Mkoba wa Mama
JF-Expert Member
- May 5, 2021
- 201
- 84
Sekta ya afya ni sekta muhimu sana na inapaswa kupewa kipaumbele.
Kumekuwepo na changamoto kadhaa katika utoaji wa hudumu za afya nchini zinazosababishwa na mambo mbalimbali.
Hapa kuna baadhi ya maboresho yanayoweza kufanyika ili kutoa huduma bora nazakuaminika zaidi.
Wahudumu wa afya wasitumie simu binafsi wakati wa kazi/wanapotoa huduma, kuwepo na simu maalumu za ofisini hizo ndio zitumiwe na watoa huduma za afya pale wanapohitaji kuwasiliana hasa mawasiliano yanayohusu huduma kwa wagonjwa katika vitengo mbalimbali ndani na nje ya hospitali.
Wahudumu wengi wa afya wamekuwa wakitumia simu wakati wanasikiliza/kumhudumia mgonjwa, hii inapunguza umakini na ubora wa huduma inayotolowe, wakati mwingine inatokea mgonjwa anatoa maelezo ya tatizo alilonalo wakati huohuo daktari akiendelea kutumia simu yake aidha akichati/kuangalia video/kusikiliza sauti zinazosikika katika simu yake/kupokea na kuongea na mtu kwenye simu katikati ya mazungumzo na mgonjwa, na mbaya zaidi mazungumzo hayo hayahusiani na kumhudumia mgonjwa, hii inapelekea huduma mbovu inayotokana na kutokusikia vizuri maelezo muhimu anayokuwa akiyatoa mgonwja, mgonjwa kutokuwa na Imani na ubora wa matibabu atakayopatiwa, mgonjwa kutokuwa na imani na mtoa huduma na pia inamfanya mgonjwa kujisikia vibaya/kutokuthaminiwa.
Kuwepo na kamera za kunasa matukio (CCTV) katika wodi za wagonjwa.
Itasaidia kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma hasa kwa wauguzi.
Mara kadhaa kumekuwepo na malalamiko kuwa baadhi ya wauguzi kutoa huduma kinyume na taratibu zilizopo/chini ya kiwango pamoja na lugha mbaya kwa wagonjwa/ndugu wanaowauguza wagonjwa.
Kuwepo kwa kamera hizi itasaidia kunasa na kuhifadhi matukio yote yanayoendelea wodini kwa ajili ya kumbukumbu na ushadidi pale itakapo hitajika.
Kuwepo kwa kitengo maalumu au dawati la polisi katika kila kituo cha kutolea huduma za afya.
Utaratibu huu utaboresha, kurahisisha na kuharakisha utoaji wa huduma za afya hasa zile zinazomtaka mgonjwa awe na fomu ya maelezo kutoka polisi (PF3 Form) ndipo atibiwe.
Kwa sasa kuna changamoto kubwa kulingana na utaratibu uliopo, mgonjwa anatakiwa kwanza, kwenda kituo cha polisi kupata fomu ndio aende hospitali kwa ajili ya kupata matibabu, hii inaweza kusababisha madhara makubwa au pengine kifo kutokana na mgonjwa kuchelewa kupata matibabu kwa wakati, ukizingatia hospitali nyingi zipo mbali na vituo vya polisi. Kuwepo kwa dawati la polisi katika kila kituo cha kutolea huduma za afya itarahisisha mgonjwa kwenda moja kwa moja hospitali na kupata fomu hapohapo huku akiendelea na matibabu.
Kutengwa kwa siku/tarehe maalumu angalau kila mwezi au baada ya miezi 2 mpaka 3 kwa ajili ya kutoa huduma ya bure ya vipimo kwa wananchi hasa kwa magonjwa yasiyo ambukiza na yasiyo pewa kipaumbele kama vile shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo, saratani, magonjwa ya macho, n.k.
Hii itawasaidia watu wengi kutambua mapema ikiwa wana magonjwa hayo na hivyo kuanza matibabu mapema kabla ya ugonjwa kufika hatua mbaya ambayo itahitaji gharama kubwa zaidi ya matibabu au kulete madhara mengine mwilini.
Watu wengi hutambua magonjwa haya yakiwa tayari katika hatua mbaya kutokana na kushindwa kwenda vituo vya afya kwa ajili ya uchunguzi au kutokana na gharama.
Siku/tarehe hiyo pia itumike kutoa elimu kwa umma kuhusiana na magonjwa hayo na kuhamasisha wananchi kujenga utaratibu wa kuchunguza afya zao mara kwa mara hata kama hawahisi mabaliko yoyote ya kiafya.
Huduma ya kuhifadhi miili (maiti) itolewe bure kwa wale waliofariki wakati wakiendelea na matibabu katika hospitali husika.
Unakuta mtu amelazwa hospitali kwa mda mrefu sana na baadae kufariki wakati akiendelea na matibabu na mtu huyu ametumia gharama nyingi sana wakati wa matibabu yake, kuwadai ndugu kulipia gharama za kuhifadhi mwili wa mtu ambaye ametibiwa katika hospitali hiyohiyo kwa kipindi kirefu na kulipia gharama nyingi za matibabu ni kuwaongezea gharama na kuwasononesha zaidi.
Wagonjwa wasipewe karatasi ya dawa (prescription) na fomu za bima.
Kwa kuwa teknolojia imekua, mgonjwa akishafika mapokezi bima yake ikahakikiwa/analipia pesa, kupitia mfumo taarifa zitumwe moja kwa moja kwa daktari anayetaka kuonana naye, akishaonana na daktari taarifa zinatumwa maabara, akifika maabara anataja jina lake/namba ya faili watu wa maaabara wanaangalia kwenye mfumo vipimo anavyotakiwa kupima, akimaliza kupima anarudi kwa daktari kupokea majibu ya vipimo, baada ya hapo anaenda duka la dawa ambapo atakuta tayari taarifa zake zimeshatumwa, anatakiwa kupewa dawa gani, baada ya kupata huduma, kwa wagonjwa wa bima wasaini kwa kutumia alama za vidole/zile mashine za kusaini kwa kalamu maalumu. Karatasi zitumike pale tu mteja anapotakiwa kununua dawa nje ya hospitali Tupunguze uchafuzi wa mazingira, kubebesha wagonjwa mizigo mingi na matumizi yasiyo ya lazima ya karatasa yanaongeza gharama.
Kuwepo na namba maalumu ya kupiga simu bure kwa mamlaka za juu na sio kwa uongozi wa hospitali husika, mara baada ya kupokea huduma na kutoridhishwa nayo, mgonjwa/mteja aelezee huduma aliyopewa na jina la aliyemhudumia na aeleze hajaridhishwa kwa namna gani na ikitokea mhudumu mmoja amelalamikiwa zaidi ya mara 2 uchunguzi ufanyike kubaini shida ipo wapi na hatua zichukuliwe.
Majengo ya maabara yajumuishe vyoo ndani kwa ndani ili kurahishisha na kuongeza ubora wa uchukuaji wa vipimo (sample), kuondoa usumbufu wa wagonjwa kutoka nje na kwenda katika vyoo vya nje ambavyo wakati mwingine sio safi na vinakuwa mbali kukoka ilipo maabara, kuhifadhi siri za mgonjwa, utakuta mgonjwa amebeba mkononi vipimo na kutembea navyo kutoka chooni mpaka maabara na kufanya kila mtu aliye karibu kufahamu kinachoendelea, kuhatarisha afya za watu wengine kwa kutembea na vipimo hivyo mkononi bila hata kuvaa gloves/tahadhari nyingine yoyote, lakini pia humfanya mgonjwa kukosa kujiamini kwa kushikilia mkononi vipimo hivyo.
Kila hospitali kuwepo na jengo la kupumzika na kulala ndugu wanaowauguza wagonjwa ambao wanahitaji mtu awepo karibu kwa ajili ya kumsaidia.
Baadhi ya wagonjwa mfano, waliotoka kujifungua, wanaosubiri kufanyiwa upasuaji, wasio weza kuzungumza, n.k huhitaji uwepo wa karibu wa ndugu kwa ajili ya kuwasaidia/kutoa maelezo ya mara kwa mara kwa wauguzi, lakini kutokana na utaratibu mtu ambae sio mgonjwa haruhusiwi kukaa wodini isipokuwa ule mda maalumu wa kuona wagonjwa, uwepo wa majengo maalumu ya kupumzika itarahisisha, kuwapunguzia gharama na kuwasaidia kuwepo karibu wanapohitajika.
Itungwe sheria ya kuwachukulia hatua na kuwashitaki ndugu wa mgonjwa wanaokaa na mgonjwa nyumbani mpaka pale anapokuwa na hali mbaya kiafya (mahututi) ndio wanampeleka hospitali. Tabia hii inachangia usugu wa ugonjwa, inasababisha vifo vingi ambavyo vinaweza kuepukika na kuongeza gharama za matibabu.