Machinga wathibitiwe maana wenye maduka tunashindwa kulipa kodi

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,956
1,114
Rais JPM aliruhusu wamachinga yaani biashara ndogo ndogo za mboga, matunda na nafaka na mitumba inaweza kufanyika pembezoni mwa barabara za mijini. Lakini hapa Arusha hao machinga sasa wameingilia biashara za maduka ambazo zinakatiwa leseni na kulipiwa kodi ya mapato.

Wanauza sukari, mafuta ya kupikia, sabuni na hata nguo mpya. Sisi wenye maduka tumelalamika lkn Viongozi wa halmadhauri ya jiji wanaogopa kuwakamata eti kwa kuwa ni agizo la Rais. Tunaomba Mkuu wa Mkoa Mhe Mrisho Gambo utatue tatizo hili kwani tutashindwa kulipa kodi na benki na saccos zitatufilisi kwani hatufanyi mauzo.

TFDA na maafisa afya pia wanaruhusuje sukari na mafuta ya kupikia kuuzwa maeneo yenye uchafu?
 
Na bado. Baki ukimsubiri mkuu wa mkoa mpaka ufilisiwe ili ujiue. Kwanini na wewe usihamie mtaani?
 
Wamachinga ndio walimpa kura, ukiwagusa hao ni kama umguse jesca....
Be carefully
 
Back
Top Bottom