Mabomu na wategaji wake, je usalama wa taifa huwa wapi?

Mabomu na wategaji wake, je usalama wa taifa huwa wapi?

Makene

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
1,475
Reaction score
282
Najiuliza inakuwaje watu kutega mabomu na kuyalipua bila usalama wa taifa na inteligensia ya polisi kushindwa kujua kimbele na kuchukua hatua za kuzuia madhara yanayotokea?
Sioni mantiki ya majigambo na 'coverage' wanayofanyiwa wakuu wa polisi wa mikoa baada ya kutokea tukio ambalo raia wanakuwa tayari wamepata matatizo. Usanii umezidi.

Wadau nitoeni mashaka na hii mifumo legelege.
 
ingekua mkutano wa CDM wangesshatoa taarifa za kiintelijensia

Wako bize kuandaa video za kuonyesha viongozi wa CHADEMA wakipanga ugaidi...
 
Najiuliza inakuwaje watu kutega mabomu na kuyalipua bila usalama wa taifa na inteligensia ya polisi kushindwa kujua kimbele na kuchukua hatua za kuzuia madhara yanayotokea?
Sioni mantiki ya majigambo na 'coverage' wanayofanyiwa wakuu wa polisi wa mikoa baada ya kutokea tukio ambalo raia wanakuwa tayari wamepata matatizo. Usanii umezidi.

Wadau nitoeni mashaka na hii mifumo legelege.

Wao ndiyo wahusika refer Ramadhan Ighondu
 
Wameumuuwa Padri Mushi (RIP) Zanzibar leo wanataka kumuua balozi wa Papa.. Endeleeni kuwachekea anakina Ponda na Ilunga
 
Kwa kweli nchi iko hatarini maana ni kama wanausalama wako likizo. Watanzania tuwaamshe wanausalama wetu kwa kufanay maandamano ya amani nchi nzima.
 
ni vigezo gani vilitumika kumteua Mkurugenzi wa Usalama wa taifa na IGP??

mkuu wa kaya mbona hataki kuwaondoa hawa watu??

wenye akili tumeishagundua kuna kamtandao, kanakoratibiwa na mkuu ili nchi iingie kwenye machafuko,

nadhani ni kwa manufaa ya mabeberu na vibaraka wao ili waje wachote rasilimali kiulaini,

mchafuko yakianza mkulu atapewa hifadhi katika mojawapo ya nchi za ughaibuni??

je atakimbia na ndugu zake na ukoo wake wote?? tusubiri time will tell

Najiuliza inakuwaje watu kutega mabomu na kuyalipua bila usalama wa taifa na inteligensia ya polisi kushindwa kujua kimbele na kuchukua hatua za kuzuia madhara yanayotokea?
Sioni mantiki ya majigambo na 'coverage' wanayofanyiwa wakuu wa polisi wa mikoa baada ya kutokea tukio ambalo raia wanakuwa tayari wamepata matatizo. Usanii umezidi.

Wadau nitoeni mashaka na hii mifumo legelege.
 
Maafisa usalama wengi wa siku hizi wanachaguliwa kiundugu na kiurafiki bila kuangalia IQ zao
Hawana uwezo kiintelijensia
 
Rais moja kwa moja anahusika kwenye matukio haya sio hali ya kawaida kabisa, Rais wetu huyu bana akili zake anazijua mwenyewe madaraka aliyopewa hafanyi kama watu walivyotegemea mdini sana jamaa anafurahi tu .ukiangalia waliofanya uhalifu kwenye makanisa mbagala kule waliokamatwa hawawezi hata kulipa hata nusu ya hasara waliyosababisha lkn bado haya mambo yanaendelea tu .
 
Waliochaguliwa hawajui kazi zao mana walikua kijiji kama maafisa wa utendaji leo usalama wa taifa atajua nini? Kama sio kusubili mwisho wa mwez ahamie bar na kurubuni watoto wadogo na kuwapa chips,.. Hawafahamu ni mizigo tu. Subili wanandaa Tume
 
wameumuuwa padri mushi (rip) zanzibar leo wanataka kumuua balozi wa papa.. Endeleeni kuwachekea anakina ponda na ilunga

mungu wetu yu hai wataaibishwa kama lucifer! Anguko lao ni kubwa na ndio maana wanachuki.
 
ostsNi matokeo ya kupeana kaz na ajira kwa misingi ya dini kabila ushost na upendeleo mwingine bila kujali taaluma mtu aliyosomea! kila mtu analo jibu kilichobaki ni kipenga kupulizwa tu mechi ianze
 
Nchi iko peke yake hii

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Inaonekana wana usalama wetu wako kwa ajili ya kuwalinda vigogo na sio wananchi wa kawaida. Kama kwenye ufunguzi wa kanisa lililolipuliwa Rais angekua anakuja, watu wangepekua kila kona kabla mheshimiwa hajaingia na macho yangekua kazini muda wote akiwa hapo kwenye tukio, kwa bahati mbaya hakuwepo..maisha yamepotea, watu wamepata vilema vya maisha just because watu hawajali.

Usalama wa Taifa na polisi mna damu mikononi mwenu, kwa yaliyotokea leo hamuwezi kuepuka lawama. Wananchi maskini wanauwawa kwa jambo ambalo mngeweza kulizuia kama mngekua makini na kazi zenu, kwa kuwa leo ni jumapili- priority ilikuwa ni bia na nyama choma na wengine mlipoamkia mnajua wenyewe. Kwa matukio mabaya machache tu ambayo yametokea recently kwa waumini wa kikristo, hata mwanangu aliyepo nursery sasa hivi angejua nini kinapaswa kufanyika kabla tukio la ufunguzi wa kanisa lile haujaanza na wakati shughuli nzima inaendelea.

Raisi wangu JK, kama unaijali nchi katisha ziara ya huko ulipo urudi nyumbani sasa hivi! Najua hutafanya hivi kwa kuwa hujali na utalala usingizi mnono huko ulipo as if nothing has happened.....prove me wrong on this! Anyway, kazi ya kwanza ninayokuomba uifanye utakapojiskia kurudi ni kuwapiga chini wakuu wa jeshi la polisi na mwenzie wa usalama wa taifa kwa kuwaangusha watanzania kwa mara nyingine tena. Wakristo wamekuwa wavumilivu sana na waelewa kwa yote mabaya wanayotendewa, itakua ni kosa kubwa tuki assume kuwa wataendelea kuwa wavumilivu, vita ya waislamu na wakristo inanukia, nimeskia watu wakianza kusema 'enough is enough', taifa linaelekea kubaya..Can you imagine kama msikiti ndio ungekua umepigwa bomu leo ingekuwaje?
 
Hapa bongo usalama wa taifa kazi yao ni kutishia raia tu ili wawe wanakunywa bia bure!!! Na kufanikisha nipangi ya "siem-siem"
 
hawa maaskofu nao wanausika kwa yote haya yanayotokea hawana pa kutokea waache kurukaruka. Kwani walishatoa kauri tata leo ndo tunaona matunda. Au mnajifanya mmsahau .rais gani mwenye mambo ya k...ke. Sisi ndo tulomweka madarakani tukiamua nchi hii aitawaliki. Kauli hizo na nyingine nyingi zimetolewa na haohao. Leo mnashangaa nini ?
 
Elimu ya kutengeneza Bomu Watz wameipata wapi jamani? mbona hiyo ni elimu hatari Haidhibitiwi kama ilivyo kumiliki silaha kama Bastola.? Wale Boston kue Marekani nasikia walitumia Sufuria Pressure cooker kulipua watu.
 
hawa maaskofu nao wanausika kwa yote haya yanayotokea hawana pa kutokea waache kurukaruka. Kwani walishatoa kauri tata leo ndo tunaona matunda. Au mnajifanya mmsahau .rais gani mwenye mambo ya k...ke. Sisi ndo tulomweka madarakani tukiamua nchi hii aitawaliki. Kauli hizo na nyingine nyingi zimetolewa na haohao. Leo mnashangaa nini ?
wacheni viongozi wa dini wapumue mlitaka waseme ni chaguo la shetani wakati amechaguliwa na wananchi wengi?
 
Back
Top Bottom