Machinga kwa haya wasulubiwe tu

Machinga kwa haya wasulubiwe tu

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,120
Reaction score
24,396
Hawa jamaa walifanya Tanzania tukaambiwa na majaliwa kwamba tuna viwanda elfu 50 kumbe walikua wakihesabu vibanda vya machinga kama viwanda.

Pia hawa wameharibu taswira ya mji: Kila mahali ni mavibanda tu unakuta barabara nzuri, garden poa lakini mavibanda machafumachafu tu

Vibanda vyao havikua na hadhi kwa kweli mfano pale ubungo flyover kulikua na mavibanda machafu machafu halafu mavibanda hayana mpangilio

Machinga walichangia mji kuwa mchafu: Dar ilikua chafu na inaendelea kuwa chafu machinga wamechangia pakubwa maana wakimaliza wanamwaga mwaga makaratasi na mabaki ya vifungashio kila mahali pia hata haja ziliendwa vichakani kila mahali palinuka

Machinga walifanya Dar hewa ikawa chafu na nzito: Kila mahali ni kaboni na joto kali kwasababu ya vibanda kusongamana kila mahali hakuna pa kukosa hewa

Machinga walisababisha ajali na watu kugongwa na vyombo vya usafiri: Inatokea huku ni vibanda kila upande kiasi kwamba wakati unaendesha gari likitokea la kutokea huwezi kukwepa ajali au kumgonga mtu au watu wanakosa pa kupita pembeni mwishoni wanagongwa na magari,bajaji au pikipiki.

Machinga walishusha mapato ya nchi: Walisababisha serikali kukosa kodi na makato hawa hawalipi kodi.

Machinga walifanya biashara rasmi zikafa: wewe una duka lako kubwaa unalipa kodi laki tano TRA kwa mwezi watu wanakuja wanakuwekea vibanda mbele yako huuzi mwisho unakula hasara unarudi nyumbani, hela ulikopa unapata bp unakufa fasta.Biashara nyingi zilifungwa mafrem meupe kwasababu ya hawa viumbe machinga.

Machinga walichangia kuzagaa kwa bidhaa feki na zenye kiwango kidogo: Yaani hawa walifanya vitu feki vikatamalaki mtaani na vitu vyenye ubora mdogo.

Mwisho machinga walituletea yule mtu:Hili ndo kosa kubwa kabisa. Yaani machinga nyie October ya 2020 sitowasahau aisee maana nyie mlikua mnamsifia na kumlinda yule mtu sana, na nyie ndo mmechangia pakubwa kutuletea yule mtu wenu wa chato sasa wacheni dawa iwaingie mliowaona wapinzani ni maadui mkaona mumpe yule mtu kwa mbwembwe zote malipo ni hapa hapa.

My take: Hakuna wa kuwatetea,na hayupo na hatokuwepo, kwa hizo hoja hapo mnastahili msulubiwe kwa sheria za nchi, mpelekwe maeneo maalum tena mlipishwe kodi sawa na wenye maduka ili akili iwakae sawa siku nyingine mjue kutumia vyema sanduku la kura.

Mwisho: Imeandikwa kuwa kila mtu atavuna alichopanda. Sasa mnavuna mlichopanda

WASULUBIWE TU

Tujikumbushe

October 26,2020
IKIWA imebaki siku moja Uchaguzi Mkuu ufanyike, Jumuiya ya wafanyabiashara ndogondogo ‘machinga’ na madereva pikipiki ‘bodaboda’ nchini, wametoa msimamo wao kuwa watampigia kura mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.

Wamesema hatua hiyo inatokana na mgombea huyo kubeba agenda za Watanzania na makundi yao ikiwamo kuwapatia vitambulisho vya umachinga ambayo ni sababu kuu inayowafanya wao kumpa kura nyingi na za kishindo kesho.

Wakizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam jana, wamesema lao kuelekea Uchaguzi Mkuu tamko lao ambalo limetolewa na wenzao katika mikoa mitano ikiwamo Simiyu, Mwanza, Iringa, Katavi na Mbeya leo ndiyo msimamo wa wafanya biashara wote kwani wamechoka kutumiwa kama amdaraja na kisha kutelekekzwa.

Lengo mahsusi la kuifanya nchi yetu ifanye uchaguzi wa amani na utulivu. Makamu Mwenyekiti Mwenyekiti wa Machinga Taifa, Steven Lusinde serikali ya awamu ya tano imewafanyia mambo makubwa kwa ujumla na wanamuunga mkono Rais Magufuli haya tunayozungumza yameonekana.

“Tumepewa vitambulisho vina faida kubwa kwetu kwenye maeneo ya mjini, tunapata mikopo, bima ya afya nab ado watu wanafanya biashara bila kusumbuliwa.

“Rais ametutoa utumwani kutupeleka nchi ya ahadi na ndani ya miaka mitano tumepata faida kubwa kuliko wakati mwingine. Kwa hiyo sisi wote nchi nzima lengo letu ni moja tu, ashinde hivyo tutajaza kura za kutosha kwenye debe la kura.

“Alituamini bodaboda, machinga na mama lishe, kwanini sisi leo tusimthamini kwa kumpa kura, bado siku moja tu tutamfanyia jambo zuri tutatia tiki tu pale kwa rais, wabunge na madiwani wote wa CCM,” amesema.

Lusinde amesema hawajawahi kuiunga mkono serikali yoyote tangu nchi hii imepata uhuru na kwamba hii ndiyo serikali ya kwanza.

“Wafanyabiashara wanaenda kuwa matajiri na tunaenda na imani kubwa tusikubali kutumika, tumetumika vya kutosha na wanasiasa wanatufanya madaraja wanatupandia kisha wanatutelekeza.

“Lakini Magufuli ametupelekea sehehemu ambayo hatujawahi kuitegemea tangu nchi ipate uhuru. Wamachinga wote tunakwenda na Magufuli, na wafanyabishara wote kuanzia leo tutafute pesa leo na kesho ili kesho kutwa twende tukapige kura na kwenda nyumbani kula pilau kusubiri rais aapishwe,” amesema.

Kwa upande wake Mweka Hazina wa bodaboda jijini Dar es Salaam, Saidi Chenja amesema wajasiariamali wakiwamo waendesha bodaboda na bajaj lazima wahubiri amani kwani ndiyo tunu ya taifa ambapo Oktoba 28 lazima wafanye maamuzi sahihi.

“Viongozi wa upinzani wamezoea kutupandia sisi kama majukwaa wanatutumia kisasa kisha wanatuelekeza, sasa tumeamua jambo moja, ni bora ule ugali maharage kwa furaha kuliko biriani kuku kwenye machozi.

“Bodaboda ulikuwa nzuio la kuingia mjini tangu sasa tunaingia mjini bila bughudha. Tulikuwa tunaonekana tuna vurugu lakini niwahakikishie Watanzania hakuna atakayevunja amani iwe Dar es Salaam au mkoa mwingine wote tutakwenda kupiga kura,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema wameshuhudia kazi imefanyika ndani ya miaka mitano na kusisitiza waendelee kumchagua Magufuli kwani ni kingozi mzuri ili aendelee kuwatendea mazuri.

“Kiongozi mzuri lazima apate upinzani.
Ametuteteta wanyonge bodaboda, machinga na mama lishe Oktoba 28 tusifanye masikhara ili atakeyesema kura zake zimeibwa aone Magufuli anaongoza kuanzia asilimia 90. Tusifanye makosa, rais anataka mafiga matatu ili akitaka kutoa mikopo kwetu kusiwe na vikwazo ndiyo maana tunataka kumpelekea mafiga matatu,” amesema.

Naye mfanyabiashara Saidi Mrisho, amesema kitambulisho cha wamachinga kwa mara ya kwanza wamekipata baada ya kuhangaika sana lakini kwa busara zake Magufuli aliona kwanini zoezi hilo linasuasua akawapatia.

“Kitambulisho hiki kimetusaidia kupata mikopo, Magufuli katuondolea adha ile ya kukimbizwa kimbizwa mitaani tukifanya biashara leo hiii tusingekuwepo lakini pia nina bima ya afya hii haijawahi kutokea tangu uhuru.

“Tunapata mikopo CRDB na NMB, yaani ni nafasi yako hakuna hati ya nyumba wala kiwanja. Jukumu letu ni kumfurahisha yule eliyetuweka sisi tuwe juu. Hakuna chinga aliyekuwa anakipenda chama chochote isipokuwa yeye ametufanya tuipende CCM, tumeanza pamoja na tutamaliza pamoja.

Mjumbe wa Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Chengula amesema Serikali ya awamu ya tano inatofautiana sana na awamu zilizopita kwani kafanya makubwa sana hususani kwa bodaboda pale aliporidhia kutambua boda kuwa usafiri rasmi kisheria.

“Nasiki kuna miaka mitano tena na miaka mitano kwanza, hakuna sababu ya mitano kuipeleka sehemu nyingine zaidi ya CCM.

“Hakuna asiyemfahamu Farao aliwaua watoto wa kiume lakini Mungu alimvumilia Musa akakua. Lakini tukizungumia Sodoma na Gomora Mungu hakuvumilia, huyu mgombea wa miaka mitano kwanza anatuletea mambo ambayo katiba yetu hairuhusu.

“Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mawasiliano siyo mahusiano, nchi yetu hairuhusu mambo hayo,” amesema.
 
Waliitwa wanyonge wakakubali Sasa serikali ile ile ya wanyonge ndo inayo washughulikia wanyonge machinga licha ya kupewa vitambulisho
 
Hawa jamaa walifanya Tanzania tukaambiwa na majaliwa kwamba tuna viwanda elfu 50 kumbe walikua wakihesabu vibanda vya machinga kama viwanda.

Pia hawa wameharibu taswira ya mji: kila mahali ni mavibanda tu unakuta barabara nzuri, garden poa lakini mavibanda machafumachafu tu.
Maana ya malipo ni hapahapa imetimia🤸.
 
WAKATI UMEFIKA SASA KWA SERIKALI KUJA NA PERMANENT SOLUTION KUHUSU WAMACHINGA!

ova

1.anzisha sera nzuri ya mikopo nafuu ya kilimo na urejeshwaji uratibiwe vizuri na kuwaelekeza vijana mazao yanayoweza kumpatia pesa ya chapchap kwa mfano wafundishwe kilimo cha soya waelezwe Songea ardhi ilipo ili wakalime soya ambayo ni zao linalohitajika China kwa sasa kwa kiwango kikubwa na linapandwa mwezi wa 11 mwezi wa pili watu wanavuna na kuanza kula pesa.
 
2.vijana wasomeshwe elimu mbalimbali za stadi za kiubunifu na maisha kwa mfano utengenezaji wa mkaa kwa kutumia taka ngumu, utrngenezaji wa pavement kwa kutumia matairi used na plastiki na wawezeshwe kupata mashine za uzalishaji halafu watalipa kidogokidogo
 
3. Machinga wa Tanzania wajiunge kundi la watu hata watatu halafu wanachukua frem wanauza bidhaa zao hapo huku TRA ikikusanya makadirio yao kwa pamoja tena kiwango kiwe nafuu, sasa kwa Tanzania sidhani kama wataweza maana uaminifu kwa Mtanzania ni msamiati mgumu tofauti na Waganda wao hata wanne hukaa frem moja na kazi wanapiga bila kinyongo iwe wanauza bidhaa za kufanana au bidhaa tofauti.
 
1.anzisha sera nzuri ya mikopo nafuu ya kilimo na urejeshwaji uratibiwe vizuri na kuwaelekeza vijana mazao yanayoweza kumpatia pesa ya chapchap kwa mfano wafundishwe kilimo cha soya waelezwe Songea ardhi ilipo ili wakalime soya ambayo ni zao linalohitajika China kwa sasa kwa kiwango kikubwa na linapandwa mwezi wa 11 mwezi wa pili watu wanavuna na kuanza kula pesa.
Kweli kabisa siku zote naamini kilimo

Ndiyo itapunguza umachinga

Serikali ingewekeza nguvu huko,kuanda miundombinu nk ya kilimo watu,vijana wengi
Wangejikita huko

Ila sahv ukihoji hivyo utaambiwa kwani wamekatazwa kulima??

Ova
 
Kweli kabisa siku zote naamini kilimo

Ndiyo itapunguza umachinga

Serikali ingewekeza nguvu huko,kuanda miundombinu nk ya kilimo watu,vijana wengi
Wangejikita huko

Ila sahv ukihoji hivyo utaambiwa kwani wamekatazwa kulima??

Ova

Kilimo serikali inategemea mvua ni kosa kilimo cha pesa ni umwagiliaji, then masoko huko bado kuna future ya kueleweka lakini tofauti na hapo tutakua taifa la wachuuzi tu ambao hatuna dira kiuchumi
 
Back
Top Bottom