Joel kaigarula
Member
- Jun 3, 2014
- 28
- 16
Lengo la tweet hii toka kwa mkurugenzi mtendaji (CEO) wa kampuni ya Apple lilikuwa ni kuonyesha jinsi kampuni inavyotekeleza sera yake ya kurudisha uzalishaji wa bidhaa zake nchini Marekani badala ya kutumia viwanda vya nchini China. Lakini badala yake tweet hii imezua mjadala ambao haukutarajiwa. Kompyuta za Mac pro ambazo zinaonekana kwenye picha hiyo zinaonekana wazi kuwa zinatumia operating system ya windows, mpinzani wa kampuni ya Apple.
Ni karibu wiki moja tu imepita tangu mkurugenzi huyu huyu wa Apple, kurusha vijembe (ambavyo havikuwa sahihi) kwa Microsoft, kwa kudai kuwa win 8 ina mauzo hafifu kulinganisha na Operating system ya Apple, OS X. Lakini hapa tweet yake mwenyewe inaonyesha kuwa kumbe katika kutengeneza kompyuta za Apple unahitaji windows!
let the fan boys war begin! 🙂
imetoka: Bofyatz.com:: Tanzanian tech blog