Wanachokifanya NCCR Mageuzi ni upuuzi mtupu, niliwafuatilia vizuri akina machali star tv lakini nikagundua migogoro yote ni sababu ya chuki binafsi, na tamaa ya madaraka.Kama kweli kafulila aliwaomba msamaha kama vimemo vyao vinavyoonyesha walishindwa nini kumsamehe mbona hata Mungu anatusamehe.Walichokifanya kinawaua kisiasa wenyewe 100%.Mimi kama mtanzania halisi sipendelei vyama vyenye migogoro.Pia kama mliombana msamaha hiyo ni siri yenu na chama chenu si vyema kuja kutuonyesha mambo yenu ya ndani.Ukimuacha mke au Mme si busara kuanika udhaifu wake wa ndani mpaka mlivyoombana msamaha hadharani, kwa kufanya hivyo nadhani hata wewe mhusika utakuwa na matatizo makubwa kifikra na kimawazo.