Mabilionea sio kitu vizuri kwa taifa

Ikulumaliyawananch

JF-Expert Member
Mar 14, 2018
339
533
Mabilionea sio kitu kizuri kwa taifa.

Screenshot_20191111-223944_Twitter.jpg
 
Mabilionea sio kitu kizuri kwa taifa.

View attachment 1261012
huo ndio ukweli sema tu watu wengi hawaeliwi watu wanawezaje kuwa mabilionea. nilisha wahi kupost kuwa mabilionea hawana tafauti na madictator watu wakapinga ila miaka ishirini ijayo kama mabilionea watazidi kuongezeka tutegemee umasikini kuongezeka ulimwenguni.Mfano mzuri ni marekani, ambako mabilione wanaongezeka kwa kasi kubwa na idadi ya watu wanao shuka kutoka kipato cha kati na kuingia level ya umasikini inaongezeka na masaa watu wanayo fanya kazi inaogozeka kwa kasi. pia hali ya tofauti kati ya masikini na tajiri inazidi kupanuka kwa kasi ya ya ajabu.
 
Huyo mbunge yupo negative sana. Atupe list ya mabilionea ambao wamepata ubilionea wao kwa kuwanyonya wananchi wenzao.
 
Ubatili mtupu, huku tunapimana kwa Tsh. Wao wanapimana kwa ela zenye thamani kubwa kuliko zetu, Mabeberu hawana akili, utajiri wa ukweli ni kilimo na mifugo
 
Huyo mbunge yupo negative sana. Atupe list ya mabilionea ambao wamepata ubilionea wao kwa kuwanyonya wananchi wenzao.
Anachozungumza ni kweli wewe hujui uliza tunaofanya kazi kwenye makampuni ya watu full mnyonyo hadi sio poa
 
Kwa sasa zaidi ya nusu ya utajiri wa dunia unamilikiwa na asilimia moja tu ya watu. Hawa ndiyo mabilionea na mamilionea wa dunia.
Screenshot_20191114-143004~2.jpeg


Hoja ni kwamba hali hii ikiendelea kutakuwa na matatizo huko mbele ya safari hasa ukizingatia misukosuko inayotabiriwa kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanatazamiwa kuleta kasoro kubwa katika upatikanaji na usambazaji wa chakula, maji na huduma zingine muhimu. Pia kuna misukosuko ya kiuchumi, uhasama wa kibiashara pamoja na kumalizika kwa malighafi zinazotegemewa na mataifa mbalimbali. Ukiangalia kwa undani hata misukosuko mingi ya kisiasa inayotokea katika nchi nyingi (mf. Lebanon, Argentina, Bolivia) chimbuko lake ni mgawanyo mkubwa wa matabaka. Unakuwa na mabilionea wachache wanaomiliki kila kitu halafu 99% ni masikini hohehahe. Hawa 99% inafika mahali wanachoka wanaamua kuingia mitaani wakilaumu wanasiasa waliopo madarakani japo ukiangalia kwa undani sababu hasa ni za kiuchumi. Wenyewe wanasema mfumo huu hauko sustainable hasa huko mbele ya safari ambako vikwazo vinavyoikabili dunia ni vingi. Ogopa sana mtu masikini mwenye njaa aliyekata tamaa.
Billboard%2C%20oneday%20the%20poor%20have%20nothing%20to%20eat%20but%20the%20rich.jpeg
 
Back
Top Bottom