Mabunge huwa na siri ambazo hazitangazwi wala kuwekwa kwenye Hansard

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
52,003
Bunge la kwanza la marekani lilipofanyika mara walipopata uhuru kulikuwa na Agenda moja kuu ambayo walijifungia nayo ndani na hawakuweka kwenye Hansard.Agenda hiyo ilikuwa walijiuliza hivi Kwa nini Wamarekani TULITAWALIWA ?

Wakachambua hiyo hoja wakaishia kusema kuwa walitawaliwa kwa kuwa walikuwa ni Wajinga.Kwamba kama wasingekuwa wajinga wasingetawaliwa.Wakajiadiliana kuwa ili wasitawaliwe wafanyaje? Wakakubaliana kuwa inabidi wabadilishe DNA.Sababu inaonyesha wazi kwamba kizazi kilichokuwepo wakati huo Marekani kilikuwa cha Wajinga ndio maana wakatawaliwa.

Wakajidiliana watabadilisheni DNA wapate kizazi cha watu wenye akili? Wakaona Dawa ni kuingiza nchini vijana wenye akili sana toka mataifa mbalimbali wahamie marekani.Sababu ya mkakati huu ilikuwa ni kuwawinda wale vijana ambao hawajaoa wala kuolewa wakijua kuwa wakifika wale uwezekano mkubwa wa kuparamia au kuparamiwa na mmarekani ni mkubwa sababu ya ashiki wanazokuwa nazo kwenye huo umri.

Mkakati huo ulisaidia mno kwani kundi la kwanza la vijana wengi wa kiume wa kiyahudi wenye akili za kuua mtu toka mataifa mbali mbali ikiwemo ujerumani,Israel n.k waliwasili Marekani na wote waliishia kuoa Wanawake wa Marekani na kuwa raia.Matokeo ya kizazi cha baadaye cha hao vijana ni Pamoja na yule aliyegundua bomu la atomic mmarekani J. Robert Oppenheimer,Watu kama akina Henry KISSINGER na wengine wengi.

Marekani tokea wakati huo ikawa na sera yao iliyojificha na wengi tuainjua kama BRAIN DRAIN ambayo kazi yake ni kuwinda watu wenye akili mno hasa vijana na kuwapa uraia marekani kwa kuwarubuni kwa maslahi makubwa nk.Ndio maana ukiitizama Marekani kwa sasa ni nchi ya mataifa mengi.Ni nchi ambayo raia wenye akili kutoka duniani kote wanapatikana marekani.Madaktari wazuri wako marekani wakiwemo watanzania,Maprofesa wazuri wako marekani wakiwemo watanzania nk

Mambo yale yaliyoamuriwa na bunge kwenye vikao vya siri yanafanya kazi hadi leo

Ukienda India waliisoma Tanzania wakaona haina wataalamu wa kutengeneza vito vya thamani vya madini ya Tanzanite.Bunge lao wakakaa kimya kimya wakapitisha na kuufanya mji wa Jaipur India kuwa wa viwanda vya kutengeneza vito vitokanavyo na Tanzanite.Na wanapata pesa nyingi kuliko Tanzania kwa biashara hiyo na sekta hiyo inaajiri zaidi ya wahidi elfu kumi na tano.

Wabunge wetu wanapobwata eti waonyeshwe live sura zao!!! Nawashangaa.Waangalie mabunge kama hayo ya wenzao kuna mengine walijifungia ndani wakajadili kimya kimya wakatoka kimya huoni hata kwenye Hansard.Lakini kitu walichotoka nacho ni cha uhakika kilichoenda shule na kinachosaidia nchi kwa miaka nenda rudi.Wananchi wangependa kuona matokeo

Nashukuru Nape MBUNGE NA WAZIRI MWENYE AKILI KULIONA HILO NA Kusema Si lazima liwe linarushwa bunge Live.wabunge wafike mahali waondoe utoto wajue bunge ni chombo nyeti chenye mambo nyeti mengi ambayo si yote mwananchi anatakiwa ajue wala nchi zingine wajue kwani hata hizo nchi zinazojifanya ziko transparent ni waongo wakubwa kuna vingine huwa hawaniki na wasivyovianika ni vingi kuliko wanavyoanika hadharani.
 
Ulianza vizuri sana lkn umemaliza vibaya kwa sababu ya mahaba Niue uliyo nayo kwa chama chako, ndo yanokufanya uwe kipofu,
 
Ungeonekana muungwana kama ungehitimisha kwa kuzingatia marejeo yako ya mataifa ya Magharibi ila sasa ninadiriki kusema kuwa wewe unafikiria kwa kutumia tumbo badala ya akili!!!!!!!!!!!!
 
Sasa mleta maada labda uulizwe!
Mantiki ya uzi wako iko wapi?
Bunge kutokwenda hewani live likijadili budget na miswada ya sheria au kuto kwenda live likijadili mambo ya siri?
Kama ungekua na akili heading tu ungebadilisha
Acha mahaba ya kijinga, acha watu waone wawakilishi wao ili next time wafanye maamuzi stahiki kwa mbunge husika!
 
Sasa hata wasipoonesha live hilo bunge watakuja na mrejeshio chanya wa kile wanachokificha. Au ndio kukandamiza wapinzani tu kwa hoja zao na wakileta editing yao luningani hatuoni pale upinzani walipotoa challenge kwao. Huu uzi hauna mashiko umekaa kiushabiki zaidi...
 
Ungeonekana muungwana kama ungehitimisha kwa kuzingatia marejeo yako ya mataifa ya Magharibi ila sasa ninadiriki kusema kuwa wewe unafikiria kwa kutumia tumbo badala ya akili!!!!!!!!!!!!

Mataifa ya Magharibi mengi hayana hiyo sera sababu mengi yao yalikuwa ndio wakoloni waliotawala nchi zingine.mfano uingereza iliitawala marekani.Marekani lilikuwa koloni la Uingereza kama sisi watanzania.Wao wanajiamini kuwa wana akili hivyo ukiwatizama kwenye maswala ya brain Drain hawashupalii kama wamarekani kuhitaji BRAINS toka nchi nyingine.Marekani ndiko kumejaa vijana wengi wenye akili kutoka nchi karibu zote duniani wa kila rangi na kila kabila.Marekani ni nchi ya nchi nyingi

Sera hiyo ya kubadilisha na kuchanganya DNA kwa kuleta vijana wenye akili ndio ilifanikisha hata Raisi OBAMA kupatikana.Baba yake Obama alikuwa kijana wa Kijaluo mwenye akili mno aliingia Marekani kutokana na ujana kuchemka alipokutana na mama yake Obama HAKUMKAWIZA hivyo akaacha DNA mpya marekani kwa mama wa kizungu ya mtoto mwenye akili ambaye sasa ni raisi wa marekani.

Kuna hata baadhi ya makabila tuliyonayo Tanzania kuna baadhi inabidi yatumie hii sera ya Marekani kujikwamua.Unakuta kabila liko nyuma mno na ni la wajinga wajinga fulani hivi.Serikali inaweza saidia mfano mchaga akimaliza chuo kikuu serikali ihakikishe anapangiwa mikoa ile iliyo nyuma sana kimaendeleo na asipewe uhamisho walau akae hata miaka kumi huko.Akikaa aweza oa au olewa huko akachanganya DNA vikaanza kuibuka vizazi vya wenye akili za biashara WAKIOA AU KUOLEWA NDOA ZA MCHANGANYIKO NA MAKABILA HUKO WALIKOENDA.

Pia wale vijana mfano wanaomaliza vyuo wanaotoka makabila yaliyo nyuma sana ni vizuri kuwapangia mikoa ile iliyoendelea sana wakae huko wajifunze maendeleo na waweza bahatika kuoa na kuolewa huko wakachanganya DNA.

Hata humu JAMIIFORUMS kuna watu inatakiwa wachanganye DNA.Ukiangalia mtu anachoandika unaogopa kuwa kama yuko hivyo asipochanganya DNA aweza toa mtoto jinga wa ajabu.
 
Back
Top Bottom