Points: 280
  Hacha mfumo dume wewe, mkeo kakimbizwa na kazi pia, sitoshangaa wewe kuficha kwamba ulimpiga!

  Umelelewa vibaya ata kupika ugali ujui!
   
 15. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mi ndio amenichosha hapo. kazi mwanzo mwisho. mke anakumbukwa kwenye shida tu.
   
 16. next

  next JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 601
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  hahaha, ili hii kauli badi ipo, niliitumia shule back in the 90‘s nilikoma mbona
   
 17. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sababu za kuondoka ni nini? embu jitazame mwenyewe ulivoandika ni kama mkeo alikuwa mashine ya kazi hakuna sehemu umeonyesha una penzi kwake zaidi ya kukulea watoto....Binadamu watu wa ajabu sana waeza kuta ulimuonyesha dharau zote kwamba si chochote wala lolote leo hayupo unaiona thamani yake.
   
 18. Nambe

  Nambe JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 1,455
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Duh nawaonea huruma hao wana kwa kula hotelin daily, kaka wanawake wanapnda kujaliwa, kupendwa kutunza na kuwa appreciated. kaka humjali mkeo na hii ni kutokana na uliyoyaandika hapo juu, huyu mama mpaka kaamua kuondoka na kuwaacha watoto naamin amechoshwa kweli kweli, cha msingi ni ww kuangalia ulipokosea jirekebishe onga na mkeo na umuombe msamaha na kuahd kubadilika, jarb hata kuwatumia ndugu, ila ndio uharakishe kabla hawajamuwah wanaojua thaman ya mwanamke. Pole sana naamn umejifunza kutokana na makosa yako
   
 19. Haven

  Haven Senior Member

  #19
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bora umemsome...nakupa like 101!!, yaani watu wengine unashindwa hata kuwashangaa!
   
 20. magdarena

  magdarena Member

  #20
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  pole sana. kitu chochote ukiwa nacho huwezi kujua umuhimu wake. ukikikosa ndio unajua umuhimu wake. wewe sasa ndio unaona umuhimu wamkeo???????????????
   
Loading...