Machafuko yanayoendelea Sudan yailaumu Israel

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Mtu mwingine auawa katika ghasia Sudan, Khartoum yasema Israel inachochea machafuko
Mkuu wa taasisi ya upelelezi ya Sudan amesema kuwa waasi wenye uhusiano na utawala haramu wa Israel ndio wanaochochea maandamano yanayoendelea kwa siku kadhaa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ambayo yamesababisha kifo cha mtu mmoja jana baada ya mauaji ya waandamanaji wengine wasiopungua 8 siku kadhaa zilizopita.
Salah Abdallah Gosh amesema mtandao wenye makao yake katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi ambao una uhusiano na Israel umeingiza mamia ya waasi nchini Sudan kwa shabaha ya kuchochea machafuko nchini humo.
Mkuu wa vyombo vya upelelezi vya Sudan amesema kuwa vyombo vya usalama vimewatia nguvuni watu kadhaa ambao ni sehemu ya wafuasi 280 wa kundi la waasi la Abdul Wahid Mohamed Nur walioingizwa Sudan kupitia Nairobi.
Gosh ameongeza kuwa watu hao wameajiriwa na shirika la ujasusi la Israel, Mossad na wamefungua ofisi za kuendeshea operesheni zao katika miji ya Kharoutm na Omdurman. Ameongeza kuwa vyombo vya usalama pia vimewatia nguvuni watu kadhaa waliohusika na machafuko ya siku kadhaa zilizopita katika mji wa Atbara.
Vyuo vikuu na taasisi za elimu zimefungwa nchini Sudan na serikali imetangaza hali ya hatari katika miji kadhaa ya nchi hiyo kutokana na maandamano yanayoendelea kupinga hali mbaya ya uchumi na ughali wa bidhaa.
Waandamanaji hao pia wamechoma moto majengo ya serikali na vituo vya chama tawala cha Kongresi ya Taifa.
Waandamanaji hao ambao wanalalamikia kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu kama mkate na hali mbaya ya uchumi wanataka kuondolewa madarakani serikali ya Sudan.
 
kwa kwel mm huwa najiuliza sana kuhusiana na hili swala la baadhi ya nchi za afrika tena ukifatilia kiundan n sehemu ambazo zina malighari muhim (kama sio mafuta bas n madin).
Sasa je hiv n kwel hawa watu weupe wanatumia hii njia kuendelea kuinuonya afrika?
 
Asante kwa taarifa.ila hao wasudani ni mapang'ang'a kama walivyo Arabs wa middle east and Co.
 
Kinachoshangaza watu wengi wanaofuatilia siasa za nje, nchi nyingi za kiarabu huwa na hali nzuri kiuchumi wakiwa wamewekewa vikwazo vya kiuchumi. Lakini huwa na hali mbaya na migogoro pale vikwazo vya kiuchumi vikiondolewa.
Hii pia imewahi kutokea Iran.
 
Mtu mwingine auawa katika ghasia Sudan, Khartoum yasema Israel inachochea machafuko
Mkuu wa taasisi ya upelelezi ya Sudan amesema kuwa waasi wenye uhusiano na utawala haramu wa Israel ndio wanaochochea maandamano yanayoendelea kwa siku kadhaa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ambayo yamesababisha kifo cha mtu mmoja jana baada ya mauaji ya waandamanaji wengine wasiopungua 8 siku kadhaa zilizopita.
Salah Abdallah Gosh amesema mtandao wenye makao yake katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi ambao una uhusiano na Israel umeingiza mamia ya waasi nchini Sudan kwa shabaha ya kuchochea machafuko nchini humo.
Mkuu wa vyombo vya upelelezi vya Sudan amesema kuwa vyombo vya usalama vimewatia nguvuni watu kadhaa ambao ni sehemu ya wafuasi 280 wa kundi la waasi la Abdul Wahid Mohamed Nur walioingizwa Sudan kupitia Nairobi.
Gosh ameongeza kuwa watu hao wameajiriwa na shirika la ujasusi la Israel, Mossad na wamefungua ofisi za kuendeshea operesheni zao katika miji ya Kharoutm na Omdurman. Ameongeza kuwa vyombo vya usalama pia vimewatia nguvuni watu kadhaa waliohusika na machafuko ya siku kadhaa zilizopita katika mji wa Atbara.
Vyuo vikuu na taasisi za elimu zimefungwa nchini Sudan na serikali imetangaza hali ya hatari katika miji kadhaa ya nchi hiyo kutokana na maandamano yanayoendelea kupinga hali mbaya ya uchumi na ughali wa bidhaa.
Waandamanaji hao pia wamechoma moto majengo ya serikali na vituo vya chama tawala cha Kongresi ya Taifa.
Waandamanaji hao ambao wanalalamikia kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu kama mkate na hali mbaya ya uchumi wanataka kuondolewa madarakani serikali ya Sudan.

Hio ni kisiasa tu, lazima apatikane wa kumlaumu, Hata Marekani wanaisingizia Urusi kuingilia uchaguzi wake, Uingereza pia wanaisakama Urusi kwa Mambo yao kwenda mrama. Lazima mbuzi wa kafara apatikane mkuu....
 
kwa kwel mm huwa najiuliza sana kuhusiana na hili swala la baadhi ya nchi za afrika tena ukifatilia kiundan n sehemu ambazo zina malighari muhim (kama sio mafuta bas n madin).
Sasa je hiv n kwel hawa watu weupe wanatumia hii njia kuendelea kuinuonya afrika?
Hii ni tabia ya wanasiasa kulaumu serikali za nje na imeshazoeleka. Utaskia Israel ndiyo wanachochea wananchi kuandamana.

Wakati huo huo uhalisia hamna maji, bei ya vyakula imepanda na mafuta nayo yamepanda.

Na tatizo hili anayo hadi mmarekani...utskia Urusi hivi na hivi.

Ila Bashir mbabe saana hata waandamane sidhani kama ataondoka. Kama alishindwa kuondoka 2005..2015
 
Waarabu wana mambo sana
Screenshot_2018-12-23-11-48-43.jpeg
 
kwa kwel mm huwa najiuliza sana kuhusiana na hili swala la baadhi ya nchi za afrika tena ukifatilia kiundan n sehemu ambazo zina malighari muhim (kama sio mafuta bas n madin).
Sasa je hiv n kwel hawa watu weupe wanatumia hii njia kuendelea kuinuonya afrika?
Ushafika sudan?
 
Hio ni kisiasa tu, lazima apatikane wa kumlaumu, Hata Marekani wanaisingizia Urusi kuingilia uchaguzi wake, Uingereza pia wanaisakama Urusi kwa Mambo yao kwenda mrama. Lazima mbuzi wa kafara apatikane mkuu....
Hata urusi wali isingizia marekani umoja wa kisovieti ulipo vunjika.
 
Back
Top Bottom