Macho yanacheka..Moyo unalia

Tetra

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
1,520
764
::
Nilimpenda kwa dhati
Alipojua akanidharau
Nikavumilia kwa haki
Lakini haikuw jibuu
Nikamwacha kwa utii
Nikakimbia maumivu
Macho yanacheka,
Moyo unalia.
::
Ilikuwa wiki iliyopita,
Ktk safari za maisha,
Nikakutana nae ghafla
Kadhoofu ktk afya
Uzuri wake umepotea
Machozi kanililia,
Kasema alidanganywa
Mwanajeshi akapata
Na akaahadiwa ndoa
Akaanza nitenga mie,
Sasa anajuta sana
Akaachwa kwa kashfa
Macho yanacheka,
Moyo unalia.
::
Sikumjibu chochote
Nikaamua kuondoka
Kweli nilimpenda
Mengi tuliyapanga
Magumu tuliyapitia
Akabadilika ghafla
Nikatoa chozi kumlilia
Akakataa tukaachana
Leo tena ananitaka
Moyoni nilishamfuta
Macho yanacheka,
Moyo unalia.
::
Kosa langu ni lipi?
Kuwa wa kwanza kumuacha?
Au kutosamehe tena?
Kusamehe nilisamehe kwani lazima turudiane?
Jamani wana JF nisaidieni maana mie
Macho yanacheka,
Moyo unalia.
=
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom