Mabomu Mbagala yadaiwa kulipuka kwa uzembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu Mbagala yadaiwa kulipuka kwa uzembe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, May 14, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  Date::5/14/2009
  Mabomu Mbagala yadaiwa kulipuka kwa uzembe

  Na Mwandishi Wetu

  Mwananchi

  IKIWA ni majuma mawili tangu kulipuka kwa mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyoko Mbagala, jijini Dar es Salaam, inadaiwa kuwa tukio hilo lilisababishwa na uzembe.

  Mtaalamu mmoja wa mabomu wa JWTZ ambaye hakutaka kutajwa gazetini kuwa sio msemaji wa jeshi, alidai kuwa milipuko ya mabomu hayo yalisabioshwa na uzembe ulisababishwa na askari wasio wazoefu kuingia katika ghala hilo lililokuwa linatumiwa kihifadhi mabomu ya aina mablimbali na risasi.

  ‘‘Huu ni uzembe na kwamba askari walioingia katika ghala hilo walikufa baada ya mabomu kulipuka,” alidai askari huyo.

  Alifahamamisha kuwa mabomu hayo yana tabia ya kulipuka na kuleta athari kwa viumbe kuanzia usawa wa kiuno, ndiyo maana askari hulala chini, muda mfupi baada ya kulilipua.

  Mtaalamu huyo alieleza uzembe mwingine alidai kuwa unatokana na baadhi ya mabomu kuwa ya muda mrefu hivyo muda wake wa kutika ulikwisha.

  Hata hivyo alidai kuwa mabomu yaliyolipuka Mbagala hayana athari kubwa kiafya ispokuwa kisaikolojia.

  ‘‘Wakazi wa Mbagala wanaweza kupata athari za kisaikolojia na tatizo la msukumo wa damu kwa mshituko kutokana na kishindo cha mabomu hayo yalipokuwa yanalipuka,” alidai mtaalamu huyo.

  Madai ya mtaalamu huyo yametolewa wakati wakazi wa mbagala wakiendelea kukabiliwa na athari za mabomu hayo ambayo yanaendelea kulipuliwa na kuokotwa katika eneo hilo na kulifanya kuwa si salama kuishi.

  Mpaka sasa zaidi wa watu 25 wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa, kaya 3,000 haina mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa pamoja na watoto kadhaa kupotea na mpaka sasa hawajulikani kama wamekufa au la.

  Zaidi ya hapo, athari za mabomu hayo zimesababishwa watoto wapatao 200 wanakabiwa na uziwi uliosababishwa na sauti nzito za mlipuko huo akiwemo mmoja ambaye ameathirika kisaikolojia kisai cha kutopenda kusikia kelele na mwingine kutopata usingizi.

  Pia mahuddhurio wa wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi yamepungua huku ikiripotiwa kwamba, nusu ya wanafunzi wa shule za Mbagala Kuu na Maendeleo zilizokaribu na kambi hiyo hawafiki shuleni.

  Wanasheria waonya

  Boniface Meena anaripoti kuwa, wanasheria maarufu jijini Dar es Salaam Jerome Msemwa na Professa Abdallah Safari wamesema Serikali ilipaswa kuchukua tahadhari ya suala hilo haraka kwa kuwa kambi hiyo ipo karibu na makazi ya watu.

  "Hiyo ni sheria ya madhara na tahadhari, ni kanuni ya sheria ya uzembe, hivyo serikali ilitakiwa kuwalinda majirani wa kambi hiyo ili wasipate madhara," walisema wanasheria hao.


  Waliongeza: "Wale ni jirani zao hivyo kuweka mabomu karibu na makazi ya wananchi walitakiwa wachukue tahadhari, hivyo kwa yaliyotokea wamekiuka kanuni ya tahadhari ikimaanisha kuwa serikali imefanya uzembe".

  Profesa Safari alisema serikali haikutakiwa kufanya uzembe katika masuala kama hayo kwa kuwa inajua kuna wananchi wanakaa maeneo hayo na wanajua kuwa mabomu hayawezi kulipuka yenyewe, hivyo inaweza kushtakiwa na wakazi wa eneo hilo.

  "Serikali imefanya uzembe na inaweza kushitakiwa kwa uzembe," alisema Prof Safari.

  Msemwa alisema kanuni ya sheria ya uzembe inaeleza kwamba, kila mtu anapofanya shughuli zake anatakiwa amlinde jirani yake; hivyo serikali ilitakiwa iwalinde majirani wa kambi hiyo ya jeshi ambao ni wananchi.

  Alisema pamoja na kwamba serikali imesema itawasaidia kwa hali na mali na kuwalipa, bado wananchi ambao hawataridhika na fidia watakazolipwa na serikali wanaweza kufungua kesi ya kutaka kufidiwa.

  "Mtu yeyote anaweza kwenda mahakamani kama hataridhika na fidia itakayotolewa na serikali," alisema Msemwa.

  Prof Lipumba ashauri

  Naye Salim Said anaripoti kuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka Serikali, kutangaza Mbagala eneo la maafa ili kunusuru maisha na mali za wananchi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Profesa Lipumba aliilaumu serikali akidai kuwa imeshindwa kutoa taarifa sahihi juu ya usalama wakzi wa eneo hilo na mali zao badala yake inatoa taarifa za kupotosha kuwa eneo hilo sasa ni salama.

  “Ni vyema serikali ikatoa kauli ya kutangaza kuwa eneo hilo si salama ili kunusuru maisha na mali za wananchi, kwani kukaa kwake kimya kutasababisha vifo vya ghafla vya wananchi kutokana na mishituko wanayoipata,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza:

  “Hadi jana (juzi) tayari vimeripotiwa vifo vya watu 27 kutokana na milipuko ya mabomu hayo.”

  Profesa Lipumba alifafanua kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwa watoto kupata matatizo ya ulemavu wa kusikia, kutokana na mishindo na mitetemeko mikubwa inayosababishwa na milipuko hiyo.

  Alisema, kutokana na mgongano wa takwimu zinazotangazwa na serikali ikilinganishwa na milipuko inayotokea, inaonekana wazi kuwa serikali haiko wazi, juu ya hali halisi ya milipuko hiyo na idadi ya mabomu yaliyokuwa yamehifadhiwa.

  “Taarifa ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Hussein Mwinyi, ilishindwa kudhihirisha na kuweka wazi uhakika wa zoezi lenyewe na usalama wa eneo la Mbagala Kuu,” alisema Profesa Lipumba.

  Profesa Lipumba, ambaye alidai kuwa milipuko ya mabomu si ya kwanza nchini, na kwamba mwaka 2004 ilitokea katika kambi ya jeshi ya Gongo la Mboto.

  “Inaonesha serikali haijui, kuna mabomu mangapi yenye hatari kwa wananchi na ambayo hayajapatikana hadi sasa na mangapi yaliyolipuka.”

  Alilaumu taarifa za zisizo sahihi zilizotangazwa na serikali kwa ajili ya ulipuaji salama wa mabomu manne uliofanyika Mei 13, mwaka huu majira ya jioni katika eneo la tukio, ambapo ulisababisha baadhi ya nyumba kuendelea kuanguka na watu 80 kulazwa hospitali kwa mshituko.

  “Awali waliwatangazia wananchi kuwa watalipua bomu moja, lakini cha kushangaza na ambacho wananchi hawakutarajia, milipuko ikaongezeka na kuzua hofu kubwa kwa wakazi wa karibu na eneo la tukio” alisema Profesa Lipumba.

  Aidha aliishauri serikali, kuangalia upya suala la milipuko ya Mbagala, ikiwa ni pamoja na kuwatafutia eneo jingine la makazi ya kudumu na kuhakikisha wanawalipa fidia haraka iwezekanavyo waathirika wote, ili waweze kurudi katika hali zao za maisha ya kawaida.

  Pamoja na hilo, Lipumba aliitaka serikali kuwashirikisha wataalamu kutoka nchi za nje, ikiwa ni pamoja na Ujerumani na Marekani katika Baraza la kuchunguza chanzo cha milipuko hiyo ya Aprili 29.

  “Hakuna haja ya kusema kuwa tuna siri hatuwezi kuwashirikisha, Marekani wanatusaidia katika mafunzo ya kijeshi hivyo wanatujua na Ujerumani wanatusaidia katika hospitali za kijeshi, hivyo pia wanatujua, tuwashirikishe basi, ili tuweze kupata data nzuri zaidi” alisema Profesa Lipumba.

  Hata hivyo, Lipumbna alieleza masikitiko yake katika malalamiko yanayojitokeza wakati wa ugawaji wa misaada ya kibinadamu kwa waathirika, akisema hiyo ni aibu kubwa kwa taifa.

  “Ni aibu kubwa kwa taifa letu kwa ufisadi uliojitokeaza katika ugawaji wa misaada ya kiutu kwa waathirika wa mabomu Mbagala Kuu. Kuna watu hawana nyumba lakini watajenga kupitia misaada ya waathirika” alilaumu Lipumba.
   
 2. j

  jibabaz Member

  #2
  May 15, 2009
  Joined: Jun 23, 2008
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaaaaaaaaaaaaawwwwwwwwwwwwwwwwnnnnnnnnnnnnnn!!! (mwayo)
  What is new??
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135

  Sasa kama mwanasheria anawasaidaje wananchi? Mnataka waende mahakamani wenyewe? Na mnasoma sheria kwa ajili ya nini kama sio kusaidia wananchi?

   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Wanataka mjitoleeee muwafuate muwape kazi kufungua kesi ili wapate cha juu...hawana uzalendo.....
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hivi kuna utaalamu gani hapo tulioupata au tulioelezewa ? Na huo uzembe aliujuaje wakati wote waliokuwemo wamekufa ,au anataka kutuambia kuwa wajeshi walioingia hawakulala chini milipuko ilipoanza na kusababisha madhara ya usawa wa kiuno ,sasa sijui kiuno kinapinda au vipi ? Yaani jamaa hata jina la mtaalamu wameficha ,waandishi naona ndio wanaokosa utaalamu wa kumhoji mtu na wanawapachika tu eti mtaalamu kitu gani kitamfanya msomaji aamini kama aliehojiwa ni mtaalamu hakuna ,zaidi ya tungo tata "madhara usawa wa kiuno" Inaonyesha hata huyo mtaalamu ni bomu :D
   
 6. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Uzembe huu ni sehemu ndogo sana ya uzembe mzima wa Serikali ya CCM.Tutalaumu Jeshi.Hivi tunaelewa vyema wanajeshi wetu wanaishi katika mazingiragani?Jeshi letu lipo kimazoea tu, routine za kijeshi za ukaguzi wa vitu muhimu ndani ya jeshi ni kama vile zimezimia au kufa kabisa.Subiri siku tutakapoambiwa kuna Vifaru mpaka BM ndani ya jeshi haijulikani ilipo.Iwapo watu wanaweza kufungua milango ya srong Room za BOT na kuchota hazina, kwa niniwatu wengine washindwa kuuza vifaru kadhaa na mizinga huko Somalia Rwanda Sudan na Congo??Hapa naongea kama mjinga vile, lakini ukweli ni kwamba silaha nyingi hatari za jeshi zimekwisha uzwa kilichobakia ni Log books tu.Mpaka wa kufisadi mali ya umma umewekwa umbali gani kutoka pale maadiri yalipo??Ufisadi hauna ukomo.Kila mtu atauza kilichopo mezani kwake ili awakoge wenzi wake kwa utajiri.Hakuna kilicho salama Tanzania.Ukitaka kuwa rai ni pesa yako.Ukitaka kununua ardhi yote ya kijiji ni pesa yako tu.Iko siku tutaambiwa Ikulu ya Dar inavunjwa na kuhamishiwa Ras Kutan kupisha Mwekezaji toka Uarabuni ambaye anataka kujenga Hotel kubwa na sehemu ya kupumzikia familia za masheik kutoka kwao.Vile visiwa vya Bongoyo sijui bado ni mali ya Tanzania au tayari kuna Taicun kutoka Ulaya kanunua na kuweka Ghala la mihadarati??Naamini kuna kundi kubwa tu la Mafisadi wansubiri kuona kama kuna uwezekano wa kuuza mama na dada zao kwa mataicun wa Italia Ufaransa na Uarabuni.Kwani kuna ubaya ganbi kumuuza mama na dada yako endapo kufanya hivyo kutakuongezea ngawira ya kukoga watu???Ukila nyama ya mtu mmoja nini kitakuzuia kula nyama za watu wengine wote waliobaki???Utatamani nyama ya mbuzi tena??!!!??
   
Loading...