Mabilioni ya mababu zetu waliofariki kabla ya kuletewa Uislam kwasasa Wapo Motoni au peponi?

Mi ibada hua nashiriki mara moja moja ili nsitengwe sana na jamii ila kwa kwel hamna nachopata cha maaana
Mkuu kama bado unaogopa kufa na unatamni kwenda mbinguni ni bora uboreshe mahudhurio yako ,kwa sababu kujitambua ni njia ngumu kuliko kuokoka 😁😁😁
 
Mkuu kama bado unaogopa kufa na unatamni kwenda mbinguni ni bora uboreshe mahudhurio yako ,kwa sababu kujitambua ni njia ngumu kuliko kuokoka 😁😁😁
Mimi kuacha kbs ni ngumu na kuboresha mahudhurio ni ngumu, Bado najitafuta nashikwa Mkono na Mzee na yy ni mtu wa church sana asije akantosa kisa nimeacha imani
 
Hukumu itategemea dhamira ya tendo; Sheria ya dini haitatumika kwa wale ambao Elimu ya dini ilikuwa haijawafikia.
Mfano; Kama muongozo wa dini haukuwepo, huwezi kusema kwa mfano mtu amefanya kosa kwa kunywa pombe
Ok sawa, tuchukulie mfano mtu ambaye tayari amefikiwa na elimu za dini lakini akuzifuata kutokana na sababu mbali mbali lakini matendo yake yamebeba thawabu. Je, huyu atawekwa kundi gani?

Mfano, leo migogoro mingi inayoikumba dunia chanzo ni siasa na dini, wakati lengo hasa la waanzilishi wa hizi dini ni upendo( dini zote zimenzishwa na wanadamu ), sasa kutokana na mkanganyiko huo mtu akaamua kuishi maisha yake nje na dini lakini anamwini Muumba na kufuata mapenzi yake. Je, kwa kutumia akili unafikiri huyu mtu atapewa hukumu ya kutokufuata sheria za dini ama kulingana na matendo yake?
 
Mara kwa mara nimekuwa nikiona hili neno kuwa mnasema mara nyingi Uislam ni Dini ya haki na sometime mmekuwa mkiwaita Dini nyingine Makafiri, hayo maneno yamekuwa ukinitatiza sana

Lakini mimi nachotaka kujua ni kwamba Mababu zetu kabla ya kuja wa Waarabu walikuwa na imani zao na maisha yalienda, Mabilioni ya mababu zetu walishafariki kabla ya Mwarabu kuja kuwasilimisha waliokuwa hai kwa wakati huo na ndio nyie leo mnaitwa Waislam.

Swali langu ni moja tu, Mabilioni ya mababu zetu waliofariki kabla ya kuletewa Uislam kutoka Saudi Arabia kwa sasa Wapo Motoni au Wapo peponi?

Na kama wapo Motoni kosa lao ni lipi?
Soma biblia Yud aya 1 ,4 Makafiri NI kina nani


Yuda 1 -4
Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.
 
Nikusaidie kwa elimu yangu ndogo ya uislam ni kuwa,

Kuna kundi la wanadamu siku ya qiyama watapewa mtihani wao kupimwa wanamuamini Muumba? Yaani wakifufuliwa kabla ya kuona pepo wala moto watakuwa na ulimwengu wa mtihani.(Kumbuka neno akhera ni idadi kubwa ya mi-ulimwengu) Wataoamini peponi na wataofeli motoni.Hao ni lile kundi waliishi bila kufikiwa na ujumbe wa dini mfano wakazi wa amazon kati kati huko au mfano mambabu zetu.


Ama tuliobaki na kufikishiwa ujumbe tutahukumiwa kwa kadiri tulivyofanyia kazi ujumbe
Una dalili kuhusu hiki ulichokiandika hapa?
 
Umeulizwa Swali zuri;
Kwanza nikukumbushe tu kuwa, mfumo mzima wa maisha ya Kawaida ya Binadamu hata bila kujua Uislam tayari unatosha kabisa kuwahukumu watu.

Mfano: Kwani Inahitaji dini kujua kuwa kufanyia Binadamu mwenzako jambo la kumuumiza kwa maksudi ni jambo baya? nk nk

Ninachomanisha ni kuwa: Matendo ya wale waliotangulia yata angaliwa uhalisia wake kufuatana na mazingira/Nyakati za kipindi chao walicho ishi. Kwa yale makosa yaliyofanyika kutokana na kutokuwepo na muongozo (Elimu) ya Uislam nyakati hizo mfano; Kunywa Pombe nk tuna amini kabisa kuwa, Mungu wetu Mwingi wa rehma atawasamehe
Una dalili kuhusu hiki ulichoandika hapa mkuu?
 
Kwanini hakuna taarifa yoyote ya kihistoria inayotaja uislamu kabla ya ujio wa Muhammad. Hata uarabuni penyewe waliishi wapagani na miungu yao e.g. Hubal, Al-Uzza, Manat

Kina Musa, Ibrahimu, daudi msiwaibe walikuwa Jewish na walifata sheria za Yahweh mungu wa waisraeli na alikuwa na taratibu tofauti na Allah.

Kwa hiyo kuhusu uislamu kuwepo toka mwanzo wa Dunia sio kweli
hapa kila mtu anafata maandiko boss,nimekujibu kwa maandiko na ukisoma bibilia utaona maneno yanataja mungu wa yakobo,mussa,daudi na isaya je,sisi wengine sio mungu wetu?

mungu wa israel,je mataifa mengine siyo yetu?inaonekana wanaemuabudu wakristo ni mizimu ya israel na siyo nguvu kuu ya dunia.

hizi dini,kila mtu anaasili yake.
 
Kwahiyo uislamu ni dini ya kutungwa na nijuavyo Mungu yupo toka kuumbwa kwa dunia iweje bara la afrika ndilo liwe bara la kuletewa dini kwann huyo muhamadi asingekuja kutangaza dini ya haki hadi huku afrika?
walikuja maswahaba huko ethopia mpk afrika mashariki,pia mtume kuna kisa alitaja nchi ya ethopia kwa jina la abu thania kama sikosei baada ya kuona manaswala/ahlu kitab u wananyanyasika akawaambia waende nchi ya mashariki ya mbali kuna mfalme anaongoza vizuri.
 
Mkuu hakuna watu ambao walikuwa ni wenye imani kubwa kama wazee wetu, Uislam umeingia dunia kuanzia 610 CE. Mababu walikuwa wanafahamu namna ya kuishi, na kuabudu! Ni ngumu kuamini kuwa wapo motoni kisa tu Sheikh fulani kasema kuwa Quran imeandika hivyo. Ni uongo na uzushi! Mpaka sasa kuna karibu imani 4,000 (Elfu 4) zinazotambulika kote ulimwenguni. Hata hivyo, 75% ya watu wamefuata imani kuu tano ambazo ni pamoja na Ubudha, Uhindu, Ukristo, Uyahudi, na Uislamu. Sasa kusema kwamba Wahindu wataenda motoni kwa sababu Wabudha wanaamini hivyo sio sawa! Kusema kuwa Wakristo wataenda kwa sababu katika Kojiki na Nihon Shoki wao Washinto wanaamini kuwa Wakristo ndo wakosefu, sio sahihi!
Binafsi ninaamini kwenye dhana ya reincarnation na hata kwenye kabila langu, nimewahi kuongea na wazee wanakasema kuwa hiki kitu kipo na kitaendelea kuwepo. Ila sio kwenye dini ambazo msingi wake mkuu ni kwenye kuumiza dini zingine. "No Religion is Perfect, All Religion are Perfect"
 
Mara kwa mara nimekuwa nikiona hili neno kuwa mnasema mara nyingi Uislam ni Dini ya haki na sometime mmekuwa mkiwaita Dini nyingine Makafiri, hayo maneno yamekuwa ukinitatiza sana

Lakini mimi nachotaka kujua ni kwamba Mababu zetu kabla ya kuja wa Waarabu walikuwa na imani zao na maisha yalienda, Mabilioni ya mababu zetu walishafariki kabla ya Mwarabu kuja kuwasilimisha waliokuwa hai kwa wakati huo na ndio nyie leo mnaitwa Waislam.

Swali langu ni moja tu, Mabilioni ya mababu zetu waliofariki kabla ya kuletewa Uislam kutoka Saudi Arabia kwa sasa Wapo Motoni au Wapo peponi?

Na kama wapo Motoni kosa lao ni lipi?
wapo peponi mkuu,sababu hukumu na sheria zilikuja baada ya vitabu vya mitume hivyo adamu hakupewa ila alipewa agano la uumbaji,mpk ikafika kwa mtume ibrahimu hivyo kwa wale ambao walifikiwa na ibrahimu watahukumiwa kwa sheria za ibrahimu.

waislamu kuwaita watu makafiri sio kosa lao ila mfumo wa mafundisho kuwa yeyote asiye swali ni kafiri kwahyo hata mtu akiwa na jina la kiislamu na haswali huyo ni kafiri,aMEkengeuka mafundisho ya mtume.
 
Umeuliza swali zuri na tayari swali hili lilikwisha jibiwa na mtume wetu muhammad (peace be upon him) inshaallah nitajitahidi kulijibu kwa kadiri nitakavyo afikishwa .

amaba'ad
Kwanza nianze ni ufunguzi wa surat isra aya ya 15 Allah(the almighty anasema)

Al-Isra' 17:15

مَّنِ ٱهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِى لِنَفْسِهِۦۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَاۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰۗ وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا

Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani

Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume.

Hapo kwenye maandishi myekundu Allah(the all knowing) anasema hatomuadhibu yeyote mpaka amtumie mjumbe (mitume na manabii) tena hao mitume na manabii wanatoka katika jamii ya hao hao watu i.e binaadamu .

kutoka kwa Al-Aswad ibn Sari (radhialahu anhu) anasema
Ameeleza mjumbe wa Allah(the almighty) , siku ya qiyama kutakuwa na watu wanne ambao wao watamlalamikia Allah( the almighty) na watu wanne hao ni Kiziwi, Mtumzima mzee sana( kufikia hatua kumbukumbu zinaanza kupotea), mwendawazimu na mtu aliyeishi zama baina ya nabii isa(peace be upon him) na mtume muhammad (peace be upon him) , kiziwi atasema ewe mola wangu ujumbe ulikuja lakini sikusikia kitu, mtu mzee sana atasema ewe mola wangu ujumbe ulinijia nami sikuelewa kitu (sababu ya kusahau kutokana na uzee) ,mwendawazimu atasema ewe mola wangu ujumbe ulinijia lakini watoto walikuwa wakinikimbiza na kunitupia mawe (kutokana na uendawazimu wake pia asingeweza kusoma na kuelewa) na yule aliyeishi baina ya nabii isa (peace be upon him) na mtume muhammad (peace be upon him) atasema , ewe mola wangu hakika sikujiliwa na mjumbe yeyote kutoka kwako .

Basi Allah (the almighty) atakubali malalamishi yao kisha atawapima kwa kuwaambia waingie motoni , kisha wale watakaouingia moto bila ya kubisha wala kusita ule moto utakuwa baridi na salama kwao na hao wameonesha imani yao kwamba wangemkubali mjumbe na wametii kauli ya moja kwa moja ya Allah (the almighty) hawa wataingia peponi.

Wale ambao watakataa basi watavutwa kwa nguvu kuingizwa motoni kwa sababu wameikataa kauli ya moja kwa moja ya Allah( the almighty) hii inaonesha hata mjumbe wangempinga pia na hao wataaadhibiwa motoni.

Hadithi hii ni swahihi na inapatikana katika (sahih al jami , 881) .

Kwa hivyo mpaka hapa tunapata kwamba wale ambao walijiwa na mjumbe na wakapata ujumbe ukiwa wazi kisha wakaukataa Hawa wataishia motoni na wale ambao hawakuupata ujumbe katika makundi hayo manne hapo juu kama ilivyoelezewa kwenye hadithi hiyo basi hawa watapewa mtihani siku ya qiyama .

Ama tukirudi kwenye swali lako sasa kama kuna watu baada ya mtume muhammad(peace be upon him) kuja na wao hawakufikiwa na ujumbe basi hawa wanaingia katika makundi hayo hapo juu means watapimwa siku ya qiyama.

Na Allah (the all knowing) anajua zaidi.
 
Tukubali tu kuwa tulizidiwa mbinu na wenzetu kutulazimisha imani na mfumo wao wa maisha wakati sisi tuko na makabila mbalimbali na kila kabila inafanya siri mambo yao ya imani kwa makabila mengine au ukiwa kabila lingine ni mwiko kushiriki. Walituweza hapo. Na hata huku kwa waafrica tuna mitume mingi sana na walikufa bila kuwa na record ya aina yeyote.

Wenzetu waliweza kutunza kumbukumbu na walifundisha lugha yso na imani yao kote ulimwenguni.
 
Ibrahim sio Muebrainia ni Miraq tena Muislamu
Ibrahim kwenye Safari yake alichukua Watu wengi waliobaki upande wa juu wa mto Jordan waliitwa Waebrania (Waliobaki upande wa kaanani, hawakuvuka Jordan kuelekea Eneo la Nchi ya Jordan).

Maana ya Neno Ebrania limetokana na neno "Eber" other side of the river.

Ibrahim hakuwa Muiraq, neno Iraq neno jina jipya lilitokena na Mji uliokuwa unaitwa Uruk, Leo linaitwa Warka kwa Kiarabu, Ibrahim alitokea nchi inaitwa Ur, walikuwa wanakaa Watu wanaitwa Wakalidayo, Ibrahim either alikuwa ana Asili ya hao Watu Wakalidayo au Muakediani.
 
Kwa kukusaidia tu, sheria haiwezi kumuhukumu mtu ikiwa bado haijatungwa.

Uislamu umeanza kwa Muhammad japo inasemekana toka kuumbwa kwa mwanadamu, ibrahimu,musa,daud,issa na muhammad wote walibeba mafundisho ila hapa Muhammad kayakusanya yote na katika kitabu cha Quran kimekuja kueleza hukumu(dhambi/baya au thawabu/zuri).

Ikaja kuelezea ni njia zipi atapitia watakaovuna hizo dhambi na thawabu na mwisho ikaelezea mambo ya siku za mwisho/kiyama.

Sijui kama nimekujibu
Aha
 
Back
Top Bottom