mfalmeselemani
Member
- Sep 30, 2014
- 95
- 47
WAANDISHI wa habari wametakiwa kusimamia haki na ueledi na wasikubali kutumiwa na wafanyabiashara matapeli wanaokesha usiku na mchana kubuni mbinu za kuwalaghai wananchi.
Balenga alitoa kauli hiyo, jana wakati akivishukuru vyombo mbalimbali vya habari nchini, vinavyoendelea kuripoti habari zake zinazohusiana na kesi ya kughushi aliyomfungulia mfanyabiashara maarufu, Hans Aingaya Macha.
Alisema anawashukuru watu wote waliomsaidia pamoja na waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele licha ya kuwepo kwa juhudi kubwa ya kuhakikisha habari za ukweli zenye mlengo wa kueleza tukio halisi zinazuiliwa kutoka.
"Nimepitia mengi, ila nanyi vumbueni na wasaidieni wengine, maisha ya dunia ni mapito, msikubali kutumiwa na watu wachache kwa ajili ya kupoteza haki za watu kwa kuwa haramu haiwezi kuwa halali kamwe,"alisema. Balenga alisema ameamua kutoa shukrani zake na nasaha kwa waandishi wa habari kutokana na kuwepo kwa nguvu ya pesa, inayohakikisha stori za ukweli kuhusiana na tukio hilo hazitoki.
Hivyo, alisema kwa sasa anasubiri uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi yake aliyoifungua ya kugushiwa hati na Macha kwa kuwa anaamini ukweli utajulikana na wasitishwe na watu wanaodai ni wake zangu hivi sasa.