Mtandao huu sasa naona upo kimya kuhusu mwendelezo wa mabomu kule Arusha. Ilipotokea pale mwanzo Chadema na CCM waligeuza vitendo hivyo kama mitaji yao ya siasa. Sasa mabomu yameendelea mnasemaje wana Chadema na CCM? Mbona mapovu hatuyaoni? Au ni afadhali taifa liangamie kuliko chama kuangamia?
Tatizo kubwa na ambalo huenda litaiangamiza Tanzania ni kuchukua kila kitu kisiasa. Polisi wetu ndiyo kabisa wameleweshwa siasa za Chadema vs CCM. Upelelezi wao ni lazima ulenge mambo ya siasa. Inawezekana kabisa mambo yanayotokea yana mrengo wa siasa lakini si siasa za Chadema vs CCM. Ni pana zaidi.