Mabilioni ya miaka 50 ya uhuru.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabilioni ya miaka 50 ya uhuru..

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ngoshwe, May 29, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wakati Serikali ikijua kuwa mwaka huu ilijipanga kusherehekea miaka 50 ya uhuru kwa kishindo, maandalizi hayo hayakuwekwa kwenye bajeti inayoishia mwezi juni 2011. Cha kusikitisha, wakati Bunge liliidhinisha bajeti iliyoombwa na serikali kutumika kwa shughuli za maendeleo, Serikali imwitisha toka ktk bajeti za Wizara na taasisi nyingine za umma fedha nyingi ili ziweze kutumika katika maandalizi ya sherehe za uhuru. Maaumuzi haya yanafanyika ktk hali ambayo aijulikani iwapo kibali cha Bunge kimetolewa ili fedha hizo zitumike nje ya malengo yaliyoidhinishwa awali. Pengine ktk mazingira haya ya nchi kukosa huduma muhimu za jamii kma maji, barabara, shule, zahanati, waalimu, vitendea kazi,na ktk hali ambayo wafanyakazi wanalalamikia mishahara duni nk, kuna haja gani kufanya sherehe za mbwembwe kuazimisha matatizo? Kwa nini fedha hizo zisitumike kusaidia sehemu ya maendeleo!?
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Huu ni wizi!! serikali inatuibia live! Kubadilisha mipangilio ya bajeti bila idhini ya bunge ni WIZI
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  May 29, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Improvident use of taxpayers' money. Something which we are very good at.
   
 4. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  hakuna haja ya kufanya sherehe ya miaka 50 kwa bajeti kubwa kwa kuwa hiyo itakuwa kuharibu pesa yetu walipa kodi.nashauri tu kwamba pesa iliyopangwa kutumika kwa shughuli hii ielekezwe kwenye vitu vingine vya msingi..
   
 5. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Serikali ya ajabu sana hii, inajivunia umri wa uhuru bila kutafakari maendeleo yaliyopatikana tangu tupate huo uhuru
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Walioko Madarakani wote muda wote wanatumia kufanya sherehe tuu, hawaangalii shida za wananchi wa kawaida, hasa huyu ****** naona anashabikia saaaaaaaaana sherehe nadhani ni tabia za kule bwagamoyo!
   
 7. Bushloiaz

  Bushloiaz JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hii nchi sijui viongozi wetu wanatumia nn kuwaza
   
 8. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160

  Sote tubane matumizi kivitendo;-

  1. Tuache kuchangia sherehe za harusi
  2. CDM wakome kuchangia pesa kwa ajili ya maandamano
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  May 29, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna ishu ya maana sana iliyofanyika ndani ya miaka 50 hadi hizi sherehe ziwe spesho?
   
 10. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180

  Maandamano ya Chadema kwa mtazamo wangu ni Mwamsho wa Watanzania. Ni hatua muhimu kwa wananchi kutambua kwamba uongozi uliopo umewagawa kwenye makundi ya WANANCHI, WENYENCHI NA WALANCHI. Hili ni la Muhimu sana na gharama yake inakubalika

   
 11. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,067
  Trophy Points: 280
  Nabashili kuwepo na vikundi 50 vya ngoma maana bila ngoma maisha ya ****** yanakuwa ya mashaka matupu,hata kufungua vyoo lazima ngoma ichezwe,hapo ngoma ndo special!
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Sherehe za miaka 50 ziwe ni kusafisha miji yetu ambayo imekithiri kwa uchafu na Viongozi wote washiriki katika kampeni hiyo usafi ikiwemo pia Wananchi. Kampeni hiyo ili ifanikiwe inabidi iwe ya miezi mitatu kuanzia September 9 mpaka December 9 na kisha iendelezwe Kitaifa kila mwaka kwa miezi yote 12 ili kuhakikisha miji na majiji yetu yanakuwa safi na hivyo kupunguza sehemu za kuzaliana mbu na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa magonjwa ya malaria, kipindipindu, kuharisha ambayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na uchafu uliokithiri.
   
 13. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wakuu imetengwa shilling ngapi kwa ajili ya sherehe hiyo?
  1.Ntapata hiyo tenda hata ya ku-supply maji? jibu ni NO
  2. kutakuwa na bilau uwaja wa taifa? jibu ni NO.
  3.Raia wote siku hiyo tutapata maji? No Usafiri? No
  SO money for what?

  Anyway shughuli/uratibu upo chini ya wizara gani? maana haya ma wizara hata hayajulikani
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Mkuu unadhani hawa mafisadi watasema zimetengwa kiasi gani kwa sherehe hizo!? Hawatasema maana hapo ndipo kutakuwa na wizi wa hali ya juu kama walivyopora hazina katika uchaguzi wa 2010 na sasa nchi imefilisika hakuna hata pesa za kulipia mishahara Wafanyakazi. Tunaweza kuambiwa wametumia bilioni 200 lakini ukiomba uthibitisho wa hizo bilioni 200 zimetumika vipi wataanza kung'aa macho.
   
 15. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli ni fedheha kwa wananchi, serikali kutumia mabilioni wakati kuna shule zina madarasa, nyumba za waalimu za tembe na hamna mashimo ya kutosha ya vyoo, watoto wa shule wanasoma wakiwa wamekaa chini, vitabu hamna mashuleni, maabara shule za sekondari hamna na zile zenye nazo hamna vifaa, je sekta ya afya ikoje??? Huu ni WIZI WA KODI YETU ili wachache wale na kujinufaisha

  Sasa hivi kweli ukimuuliza mtanzania ambaye ni mlalahoi mvuja jasho kama kuna haja ya "kuchoma" mabilioni yote hayo kwa kisingizio cha miaka hamsini huku miradi ya maendeleo imekwama, sekta ya elimu na afya ni HOI, kweli mtanzania huyu anaweza kunyanyua nyundo au panga na kukata mtu kichwa.

  Kimsingi hawa viongozi wetu kama wangekuwa na akili timamu wasingefanya sherehe ya miaka 50 badala yake wangetumia mabilioni hayo kufanya/kuanzisha miradi ya maendeleo kesherehekea miaka 50 ya uhuru, wananchi wote wangewapa 'big up'.
  halafu kumbukumbu zinasema tulifanya sherehe kubwa sana ya miaka 45 uhuru na zilitumika karibu bilioni 50, viongozi wengi sana wa afrika walihudhuria, sasa tena leo sherehe ya miaka 50, hainiingii akilini kabisaaaaa, ni ukichaa huu
   
 16. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kusherehekea Uhuru ni muhimu, ubunifu unahitajika kufanya maadhimisho, si lazima kila kitu watu tupinge! Sherehe hizi zina maana kubwa kiutamaduni, kujamii na kiuchumi, tukijitafakari upya, it can't pass unmarked! Unless we don't want to reflect the past and refine our way foward!
   
 17. p

  plawala JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatuhitaji hela nyingi
  Tusherekee kwa kuorodhesha makosa makuu 50 ambayo tumetenda kama taifa kwa miaka 50 iliyopita na kuapa kwamba hatutayarudia kwa kuweka sheria ndani ya katiba mpya

  Kosa la kwanza: Kuruhusu nchi yetu kukabidhiwa baadhi ya viongozi wakuu dhaifu sana.
   
 18. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Uhuru tuusherekee kwa njia nyingine inaweza kuwa kwa kuhudumia wasi jiweza, kusafisha makazi yetu, kujitolea damu, kutembelea wafungwa n a hata kutoa msamaha kwa baadhi ya wafungwa hii itangalia nature ya makosa yao. Huu npango wa kutupeleka uwanja wa uhuru nakutupigisha jua pale na wengine wale posho ni WIZI mchana kweupe
   
 19. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Japo Bunge la jamhuri linajigamba kuwa huru, lakini mara kibao limekuwa likiburuzwa na Serikali (Executives) hasa ktk masuala ya matumizi ya fedha za umma. Serikali imekuwa ikitumia Bunge kupitisha mambo yke hasa bajeti lakini ikiidhinishwa matumizi huwa tofauti kabisa, fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya ununuzi wa madawa ya hospitali utakuta zinatumika kwa posho na safari za mganga mkuu. Ona semina elekezi za hivi karibuni zimegharimu fedha kibao za umma lakini ukisoma ktk bajeti iliyopitishwa na Bunge huwezi kukuta bajeti line ya kufanyia semina mawaziri na makatibu wakuu. Kati ya mwezi Januari na Machi
  Hazina walikata juu kwa juu baadhi ya bajeti za mawizara na wamesitisha kutoa mafungu ili zilizobaki ziingie kwenye kapu la sherehe za uhuru. Inaonekana hakuna mipango ya maana ya watendaji wetu. Nini maana ya bajeti kma mambo yanafanyika kihivi?!
  Hatuwezi kuwa na maendeleo yoyote kwa mfumo na muundo wa Serikali yetu hivi sasa ambapo Rais wa jamhuri ya muungano ndie kiongozi wa kila kitu,
   
Loading...