Mtu mjinga anaweza kuropoka jambo lolote na watu tutakupuuza tu.
Sijajua Moses Machali amesema hayo akisimamia Facts zipi?
Mkutano ulikuwa wa CHADEMA na bomu limelipuliwa na risasi zilipigwa kuwalenga viongozi na wafuasi wa Chadema, waliokufa ni kiongozi na wafuasi wa CHADEMA, watu wote waliojeruhiwa walikuwa ni viongozi na wafuasi wa CHADEMA. Sasa mtu anakuja kuropoka eti huenda wahusika wa tukio hilo ni CHADEMA!!!
Uwendawazimu sio lazima uokote makopo, hata kuropoka uchafu ni uendawazimu tu.
Kama HATUMII POWDER kwa nini hajasema JESHI LA POLISI NA USALAMA WA TAIFA VIFUTWE KWA KUSHINDWA KULINDA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO?? Ni kwa sababu nina uhakika hao wote walikuwepo pale!!!