Mabomu yanalindima mjini Mtwara wananchi wamechachamaa

Mabomu yanalindima mjini Mtwara wananchi wamechachamaa

Sunshow

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2011
Posts
1,140
Reaction score
395
Hivi sasa mabomu yanalindima kati ya polisi na wananchi waliyokusanyika kupinga gesi kwenda Dar. Hali ni ya wasi wasi kweli.
 
Ee Mungu tunusuru kwa hali inavyoonekana gesi badala ya kutuletea neema inaweza yakawa kama ya sudani kusini.
 
hebu tujuze vizuri nn kinajiri hasa!!!
 
Mkuu hebu kuwa makini na yote yajirio hapo na ikiwezekana na picha uitupie mkuu!!!!


Huo ndio uongozi bora ya serikali ya chama cha majambazi a.k.a ccm......................wananchi wapiga kura wanapigwa na vitu vizito vyenye ncha kali.
 
Nipo hapa uwanja wa mashujaa watu wanatawanyika mno,milio ya mabomu inasikika kutoka maeneo ya chikongola..kwahali ilivyo ni kwamba kulikuwa na ujio wa Mbatia mbunge NCCR kafanya mkutano wa hadhara hapa mashujaa,badala ya yeye kusimama kwa hoja yake kwamba gas isihame mpaka wananchi wanufaike ye analeta xtor nyingine,maragas ipo nying tuiache tu iondoke ndipo wananch walipoona analeta siasa wakaanza kumzoea ashuke jukwaan na alipopanda gari kundi la watu wakawa wanaimba wanamfata kwa nyuma huku wakiimba gas haiami mpaka kieleweke..sasa inaonekana hali imekuwa tete mpaka polisi wameingilia kati na kuanza kupiga mabomu,ni usiku cwezi kupiga picha..sorry.
 
Jamani hebu tufafanulieni, Taarifa ambazo sina uhakika nazo zinasema Chanzo ni MBATIA James ambaye alienda kuwasisitizia wananchi kuwa gesi lazima itoke tupeni ukweli wa hili maana niliyekuwa naye yuko kwenye heka heka ya kujinusuru na milipuko na hakuwa eneo la tukio wakati linaanza alikuwa na safari zake tu huenda kauli yake isiwe sahihi.

NYONGEZA:
Anadai watu walikuwa wanataka kumshambulia mbatia kwa madai kuwa katumwa
na Rais ili mpango wa gesi kwenda Bagamoyo ukubalike.
 
hahahaha..nitahamia mtwa muda siyo mrefu..safi sana wana mtwara simamieni mali zenu msije mkawa kama sisi wasukuma ccm wanachota madini tu sisi tukibaki na mashimo tu..
 
Zoeeni wananchi, serikali yenu inawapa Inglish kozi ya kuzoea mabomu,baadae tutayaona kama viazi
 
gas inamwaga damu kwa sababu JK tayari ameshachukua mabillion ya makampuni ya gas nakuyaficha uswiss.
 
uzoefu wangu ni kuwa miradi mingi inabuniwa na watawala bila kuhusisha watawaliwa.
 
Msg kwa kikwete utachukuaje gas ya watu na tanzanight ya Arusha wangepeleka dar basi hii c fair at all
 
Kwanini mabomu yapigwe?
Kwani kuna fujo zinatokea?
Ni baada ya wananchi kutorizishwa na kauli ya Mbatia na kumuona kama vile katumwa. Mimi nimeshuhudia kundi kubwa la watu likiwa limeizingira ofisi ya NCCR Mageuzi maeneo ya Chikongola ambapo inasemekana Mbatia alikuwa amehifadhiwa ndani hao watu walikuwa wakipiga kelele hawataki Mbatia alale Mtwara na badala yake aende alale Lindi kwa kitendo alichokionyesha. Baadae kidogo Mbatia alifanikiwa kuchomoka kupitia mlango wa nyuma ndipo wananchi baada ya kugundua wakaamua kumfukuza ndipo baadae kidogo yalianza kusikika mabomu yakilindima.
 
Back
Top Bottom