Mabomu zaidi kulipuliwa Mbagala:Jeshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu zaidi kulipuliwa Mbagala:Jeshi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 23, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,490
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  Mabomu zaidi kulipuliwa Mbagala:Jeshi
  Waandishi Wetu
  WATAALAM wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wamepanga kulipua mabomu mengine mengi yanayoelezwa kuwa na athari zaidi.

  Jana wataalam hao walimfuata mkuu wa wilaya ya Temeke kwenye ofisi ya Kata ya Mbagala Kuu kuomba kibali, lakini hawakumkuta mkuu huyo ambaye amekuwa akishinda kwenye ofisi hizo tangu kutokea kwa milipuko.

  Habari za ndani zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na mmoja wa maafisa hao wa jeshi na mmoja wa maafisa wa kata ya Mbagala Kuu, zinasema kuwa jeshi hilo sasa linafanya utafiti kujua athari ya mabomu linayotaka kuyalipua.

  "Maafisa hao wamefika kuonana na mkuu wa wilaya ili wampe taarifa kwa kuwa wanafanya utafiti eneo hili kujua umbali wa makazi ya watu na eneo la kambi ya jeshi kabla ya kulipua mabomu zaidi yaliyookotwa," alisema afisa huyo ambaye hakutaka kutajwa gazetini.

  "Kwa kuwa hawakumkuta, wametuomba tumfikishie mkuu wa wilaya taarifa hiyo."

  Mmoja wa maafisa wa jeshi waliofika ofisini hapo alilithibitishia gazeti hili kuwa ujio wa wataalam hao ni kwa ajili ya kuonana na mkuu wa wilaya kwa taarifa maalum.

  "Mimi nafahamu sababu za ujio huu, lakini siwezi kusema kwa kuwa si msemaji wa jeshi, ni vema ukawatafuta wasemaji,” alisema.

  Jitihada za gazeti hili kumpata mkuu wa wilaya ya Temeke, Said Mkumbo kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda kwa kuwa jana alikuwa kwenye semina kutwa nzima.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi alilieza gazeti hili kuwa ana taarifa za ujio wa kamati hiyo, lakini hakujua kwa nini walimtafuta mkuu wa wilaya.

  "Hiyo ni kamati iliyoundwa na waziri wa ulinzi kuchunguza chanzo cha milipuko hiyo na kila wakati wanafanya kazi eneo hilo," alisema Lukuvi.

  "Kilichowapeleka kwa mkuu wa wilaya leo (jana) sijui kwa kuwa sikuwauliza kwa sababu walinieleza kuwa juma lijalo wanakuja kwangu."

  Mtaalam wa kuteketeza mabomu hayo, Brigedia Ulomi alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, alisema:"Mimi si msemaji wa jeshi isipokuwa kama kuna tukio la kulipua mabomu, jeshi haliwezi kukurupuka. Wananchi wataarifiwa kwanza."

  Mwenyekiti wa kamati hiyo, Meja Jenerali SC Riyoba hakupatikana kuzungumzia suala hilo.
  Tuma maoni kwa Mhariri
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Huh!

  More Viziwi's...

  More school absentism...

  More BUILDINGS CRACKS...

  More government expenditure as a result of compensation

  to the property owners...
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,490
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  More lovers.....
   
Loading...