Jamani tuacheni stereotypes hizi. Mimi nawajua mabinti wa huko zaidi ya mmoja wako fresh tu, wachakalikaji.
Tena mmoja alikuwa hajaridhika na kazi ya mumewe, mumewe akawa yuko poa tu, binti ndio ikawa kama kazi yake kutuma ma application, mpaka jamaa kaitwa kwenye interview kapiga mzigo akawa anachukua usawa karibu mara tatu wa awali.
Sasa binti kama huyu mpenda maendeleo na mchakalikaji, anajua hata kumsaidia mumewe kama mumewe hachangamki, unaweza kumsema vibaya kweli?
Halafu mtoto ana heshima zake zote kitu ambacho ni nadra sana kupata siku hizi.
Sasa nikimkumbuka huyu binti halafu nikisikia watu wana generalize mambo kama hivi, najisikia vibaya sana.
Watu hawako monolithic kufuatana na makabila yao, na habari yoyote inayo generalize tabia za watu kwa makabila inabidi angalau iwe qualified zaidi.