Mabomu mawili 'yaua 69' Pakistan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu mawili 'yaua 69' Pakistan

Discussion in 'International Forum' started by kilimasera, May 13, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mashambulio mawili ya bomu katika kituo cha mafunzo ya kijeshi kaskazini magharibi mwa Pakistan yamesabaihsa vifo vya watu 69, polisi wanasema.
  Watu kadhaa walijeruhiwa katika shambulio kwenye kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Shabqadar,wilaya ya Charsadda.

  Kuna taarifa kuwa walipuaji wawili walitekeleza mashambulio hayo.

  Ni shambulio baya zaidi kuwahi kutokea tangu vikosi vya Marekani vilipomuua kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden katika mji wa Abbottabad, kaskazini mwa Pakistan, tarehe mbili mwezi Mei.

  Makundi ya wanamgambo yameapa kulipiza kisasi kwa kifo cha Bin Laden. Hata hivyo,kufikia sasa hakuna kundi limetangaza kuhusika na shambulio la Ijumaa.

  "kulikuwa na milipuko miwili ya mabomu," Jahanzeb Khan,afisa mkuu wa polisi eneo la Shabqadar,ameambia shirika la habari la AFP.

  Shambulio hilo lilitokea wakati makurutu wapya walipokuwa wanaingia kwenye mabasi kwa likizo fupi baada ya mafunzo,taarifa zinasema.

  Magari kadhaa yaliharibiwa kutokana na shambulio hilo.
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  "We love death. The US loves life. That is the difference between us two." - Bin Laden
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
  :mod::mod::mod:
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
  :mod::mod::mod:
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hivi hawa wanaokufa ni waumini wa dini gani?na haya ni mashambulizi dhidi ya watu gani
   
 6. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  ni revenge dhidi ya wamarekani au dhidi ya wapakistani?
   
 7. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wanaokufa ni wapakistani na waliolipua ni wapakistan!!ingekua wanarevenge kwa wamarekani wangeenda pentagone tena
   
 8. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Manumbu hapo ndo hua siwaelewi kabisa akili yao... Kua hua inawaza vipi/nini... wakitegemea wanamkomoa nani na kwa nini.... Njia zao za kupigana ziko very vulgar, haina logic wala huwezi comprehend their ways... yaani sometimes you wish uingie akilini mwao walau upate mwanga uelewe....
   
 9. T

  The Priest JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Unatukanwa na bosi ofisini,unarudi nyumban na kumzibua kofi mtoto!
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  May 13, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Ivuga .... ?????
   
 11. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  ISI wamezembea sana! Kipind hiki ilibidi wawe makini sana maana zilikuwapo tetesi kwamba Al-qaeda wangelipiza kisasi hata kwa Pakistan yenyewe. Inakuwaje nchi inayopata 20bln usd in military aid kila mwaka kutoka US inashindwa kuzuia kitu kilichokuwa kinahofiwa kutokea? Watu wa intellijensia wakati mwingine wana-fail vibaya sana!
   
 12. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,607
  Likes Received: 6,773
  Trophy Points: 280
  Nyinyi hii game ya Ugaidi siyo rahisi kama mnavyofikiria!.
  Wataalamu wa mambo ya kijasusi wanakwambia mara nyingi vikundi vya kigaidi huwa ni stretched arm ya vyombo vya kijasusi kama vile C.I.A, MI-6 na vingine duniani.

  Mara nyingi wale wanaokwenda kujilipua huwa hawajui A wala B ya agenda nzima ya kile wanachokifanya zaidi ya kuaminishwa kwamba wanafanya hivyo kwa ajili ya kutetea vitu kama dini au nchi au demokrasia n.k, kiufupi wale wanaokwenda front kujipua huwa ni "useful-idiotss", au naives fulani, watu hawa kwenye ujasusi huitwa "Patsies". hawa huwa ni scape-goat ya lawama pindi tukio likitendeka au kushindikana, hawa hutumika bila wao kujijua kwamba wanatumika.

  Kuna kundi linaloitwa "Moles", hawa ni watu kwenye system, wengine wana vyeo vikubwa tu serikalini na ni watu ambao wanajua game yote inavyochezwa, kazi yao ni kuhakisha Patsies wanapata msaada wote wanaohitaji behind the scene, mathalani kama Patsy anakamatwa na polisi, hawa Moles hufanya mbinu za kichibichini ili Patsy aachiwe, kama Patsy anahitaji pesa, hawa Moles huhakikisha Pesa inawafikia Patsies. Lakini hawa Moles hufanya haya yote bila hawa Patsies kuelewa kwamba kuna mkono fulani nyuma yao.

  Kuna kundi la professional-technochrats, hawa ndo brain nzima iliyo nyuma ya sophisticated Terrorist attacks, hawa ni watu wenye training ya hali ya juu, matukio makubwa ya kigaidi huandaliwa na hawa, then Patsies hutolewa kafara tu ili wawe front, ili lawama zote wabebe hawa Patsies. mara nyingi Patsies huwa ni watu ambao ni extremists kama vile ishu za kidini au political ideologies, n.k, lakini wanatumiwa, na wao hawajui kama wanatumiwa.

  Sasa ni kwa nini vyombo kama CIA vinahitaji kuwa na vikundi vya kigaidi sehemu mbalimbali duniani?, ni kwa sababu katiba na sheria za marekani zinazuia hivyo vitendo, mathalani Kuua watu wanaotishia Masilahi ya Kibiashara ya Marekani ni kinyume cha sheria za Marekani, kwa hiyo ni rahisi kwa Chombo kama CIA kutumia kikundi kigaidi kuua watu kama hawa bila kufahamika muuaji halisi ni nani, au chukulia mfano kuna kiongozi anatishia masilahi Ya Marekani ya Mafuta, ni rahisi kutumia kikundi cha kigaidi kama vile Al-Qaeda kumuua kiongozi huyu kwa kisingizio kwamba wanataka kuanzisha Caliphate System au utawala wa Sharia katika nchi hiyo.

  Wakati mwingine Ugaidi hutumika ili kuzivuruga nchi, na nina wasiwasi kwamba Marekani tayari ameshaanza kuivuruga Pakistani kwa kutumia Magaidi, Kitendo cha mauaji ya mara kwa mara ya kigaidi, yatapelekea wananchi kujihisi hawako salama chini ya serikali husika, na hivyo kuikasirikia, kadri hiyo nchi itakavyokuwa inapinga sera za wakubwa" ndivyo jinsi ugaidi utakavyoongezeka mpaka viongozi hao wakubali kuwa vibaraka vya wakubwa ndivyo utakapoona mashambulizi ya kigaidi yanapungua, kiufupi ninadhani Wamarekani wanataka kuivuruga Pakistani ili iwe dhaifu, au iwe Pariah state ili baadae wajenge hoja kwamba Pakistani ni nchi inayoweza kuanguka kwa magaidi na KWA HIVYO NCHI HIYO KUMILIKI SILAHA ZA NYUKLIA NI HATARI KWA DUNIA NA KWA HIVYO UMOJA WA MATAIFA IWANYANG'ANYE HIZO SILAHA. lengo ofcourse ikiwa ni kulinda masilahi ya Wakubwa ya Mafutya katika middle east, pakistani haiwezi kuaminiwa kumiliki silaha hizo kwa sababu za kidini inaweza kuwapa "waislamu wenzake" silaha hizo, au yenyewe kujiunga upande unaoipinga marekani ktk vita.

  Mtaalamu wa Ugaidi mmoja alisema kwamba, takriban vikundi vyote vya kigaidi vimekuwa "infiltrated", na mashirika makubwa ya kijasusi, na vingine huwa ni extended arm ya Vyombo hivyo.
   
 13. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2011
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ukiangalia kiundani zaidi, ili tukio lilikuwa planned kabla ya kifo cha Osama. Kuna fununu kuwa ni Taleban Afghanistan ndio wametekeleza (haiingii akilini) kama wangekuwa wanalipiza kisasi wangelipua Bagram AFB.

  Gamba la nyoka kumbuka kuwa Pakistan ana nyuklia na asilimia kubwa ya wananchi hawaipendi Marekani, serikali ya marekani inafanya kila linalowezekana serikali iliyopo isiangushwe na islamists. Labda useme wamekuwa funded na serikali ya India.
   
 14. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,607
  Likes Received: 6,773
  Trophy Points: 280
  Ukiangalia On the surface utaona hivyo kama unavyoona wewe, hata hivyo hawa western countires wanaanglaia mbele zaidi, 5, 10. or even 20 years later. na kuhusu wapakistani wengi kuichukia Marekani, hiyo nayo ni sababu haswaa ya kuwafanya wamarekani Wajihadhari na Pakistani iliyo united, yenye nguvu. Kumbuka Wamarekani waliishambulia Afghanistani si kwa sababu Afghanistani iliishambulia Marekani, bali kwa sababu walikuwa wakiwapa hifadhi wale ambao Marekani inadai waliishambulia siku ya 9/11. sasa jiulize ni kitu gani kitaizuia marekani kuingia vitani na Pakistani, siku marekani ikiamua wakati inaelezwa kwamba Osama alikuwa Pakistani?. Kiufupi Marekani ashajitengenezea excuse ya kuishambulia Pakistani pindi condition zikiwa ripe au kuiblackmail, au kuiintimidate. hii yote si kwa sababu ya Osama kuwa Pakistani, bali kwa sababu Marekani anazitaka hizo silaha za nyuklia za pakistani.

  kwa sababu ya silaha hizo, lazima hiyo nchi iwe distabilized kwanza, then baadae utashangaa Marekani inaipa Pakistani Carrots and Sticks ili isalimishe silaha zake za Nyuklia, kwa sababu silaha hizo zinatishia Masilahi ya bwana mkubwa katika eneo la Mashariki ya kati, pindi Pakistani ikishakuwa weak, kutokana na force kama hizo za kigaidi ambao nina wasiwasi unafadhiliwa na CIA then itakuwa rahisi kuinyang'anya hizo silaha.
   
 15. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,607
  Likes Received: 6,773
  Trophy Points: 280
  Hebu chekini hii nukuu kutoka katika kitabu cha 9/11 Synthetic terror cha Mr Tarpley, ndo utaona ni kwa namna gani Mataifa haya hutumia Ugaidi ili kutimiza malengo yake.

  "The Northwoods documents start from the premise that the US should be seeking war
  with Cuba over the short term for the purpose of regime change: "[T]he Joint Chiefs of
  Staff recommend that a national policy of early military intervention in Cuba be adopted
  by the United States. They also recommend that such intervention be undertaken as soon
  as possible and preferably before the release of National Guard and Reserve forces
  presently on active duty." Part of the effort would be to demonize Castro and his
  communist government. The Northwoods planners thought that "world opinion, and the
  United Nations forum, should be favorably affected by developing the international
  image of the Cuban government as rash and irresponsible, and as an alarming and
  unpredictable threat to the peace of the Western Hemisphere." How could Castro be
  demonized? Norhtwoods: "Exploding a few plastic bombs in carefully chosen spots, the
  arrest of Cuban agents and the release of prepared documents substantiating Cuban
  involvement also would be helpful in projecting the idea of an irresponsible
  government." In addition, "hijacking attempts against civil air and surface craft could
  appear to continue as harassing measures condoned by the Government of Cuba."
   
 16. N

  Nonda JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  YouTube - Alex Jones 2011-03-31 Thurs. Part 6/9
   
 17. N

  Nonda JF-Expert Member

  #17
  May 13, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Nakubaliana na wewe katika uchambuzi wako.
  Hata ile miripuko ya balozi za US hapa Tanzania na Kenya ni katika hii long term strategy kama ilivyo kwa Libya.
  Sehemu ambazo China inajikita katika Afrika basi "ugaidi wa US" utajitokeza tu.

  Watu waipitie story ya AFRICOM, watayaelewa maandiko yako.
   
 18. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #18
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Taliban wakiri kufanya shambulio Pakistan
  Mabomu mawili katika chuo cha kijeshi kaskazini magharibi mwa Pakistan yameua watu 80, polisi wamesema.

  Watu wasiopungua 120 wamejeruhiwa katika mashambulio hayo katika mji wa Shabqadar, katika wilaya ya Charsadda.

  Baada ya awali kudhani kuwa mabomu hayo yalikuwa yametegwa, sasa polisi wamesema yalikuwa na mashambulio ya kujitoa mhanga.

  Taliban wa Pakistan wamesema wamefanya mashambulio hayo kulipiza kisasi cha kuuawa kwa Osama Bin Laden mapemwa mwezi huu.

  Shambulio la Ijumaa lilikuja saa kadha kabla ya wakuu wa kijeshi kufika mbele ya bunge kuelezea hatua walizochukua kuhusiana na kifo cha Bin Laden.

  Katika mkutano wa faragha, mkuu wa upelelezi Luteni Jenerali Ahmed Shujaa Pasha anaripotiwa kuwambia wabunge kuwa aliwasilisha ombi lake la kujiuzulu baada ya majeshi ya marekani kumuua Bin Laden, lakini mkuu wa majeshi alikataa ombi lake.
   
 19. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #19
  May 14, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  [​IMG]  [​IMG]  [​IMG]  [​IMG]
   
 20. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #20
  May 14, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  [​IMG]  [​IMG]   
Loading...