singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
MACHO na masikio ya wananchi yameelekezwa leo bungeni kusikia jinsi Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu inavyowasilisha makadirio ya bajeti.
Sambamba na hilo, pia hati nyingine itakayowasilishwa bungeni leo ni Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2014/15 , ambapo serikali itatakiwa kutoa majibu ya hoja mbalimbali za ukaguzi huo.
Bajeti hiyo inawasilishwa na Waziri Jenista Mhagama ikiwa ni wizara ya kwanza kati ya wizara 18 za Serikali ya Awamu ya Tano ambayo wabunge watajadili kwa siku tatu. Wizara ya hiyo inayoshughulika na masuala nyeti ya kijamii kama vile wabunge, vijana, kazi na ajira, inategemewa kuwasilisha bajeti itakayoonesha mpango wa kuboresha programu za kukuza fursa mbalimbali za makundi yaliyo kwenye wizara hiyo.
Hivi karibuni, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alimkabidhi Rais John Magufuli Sh bilioni 6, fedha ambazo Bunge lilisema zimetokana na wao kujibana na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
Hata hivyo vyombo vya habari mbalimbali juzi na jana viliripoti baadhi ya wabunge wa bunge hilo wakilalamika kutolipwa mishahara yao ya miezi kadhaa ya ubunge wao katika Bunge lililopita na kohoji iweje Bunge liseme wana fedha ambazo wameona hazina matumizi ya maana.
Hilo pamoja na mengine ni baadhi ya mambo ambayo leo katika bajeti ya wizara inayopendekezwa yanayoweza kuibuka katika mjadala wakati wa uchangiaji hotuba ya wizara hiyo.