Machawa wa Simba ndio sababu ya kuwapa viburi viongozi wa Simba

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,298
3,971
Hawa machawa wanaotaka watu waende uwanjani wakaaibishwe tena,ndio wanawapa kiburi viongozi.

Hawa viongozi wanashindwa kusajili na kufanya usajili wa kisiasa huku wakiungwa mkono na machawa na waandishi uchwara wanaolipwa kuwasifu viongozi.

Timu kwa sasa haina coach.Matola hana uwezo hata kidogo. Timu aliiweza Mgunda. Leo wanatafuta ili mradi awe mzungu na utapeli mwingi mwingi mara huyo kocha kapita wolves U17.

Uhuni kama huo unaungwa mkono na machawa.Inasikitisha

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Machawa maarufu wa kutetea viongozi wa Simba kina kisugu, mwakitalima, mzaramo ndio wako mstari wa mbele wanajua mkono ushaenda kinywani🤣🤣
 
Ukweli mchungu pia ni kwamba Simba inasajili kwa influence ya machawa.

Hawa watu wanaolipwa kufanya propaganda za kutetea viongozi licha ya viongozi kufanya sajili za kisiasa,sio watu wazuri kwa afya ya club.

Wao wanaangalia maslahi yao tu kwenye ushabiki wao

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Itafika kipindi Viongozi hawataweza kujificha. Ngoja washindwe kuingia robo fainali sijui watajitetea Nini. Viongozi wanawaza kupiga pesa tu basi. Angalia MO anachofanya kwenye jezi na halipi hata Senti, kwanini wasingetafuta mdhamini Kama Yanga?
 
Machawa maarufu wa kutetea viongozi wa Simba kina kisugu, mwakitalima, mzaramo ndio wako mstari wa mbele wanajua mkono ushaenda kinywani🤣🤣
Umemsahau na Aggysimba. Siku ambayo wanasimba watashtuka huo upuuzi wa viongozi kuwalipa machawa ili watetee hata kama wakifanya mambo ya hovyo na wengine wamefika mbali mpaka kuandaa "press" basi wakati huo Yanga itakuwa mbali sana. Wakati Yanga inaachana na machawa na kuanza kuendesha timu yao kitaalamu Simba inaingiza siasa na machawa matokeo yake wamekula tano na mpaka sasa hivi takribani wiki ya tatu hawajui tatizo ni nini na wasipozinduka basi wajiandae kwa matokeo mabaya kwenye michezo ijayo.

Kiongozi mzuri anaonekana wakati wa matatizo na mkwamo lakini viongozi wa Simba wakati timu imekula tano wao wakapotea mazima wakawaachia timu machawa ndio wakawa watoa taarifa. Ubaya wa chawa anakusifia tu hata kama kuna shida hakwambii ukweli ili asikose mkate wake wa kila siku.

Yoyote aliye karibu na viongozi wa bodi ya Simba awasanue ili hao machawa wapigwe marufuku kutoa taarifa za Simba na wajue mipaka yao. Ilivyo sasa haijulikani nani mtoa taarifa za Simba, ipi "press" ya Simba kama klabu ipi press binafsi ya Kisugu. Simba imekuwa kama pombe ya ngomani. Na vilevile ni wakati sasa wa matawi ya Simba kurudishiwa nguvu kama ilivyokuwa zamani tofauti na sasa ambapo hawa machawa ambao wameujua mpira juzi kujifanya wao ndio washauri wa kila kitu hata vitu vya kitaalamu kama usajili, benchi la ufundi, n.k.

Ni mtizamo tu.
 
Machawa wamejaa Sana Simba sababu ya mfumo mbovu, Hawa hawapo kwa ajili ya Simba bali kwa maslahi yao binafsi.
Nakupenda Simba toka moyoni Ila afadhali tufungwe ili wanachama wazinduke.
 
Ni upumbavu kususia timu kwani. Kama vipi hamieni upande wa pili,hakuna timu isiyofungwa,Yanga walisota miaka 4 lakini hawakupanic kiasi hiki na hapa ndiyo mnawapa nafasi Utopolo kuwakejeli kila siku mayowe haisaidii kitu.
 
Back
Top Bottom