Mabomu yarindima arusha

Mabomu yarindima arusha

Lutala

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2010
Posts
848
Reaction score
104
JESHI la polisi mkoani Arusha limelazimika kuwatawanya wafuasi wa Chadema kwa kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi. Wafuasi hao walikuwa wakitoka mahakamani huku wakimsindikiza mbunge wa jimbo la Arusha mjini, Godbles Lema (pichani kati) kuelekea ofisini kwake.

Vurugu hizo zilitokea punde wakati wafuasi hao wakiwa katika barabara ya Boma ambapo walipofika mkabla na ofisi ya mbunge huyo iliyopo jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ndipo mkuu wa polisi wilayani Arusha,Zuberi Mwombeji aliapomuru polisi kufyatua mabomu na risasi za moto angani kitendo kilichofamya wafuasi hao kutawanyaika huku mbunge Lema akikimbilia ofisini kwake.

Wafanyabiashara waliokuwa karibu na eneo hilo walionekana wakifunga maduka huku ofisi za manispaa ya Arusha na watu waliokuwa ndani ya jesngo la ofisi ya mkuu wa mkoa wakitoka nje ya jengo hilo kushuhudia vurugu hizo huku polisi waliokuwa kwenye magari mawili aina ya defender moja lenye namabri PT 1844 wakijitahidi kuwatawanya wafuasi hao .

kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha, Akili Mpwapwa alipoulizwa juu ya tukio hilo alishindwa kukiri wala kukataa juu ya tukio hilo lakini alidai kuwa ofisi yake bado inafuatilia tukio hilo kwa kina na atatoa taarifa kamili baadaye.
 
Andengenye katumwa kwa kazi maalum,.....
 
kwa hali hii watalii watakuja arusha, watuambie kulikoni??????
 
Askari wetu, bado wapo kisiasa. Wamevaa magwanda na mifukoni wana kadi za CCM.
 
Lkn utawasikia ccm wakisema itelejensia yao ilionekana kutakuwa na vurugu
 
Hao wafuasi walifanya fujo gani hadi watawanywe? kama kuna taasisi bongo inaongozwa kimbumbumbu na wafanyakzi nao ni vihiyo inapaswa kuwa ni Polisi!
 
mimi naona tahrir square ya tanzania iwe arachugga, na sio daresalam,.. Maeneo clock tower pale mpaka maeneo ya ofisi ya mkuu wa mkoa na kuendelea mpaka aicc wananchi watande tu barabarani. Tuone polisi watafanya nini...
 
najuta kwann nimezaliwa tanzania!!

Una walaani baba na mama yako kwa kukuzaa. kuzaliwa TZ sio issue coz unaweza sepa ukaenda hata hapo kenya kama huna pesa ya kukupeleka marekani au wingereza!!!

shame on you!! Wasomali pamoja na matatizo yao they are proud of their country na hutamsikia hata mmoja akitamka utumbo kama huo!! tatizo ni wazazi wako!! ila hawjaakufunga pingu na nenda kokote utakapo duniani. ila kumbuka huko unapokutamani kuna watu wamefanya kazi pakawa pazuri ili ma sponger kama wewe muende kuweka makalio yenu tu!!!!!
 
Una walaani baba na mama yako kwa kukuzaa. kuzaliwa TZ sio issue coz unaweza sepa ukaenda hata hapo kenya kama huna pesa ya kukupeleka marekani au wingereza!!!

shame on you!! Wasomali pamoja na matatizo yao they are proud of their country na hutamsikia hata mmoja akitamka utumbo kama huo!! tatizo ni wazazi wako!! ila hawjaakufunga pingu na nenda kokote utakapo duniani. ila kumbuka huko unapokutamani kuna watu wamefanya kazi pakawa pazuri ili ma sponger kama wewe muende kuweka makalio yenu tu!!!!!

Mkuu, ungetumia a polite language, bado angepata message.
Hata hivyo nakushukuru kwavile unaonekana wewe ni mzalendo kama mimi.
Pamoja na matatizo yetu ya umeme na miundombinu mibovu, naona ni bora kuishi Tanzania ambako watu wananiheshimu kwa jinsi nilivyo, kuliko kuishi nchi za watu ambako wanakuheshimu kinafiki.FOR A BLACK TANZANIAN, there is no better place than TANZANIA. Tuipende Tanzania, na tutatue matatizo yetu.
 
Back
Top Bottom