Mabinti hawa huolewa na baba zao! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabinti hawa huolewa na baba zao!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 2, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Taarifa za kitafiti ambazo zimeripotiwa kwenye jarida la Evolution and Human Behavior, zinaonesha kwamba, mtoto wa kike ambaye ana uelewano wa karibu sana na baba yake utotoni, akija kuwa mkubwa, bila kujua atakuja kuvutwa na mtu ambaye anafanana sura na huyo baba yake.
  Baadhi ya watafiti wanasema, labda hapo ndipo mahali ambapo panachimbuka ile imani kwamba, mtu na mkewe wakiishi kwa muda mrefu huja kufanana.

  Pengine siyo suala la muda mrefu, bali zaidi ni kwamba, mwanamke ambaye anafanana na mumewe ni mwanamke ambaye alipokuwa mdogo alipendwa au kuelewana sana na baba yake.
  Watafiti wengi waliofanyia kazi suala hili wanasema wamegundua kwamba, mtoto wa kike ambaye hakuwa na uelewano mzuri na baba yake, kwa kawaida havutwi kabisa na wanaume ambao wana sura kama ya baba yake.


  Labda hii inaweza pia kuelezea ni kwa nini baadhi ya wanawake wazuri sana huolewa na wanaume ambao ni wabaya wa sura (kama jamii inavyowahukumu). Ni kwamba, inawezekana baba yake msichana alikuwa na sura nzuri na hawakuwa na uhusiano mzuri. Ni wazi, mwanamume mwenye sura ya aina ya baba yake hatamvuta. Lakini, hapa inategemea uzuri huo ulikuwaje, kwa sababu anachofuata msichana siyo uzuri au ubaya wa sura, bali sura inayofanana na ya baba yake au isiyofanana na ya baba yake.

  Lakini, kama mtoto wa kike alielewana sana na baba yake ambaye ana sura mbaya kwa mujibu wa vipimo vya jamii, atajikuta akivutwa na wanaume wenye sura kama ya baba yake (mbaya) ambapo itakuwa rahisi kwake kuolewa na mmoja kati yao na siyo na wale wenye sura nzuri.
  Hebu fikiria kuhusu mtoto wa kike ambaye anafanana na baba yake, halafu anaelewana sana na huyo baba.


  Ina maana kwamba, atakuja kuolewa na mwanamume ambaye siyo tu kwamba, anafanana na baba yake, lakini pia ambaye anafanana naye (mwanamke). Kwa kuwa kuna idadi kubwa ya watoto wa kike wanaofanana sura na kuelewana na baba zao, ina maana ndoa za wanaofanana nazo ni nyingi. Lakini, je utafiti huu unataka kuwafundisha wale akina baba ambao jamii inawahukumu kwamba, wana sura mbaya, kutokuwa karibu na watoto wao wa kike ili kuwaepusha kuja kuolewa na wanaume wenye sura kama zao? Bila shaka hilo si lengo la utafiti huu.

  Inaelezwa kwamba, suala ni yupi mzuri kwenye ubongo wa binadamu, halipangwi na wale tunaowaona, bali zaidi hupangwa na wale ambao tulikuwa na uhusiano nao wa dhati na mzuri sana tulipokuwa wadogo. Hapa, baba kwa mtoto wa kike ndivyo ilivyo.
   
 2. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Utafiti huu umekosa vigezo vya kiutafiti:
  1.Hakuna source
  2.Sample ni ipi?
  3.Nani kaufanya?
  Humo mwenye nyekundu nimeshindwa kuunganisha LOGIC..kwa kuwa una'lack' vigezo nilivyovitaja basi nitarudi kuchangia kama mawazo yako tu..
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Anaolewa na baba yake au anaolewa na mtu anayefanana na baba yake?
   
 4. Imany John

  Imany John Verified User

  #4
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  ooh!

  LittleX.
   
 5. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,643
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Ndugu nadhani kwa wanasaikolojia wanaweza kusema kwa lugha fupi defence mechanism, ambopo the Ego component of personality inafel kukontrol other component{ Id and Super Ego} kinachotokea hapo kama kushindwa kwa Ego ni matokeo ya hilo jambo ambapo kitaalamu huitwa Sublimation. Sio hivyo tu bali pia Repression, projection, au regression huweza tokea kwa mtu huyo. Huu ni kwa mtazamo wa Psychoanalytic point of view!
   
 6. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,643
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Pumbatupu, Huo utafiti si kwamba mtoa mada kaubuni. Hilo ni swala la kisaikolojia. Jaribu kupitia Human development.; Freudian Theory{ psychoanalytic point of view} Wenda waweza ona hicho ulichokiita LOGIC!
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  duh...........................
   
 8. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kumbe ndio maana.......
   
 9. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sijui mi kilaza!
  Sijaelewa kitu hapo!
   
 10. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2011
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  This is true na kwa muda mrefu criteria zangu kwa wanaume zilikua ni kumfanana baba na I was very aware of that. Until 10 years ago ndio niliweza kutambua from my own point of view. Zaidi ya sura nilikua naona tabia nzuri ni ile ya baba (hata kama ilikua sio nzuri sana) na mwanaume hata awe na quality gani, kama sio quality ya baba nilikua naona anatafuta sifa ao anajifanyisha tu but siwezi kumsifia.
  It took some time and effort to set me free from it. Mbaya zaidi ni kwamba I was not the favorite daughter of Dad... Maybe this explains that?
   
 11. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Nini tena???
  Gaga inakugusa nn?
   
 12. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  Kumbe......
   
 13. gwahe

  gwahe Senior Member

  #13
  Jan 25, 2015
  Joined: Nov 24, 2014
  Messages: 147
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Post nzuri sn, nitakuja kuchangia ktk mtazamo chanya. Hasa kwenye hili la wanawake wazuri kuolewa na wanaume wabaya.
   
Loading...